Umoja wa Ulaya yaiamuru vikosi vya Rwanda na M23 kuondoka DRC Haraka bila masharti yoyote.

Bila vikwazo vya silaha na pesa ....havitaondoka ng'o..
 
Acha aendelee kuwaita kubwa jinga tuu coz anauhuru kusema chochote. Ila asisahai kwamba hao anaowaita kubwa jinga wangeamua kuwasha moto angeanza lalamika kwamba wanyamulenge wanauawa na UN, AU, EAC na SADC wakiwa wanaangalia.
 
SADC&EAC waliishia kuzunguka mbuyu tu!

Hao ndiyo wa kuiwekea vikwazo Rwanda isitumie bandari zao!
 
Ulaya wamebanwa na Trump
Pia ni kawaida mataifa makubwa kuongea lolote ingawa hawana la kufanya zaidi ya kukata misaada
Na hata kama wao ndio wanawafadhili huwezi kujua kwani wana sura zaidi ya mbili

Ndio maana Trump anawakaripia
 
hao EU ndio hasa wanaofanya kongo isitawalike..hili tamko lao ni baada ya kuona hali ya amani inaanza kurejea taratibu baada ya M23 kuanza kuungwa mkono na wananchi hata baadhi ya wanajeshi na polisi wa serikali kujiunga na hao m23..EU washaona kwa mwendo huo ni ishara nzuri kwa nchi kuja kutulia na wakongo kuwa kitu kimoja kitu ambacho EU na washirika wao hawakitaki badala yake wanataka kongo iwe na kashikashi mda wote wanakimbizana roho mkononi hasa ile miji yenye madini adimu..kwa hili tamko lao EU wanataka kuchochea moto upya ambao ulishaanza kupoa..EU washenzi sana hawa ndo wanaofanya kongo isitawalike huo ni mkakati wao maalum wapuuzwe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…