Umoja wa Machifu mkoa wa Mara watoa ONYO kwa wanasiasa wanaotoa matamshi ya kutotambua umuhimu wa Machifu nchini

Machifu wanaitisha press conference nawao! Maendelea ya Awamu ya sita
 
Hangaya kayatafuta mwenyewe na huu ni mwanzo,ipo siku machief wenzake watamgeuka tu.
 
Machifu wana umuhimu gani karne hii zaidi ya kujihusisha na uchawi, ushirikina, uganga na matambiko...........mkiendekeza mambo kama haya mtarudi zama za mawe na maendeleo yatakuwa ndoto.
 
Kuna wale wachawi 900 wa Simiyu walinzi wa jiwe sijui waliishia wapi
 
Machifu wana umuhimu gani karne hii zaidi ya kujihusisha na uchawi, ushirikina, uganga na matambiko...........mkiendekeza mambo kama haya mtarudi zama za mawe na maendeleo yatakuwa ndoto.
True tena ndio waliowauza mababu zetu kwa wakoloni.
 
Umoja wa Machifu Mara umekutana na vyombo vya habari nakutoa Onyo kwa baadhi ya Wanasiasa wanaotoa matamshi ya kuonesha kutotambua umuhimu wa Machifu nchini na kuwasihi watanzania wawaone Wanasiasa hao kama watu wenye nia ya kuvunja umoja wa kitaifa.

Pia soma > Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Mara, Japhet Wanzagi amesema kuwa kama mnavyojua Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mkuu wa Machifu wote nchini kwa jina la Chifu Hangaya sisi kama Machifu wa mkoa wa Mara tumejipanga kumpokea Chifu wetu.

Kuna mtu alikuwa anasema Machifu hawakuwepo, machifu walikuwepo muda mrefu tangu kipindi cha mkoloni. Mtu anayesema Machifu walipandikizwa na mkoloni na wakaondolewa na Baba wa Taifa huyo ni muongo.

Machifu walitolewa kwenye mamlaka ya Serikali lakini walirudi kuwa viongozi kwenye jamii zao, ila katika kipindi cha awamu ya Sita, Rais Samia ametupa heshima sana Machifu.

Majukumu yetu makubwa sisi Machifu ni upatanishi hasa kuanzia ngazinya familia mpaka ngazi ya mamlaka za juu na mara nyingi uwepo wetu umesaidia kutatua migogoro kwenye jamii zetu.

Naye Dkt. petter Makomara ambaye ni msemaji wa kabila la Wasorwa amesema kuwa

Sisi Machifu wa Mara tunamuahidi Chifu wetu Hangaya ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa tutaendelea kulinda amani yetu ili kupunguza matukio ya kiuhalifu kwa Mara.

Kuna rasimu inashughulikiwa ipo Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo itatuhusisha sisi Machifu hasa kwenye migogoro na mwisho wa siku tutapunguza baadhi ya matukio ya jinai.

Chifu wa Kiseru Rorya, Msangia Ngoje yeye amedai kuwa kuna watu wanaandika mtandaoni na kutukosea heshima Machifu, wengine tunawafahamu wana laana kweye koo zao huko nyumbani, ndio maana kila siku wanaongelea Dar es Salaam mara Morogoro au mtandaoni na nyumbani kwao hawaendi.

Tunashauri inapotokea matukio ya kijinai viongozi wa kiusalama wa mkoa waje kutufuata Machifu ili tuweze kukemea na kuondoa laana kwenye hizo koo.

Mwisho.
Hawa machifu ni wajinga sana,kwani hawajui kuwa sheria ndio haitambui uwepo wao...fools!
 
Inasikitisha kuona mambo kama haya yakifanyika in the name of kutaka kukubalika.
Watu wa MARA notably Wakuria wao wenyewe VITA vya Clanism/Kiukoo haviiishi miaka nenda miaka rudi.
WANYABASI,
WAIREGI.
WAKIRA na vi ukoo vingi na wote hawaelewani. Ni kama maji na mafuta. Kwa kifupi basi hawa watahitaji basi CHIFU wa kila Ukoo. Maana Ukoo mwingine hawatakubali matatizo yao yasikilizwe na Chifu asiye Ukoo wake. Hii ni hatari sana. It is impractical n dangerous. Angalia mfano wa SOMALIA LUGHA ni moja na nchi ni moja ila CLANS/KOO kibao. Hata Ktk uongozi wao ikiwa mtu wa Ukoo wa Isaaq atashika basi hatakubalika na ukoo mwingine kama Darood, Hawiye nk. HAWAELEWANI kabisa. Vita kila kukicha. Sababu tu ya Clanism/Ukoo na kila ukoo una MACHIFU(Akil) nao wameshindwa. Je sisi Tanzania ndo tutaweza? Mh. SSH nenda polepole. Usipokee ushauri potovu. Ongeza na zako basi. La sivyo utalifarakanisha taifa hili na hatimaye kwenda mwendo mbovu kama wa Somalia.
 
Kwa mara ya Kwanza ndo nimesikia kuwa hata rorya Kuna chief.

Sent from my Lenovo TB-7305X using JamiiForums mobile app
Wakati wanachinjana huko Rorya hao machifu walikuwa wapi kutatua Ile migogoro? Washenzi hawa .

Rais amejiingiza kwenye ishu ngumu sana hajui tu balaa analoliandaa. Leo wanatetea uchifu, kesho watataka walipwe hela na baada ya hapo watakosana na baadhi ya maamuzi ya serikali ambayo inaongozwa na huyo chifu mkuu wa mchongo then kinachofuata watasapoti chama fulani na ukabila plus ukanda utashamiri kitakachokuja kutokea huyu mwanamke hatasahau.

Nyerere aliona hilo bomu siku nyingi sana, machifu ni watu wanaosikilizwa sana na wananchi wao, ukianza kurudisha uchifu wallah tutaanza kupeana majimbo ya ubunge kulingana na Koo zetu, kabila na ukaribu ulionao kwa chifu wenu.

Itatokea siku chifu akasimama na mgombea fulani na kuwahimiza wananchi wake wamchague huyo mgombea sijui tutafika wapi??

Itatokea siku chifu mmoja akasimama na kusema watu wake wananyimwa nafasi kwenye uongozi sijui itakuwaje maana hapo itakuwa mpasuko kila mmoja atataka kabila lake liwepo kwenye uongozi wa nchi.

Haya mambo huwa yanakuja kwa stages ambazo jamii inaweza isigutuke mapema, at the end tutajikuta Kama wenzetu wakenya.

CCM kuweni na busara wakati mwingine.
 
Umoja wa Machifu Mara umekutana na vyombo vya habari nakutoa Onyo kwa baadhi ya Wanasiasa wanaotoa matamshi ya kuonesha kutotambua umuhimu wa Machifu nchini na kuwasihi watanzania wawaone Wanasiasa hao kama watu wenye nia ya kuvunja umoja wa kitaifa.

Pia soma > Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Mara, Japhet Wanzagi amesema kuwa kama mnavyojua Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mkuu wa Machifu wote nchini kwa jina la Chifu Hangaya sisi kama Machifu wa mkoa wa Mara tumejipanga kumpokea Chifu wetu.

Kuna mtu alikuwa anasema Machifu hawakuwepo, machifu walikuwepo muda mrefu tangu kipindi cha mkoloni. Mtu anayesema Machifu walipandikizwa na mkoloni na wakaondolewa na Baba wa Taifa huyo ni muongo.

Machifu walitolewa kwenye mamlaka ya Serikali lakini walirudi kuwa viongozi kwenye jamii zao, ila katika kipindi cha awamu ya Sita, Rais Samia ametupa heshima sana Machifu.

Majukumu yetu makubwa sisi Machifu ni upatanishi hasa kuanzia ngazinya familia mpaka ngazi ya mamlaka za juu na mara nyingi uwepo wetu umesaidia kutatua migogoro kwenye jamii zetu.

Naye Dkt. petter Makomara ambaye ni msemaji wa kabila la Wasorwa amesema kuwa

Sisi Machifu wa Mara tunamuahidi Chifu wetu Hangaya ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa tutaendelea kulinda amani yetu ili kupunguza matukio ya kiuhalifu kwa Mara.

Kuna rasimu inashughulikiwa ipo Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo itatuhusisha sisi Machifu hasa kwenye migogoro na mwisho wa siku tutapunguza baadhi ya matukio ya jinai.

Chifu wa Kiseru Rorya, Msangia Ngoje yeye amedai kuwa kuna watu wanaandika mtandaoni na kutukosea heshima Machifu, wengine tunawafahamu wana laana kweye koo zao huko nyumbani, ndio maana kila siku wanaongelea Dar es Salaam mara Morogoro au mtandaoni na nyumbani kwao hawaendi.

Tunashauri inapotokea matukio ya kijinai viongozi wa kiusalama wa mkoa waje kutufuata Machifu ili tuweze kukemea na kuondoa laana kwenye hizo koo.

Mwisho.
Umoja wa machifu wa Kitongo MAGU mkoani Mwanza tunaunga mkono tamko.

Chief Igobeko
 
Inasikitisha kuona mambo kama haya yakifanyika in the name of kutaka kukubalika.
Watu wa MARA notably Wakuria wao wenyewe VITA vya Clanism/Kiukoo haviiishi miaka nenda miaka rudi.
WANYABASI,
WAIREGI.
WAKIRA na vi ukoo vingi na wote hawaelewani. Ni kama maji na mafuta. Kwa kifupi basi hawa watahitaji basi CHIFU wa kila Ukoo. Maana Ukoo mwingine hawatakubali matatizo yao yasikilizwe na Chifu asiye Ukoo wake. Hii ni hatari sana. It is impractical n dangerous. Angalia mfano wa SOMALIA LUGHA ni moja na nchi ni moja ila CLANS/KOO kibao. Hata Ktk uongozi wao ikiwa mtu wa Ukoo wa Isaaq atashika basi hatakubalika na ukoo mwingine kama Darood, Hawiye nk. HAWAELEWANI kabisa. Vita kila kukicha. Sababu tu ya Clanism/Ukoo na kila ukoo una MACHIFU(Akil) nao wameshindwa. Je sisi Tanzania ndo tutaweza? Mh. SSH nenda polepole. Usipokee ushauri potovu. Ongeza na zako basi. La sivyo utalifarakanisha taifa hili na hatimaye kwenda mwendo mbovu kama wa Somalia.

Nyerere angekuwa na akili kama za Hangaya, hii nchi ingekuwa na tribalism mbaya kuliko nchi yoyote ya East Africa!
 
Inawezekana machifu wanatoa ulinzi usioonekana kama ule wa shehe yahya aliomwekea msoga kipindi kileeee, maana hao watu ni ndumba na ulozi kwa kwenda mbele.........
 
Machifu wabakie kama wazee wa kimila tu hawatambuliki kikatiba na wanaweza kuleta ubaguzi ndani ya jamii...malengo ya kuondoa machifu hayajaisha tusigawe nchi yetu vipande vipande kwa mambo ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom