Uchaguzi 2020 Umoja wa wanafunzi TAHLISO wamuunga mkono Magufuli

Nashindwa kufikiria mambo yangekuwaje endapo tamko hilo lingekuwa la kuunga mkono CHADEMA. Leo watu wangetoa mapovu. Wengine wangesema msiingize siasa vyuoni. Akina Sirro nao wangejitokeza wakitoa onyo kali dhidi ya uvunjivu wa amani. Yaani kila mtu angekuwa anatoa povu lake. Lakini kwa kuwa anayeungwa mkono ni Magufuli, hakuna ubaya wowote!
 
Unakielewa hata ulichokiandika? Umeangalia video? Unajua kauli ya umoja wowote ni ya nani? OOooh, CHADEMA ni wehu tu na umethibitisha.
Hawataki kuajiriwa hawa watu? Wenzao wako bench since 2016
 
Ngoja wamalize chuo waje mtaani ndipo watakumbuka hayo maneno vizuri, hakuna boom mtaani, ajira hazipo, biashara hazitoki kabisa
 
Jina la Magufuli kutajwa ukumbi mzima umelipukwa kwa furaha za shangwe na miruzi
 
Mbwa kula kuku sio habari ila jogoo kumkamata na kumla Mbwa, hiyo itakuwa breaking news. Ingekuwa ajabu sana eti hawa watu waandae kikao, waite media na kudeclear kumuunga mkono hadharani Membe au Lissu.
 
Sura nzuri lakini lingese!
 
UVCCM hao.
 
Kadi za kupiga kura Hamna ,hamkujiandikishwa,mnamuugaje Rais mkono?
 
Hawataki kuajiriwa hawa watu? Wenzao wako bench since 2016
Kwa fikra zako unafikiri Lissu atawaajiri wote? Hakuna Rais wa kutatua ajira ila wananchi wenyewe kwa kuanzisha biashara na viwanda kama Mo Dewji. Watanzania lazima waelewe Ulaya watu wamesoma kuanzisha biashara na viwanda kuajiri wengine ndiyo maana wana nafasi zaidi za kazi, hata hivyo ajira bado ni finyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…