Umoja wa Ulaya watoa wito kwa Rais Samia kuanzisha uchunguzi wa haraka kubaini watekaji nchini

Umoja wa Ulaya watoa wito kwa Rais Samia kuanzisha uchunguzi wa haraka kubaini watekaji nchini

View attachment 3092205
10 September 2024

Tamko la Pamoja la Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Uingereza, Canada, Norway na Uswisi kuhusu Matukio ya Hivi Karibuni Nchini Tanzania;

"Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa makubaliano na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Ubalozi wa Canada, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi na Ubalozi wa Uingereza, unasikitishwa na taarifa za hivi karibuni za vitendo vya ukatili, kupotea kwa watu, na vifo vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu. Tunatoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu matukio haya. Tunatoa pole kwa familia zote zilizoathiriwa.

Tunaihimiza serikali ya Tanzania kuhakikisha ulinzi wa upinzani, kama alivyoahidi Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kupitia mpango wake wa "4R", na kwa mamlaka kuchukua jukumu la kulinda haki za msingi za wananchi, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza.

Tunakaribisha wito wa Rais wa kuanzisha uchunguzi wa haraka ili kubaini wahalifu waliohusika na kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Tunatambua kwa wasiwasi mkubwa kwamba matukio haya ya hivi karibuni yanatishia misingi ya kidemokrasia na haki za wananchi wa Tanzania, katika nchi inayoheshimika kimataifa kwa amani na utulivu, na tunaungana na wito wa kulinda amani na utulivu wa nchi."

Soma Pia:
Tanzania pia ni wabobezi kwenye kujiteka, duu hili jibu la watu kujiteka na drama za kujiteka ni fikirishi mno linahitaji mjadala wa kitaifa
 
Jumuia ya Ulaya, Ubolozi wa Uingereza, Canada, Norway na Uswisi, kwa pamoja wametoa tamko la kulaani matukio ya utekaji na mauaji ya wanaharakati na viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani nchini Tanzania.

Katika Tamko lao, wamesema:

TAMKO LA PAMOJA LA WAKUU WA UMOJA WA ULAYA, UBALOZI WA UINGEREZA, NORWAY NA USWISI KUHUSU MATUKIO YA HIVI KARIBUNI NCHINI TANZANIA:
IMG-20240910-WA0011.jpg

Jumuia ya Umoja wa Ulaya, kwa makubaliano na Balozi za nchi ya Canada, Uingereza, Uswisi na Norway, tunasikitishwa na taarifa za hivi karibuni za vitendo vya kikatili, kupotezwa kwa watu, na vifo vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu. Tunatoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu matukio haya. Tunatoa pole kwa familia zote zilizoathirika.

Tunaihimiza Serikali ya Tanzania kuhakikisha '4R', na kwa mamlaka kuchukua jukumu la kulinda haki za msingi za wananchi, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza.

Tunakaribisha wito wa Rais wa kuanzisha uchunguzi wa haraka ili kubainiwahalifu waliohusika, na kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Tunatambua kwa wasiwasi mkubwa kwamba matukio haya ya hivi karibuni yanatishia misingi ya kidemokrasia na haki za wananchi wa Tanzania, katika nchi inayoheshimika kimataifa kwa amani na utulivu, na tunaungana na wito wa kulinda amani na utulivu wa nchi.

Watanzania wenzangu, watu wa haki, wenye mapenzi mema na Taifa letu, watu wanaomwogopa Mungu na kuuheshimu uhai na haki ya kila mwanadamu, tuungane kwa pamoja kuzidi kuchukua kila hatua inayowezekana, ili haya mashetani yanayoteka na kuua watu yasifanikiwe katika ushetani na uhayawani wao.

Linapokuja suala la haki na uhai wa kila mwanadamu, hakuna dini, kabila au mgawanyiko wa vyama, tuungane kwa pamoja dhidi ya hayo mashetani, hata kama hayo mashetani yapo ndani ya chama chako, ndani ya dini yako, ndani ya kabila lako au hata ndani ya familia yako.

Ulimwengu upo nasi tunaotetea haki za msingi dhidi ya maharamia. Watawala wanayo machaguo mawili tu, kusimama na hawa mashetani, waondoke kwenye utawala au kuhamia kwa watu wema dhidi ya maharamia, ili wasimame na wananchi wema.
 
View attachment 3092205
10 September 2024

Tamko la Pamoja la Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Uingereza, Canada, Norway na Uswisi kuhusu Matukio ya Hivi Karibuni Nchini Tanzania;

"Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa makubaliano na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Ubalozi wa Canada, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi na Ubalozi wa Uingereza, unasikitishwa na taarifa za hivi karibuni za vitendo vya ukatili, kupotea kwa watu, na vifo vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu. Tunatoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu matukio haya. Tunatoa pole kwa familia zote zilizoathiriwa.

Tunaihimiza serikali ya Tanzania kuhakikisha ulinzi wa upinzani, kama alivyoahidi Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kupitia mpango wake wa "4R", na kwa mamlaka kuchukua jukumu la kulinda haki za msingi za wananchi, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza.

Tunakaribisha wito wa Rais wa kuanzisha uchunguzi wa haraka ili kubaini wahalifu waliohusika na kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Tunatambua kwa wasiwasi mkubwa kwamba matukio haya ya hivi karibuni yanatishia misingi ya kidemokrasia na haki za wananchi wa Tanzania, katika nchi inayoheshimika kimataifa kwa amani na utulivu, na tunaungana na wito wa kulinda amani na utulivu wa nchi."

Soma Pia:
Watuletee FBI na MI6 ili hawa magaidi wakamatwe na kuwajibishwa ipasavyo.
 
Samia anamchunguza nani?Au kaagiza wamchunguze nani?Sijaelewa,kule chura kiziwi,pale mbwa mpumbavu anabwekea wenye mamlaka,tena yule kibwengo nyooka naye,Bananga naye watalinda viongozi wao kwa damu,uvccm nào wakiwapoteza msiwatafute,ni mengi mno kwa kweli niambieni anamchunguza nani?Tangu kamanda Mawazo kuuawa,kutekwa Ben Saanane hadi Roma mkatoliki,Sativa,Soka na wenzake ,ni nani wanamchunguza?
 
Huko kwao hakuna kutekana

USSR
Huko hakuna kutekana isipokuwa kama ni kwa masuala ya kifamilia au kutaka ramson.

Au watu huko Ukraine sasa hivi watekwa na kuingizwa kwenye magari ili kupelekwa vitani.

Na hata ikitokea mtu katekwa kwa sababu ingine yoyote ile polisi hutumia masaa 24 hadi 48 kuwatafuta wahusika na shughuli humalizika.

Nimeleta mada moja hapa yahusu mfumo wa Kleptokrasia ambao hulea matukio mabaya kuanzia uchumi mbovu hadi kufikia watu kutekana.

Mambo haya ya utekaji na mauaji ni aibu kwa Taifa na ndo maana nchi ziloendelea zatukumbusha na zimetoa tamko rasmi kutuhimiza kufanya uchunguzi wa matukio haya maana yaweza kuhatarisha hata usalama wa taifa.

Ila polisi hawawezi kujichunguza wenyewe.
 
Kama mnasema wanaofanya haya mambo ni watu wasiojurikana sasa mnajihami nini? tusubiri wakamatwe maana watakuwa vibaka tu, mna hofu ya nini?nazani jeshi letu linamkono mrefu hata wiki haiwezi kufika
 
Umoja wa Ulaya na Marekani wametoa Wito wa kutaka serikali yetu tukufu ianzishe mara moja uchunguzi wa kuwabaini watekaji wa wananchi pamoja na wanasiasa wa upinzani.

Tamko hili linakuja huku serikali yetu tukufu ikiwa imetolea ufafanuzi wa yanayoendelea nchini kuwa watu wengi wanaodaiwa kutekwa huwa wanajiteka na kujipoteza wenyewe.

Hata hivyo, kuna mahali mambo yanabumbuluka na hivyo kutuumbua.

Akiwa na masikitiko makubwa, Mwananchi #1 amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kifo cha Kibao na kutoa taarifa kwake.

N.B: Watanzania halisi tuna hofu ya Mungu.
 
Mkome kutembeza bakuli lenu kwao muone kama watasema kitu hata mkiamua kuchinjana mchana kweupe.
 
Hawa umoja wa ulaya inatakiwa wampige marufuku huyu kizimkazi kusafiri kwenda Nchi wanachama wa umoja wa ulaya vilevile wazuie watalii wao kuitembelea tz maana amani hakuna

Ngoja atekwe mwengine kisha afe uone jamaa watachokifanya. Wanafatilia kwa ukaribu mno.
 
Back
Top Bottom