Umoja wa Mataifa wakubaliana kumaliza UKIMWI ifikapo 2030

Umoja wa Mataifa wakubaliana kumaliza UKIMWI ifikapo 2030

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio la kisiasa, la kuyamaliza maradhi ya UKIMWI ifikapo mwaka 2030. Kulingana na azimio hilo wanachama wa baraza hilo kuu wameahidi kupunguza kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI hadi 370,000 na vifo vitokanavyo na UKIMWI hadi chini ya 250,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI, UNAIDS, Winnie Byanyima amesema bado mataifa mengi hayajafikia ahadi zao na kuonya janga la COVID-19 linaweza kuibua upya janga la UKIMWI. Mataifa wanachama yamekubaliana kulimaliza janga hilo kwa kuwafikia asilimia 95 wa watu wanaoishi na VVU, asilimia 95 ya usambazaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU na asilimia 95 ya watu wenye virusi sugu dhidi ya dawa.
 
Umalizwe kwa matamko ya kisiasa...
hawa watakuwa waliuleta ukimwi!!?
 
hii si biashara ya watu, wameridhika kwakwel
tunakoseshana utamu kijinga kisa hili gojwa bora lieshe tu.
maisha yamekua ya mashaka sn ukiuza mechi sehemu zisizo rasmi.
 
Yaani Ukimwi umalizike kwa staili hiyo?mi nikajua chanjo au dawa ipo waanze kupewa wagonjwa
Walikwenda kijijini kufundisha watu jinsi ya kuvaa kondom, ikawa muelekezaji anavaa kondom kidole cha kati huku akisema ukitaka kulala na mama kwanza fanya hivi,
Baada ya miezi sita katika ufuatiliaji wao wakagundua kuna nyumba moja mwanamke
Ni mja mzito, wakamuuluza mumewe kwani hukufuata maelezo yetu? Mume akajibu kuwa hakuna siku ambayo sikufuata katika hii miezi sita, wakamuuliza ulikua unafanyeje? Akasema kila siku nikilala na wife ni lazima nivae kondom kidole cha kati,
Kumbe jamaa alielewa kama walivyoeleza
Anavaa kidoleni anapiga vitu,
Hapo ndio nikagundua lengo lao ni kuzuia watu wasizaliane
 
Back
Top Bottom