bhoke chacha
Member
- Oct 24, 2024
- 6
- 6
Heshima,hadhi na nguvu ya Taifa la Tanzania haikuja kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu ila ilikuwa ni kutokana na umadhubuti,dhamira ya dhati na utashi ambao Waasisi wetu wa Taifa walilijenga.
Falsafa juu ya heshima ya utu wa mwanadamu,uhuru na Kazi pamoja na kiu ya kuwa na Taifa la Watu wamoja,watu wasiojitambulisha kwa utofauti wa makabila yao,Dini zao ,Kanda wanazotokea,Tabaka walizokulia na kuziishi bali Utaifa wao.
Kwa kulijenga Taifa moja la namna hiyo ndiyo ilikuwa alama ya Taifa letu,Taifa lenye Mshikamano wa hali ya juu,Taifa ambalo Matabaka halikuwa ni jambo la Ufahali wa kujivunia. Viongozi wa umma hawakutambulika kwa vyeo vyao bali walitambulika kwa majukumu waliyobebeshwa katika Taifa changa.
Ni rahisi kupuuza na hata kuzifuta kazi kubwa za Waasisi katika Kulijenga Taifa hili,lakini siyo rahisi kuwaunganisha watu waliokuwa wamekuzwa kwenye mifumo mikongwe ya kiukoloni yenye kuutukuza ukabila.Mwalimu Nyerere alilikuta Taifa lenye kabila zaidi ya 145 za Watu wenye tawala zao na Lugha zao.Kuwaunganisha Watu wenye tofauti hozo kubwa za kimfumo na ukawashawishi waweze kuitambua lugha moja ambayo ni Kiswahili kuwa lugha ya wote,haikuwa kazi rahisi hata kidogo.
Ni rahisi sana kujenga barabara unazotaka,ukajenga majengo na hata ukatengeneza viwanda vikubwa unavyotaka.Iwapo hicho ndicho utakiita kuwa ndicho kipimo bora cha Maendeleo na uongozi katika nchi,mimi nitakukatalia.
Kazi ngumu na yenye ufahali kuliko zote ni kazi ya Kuliunda Taifa ,Kuliunda Taifa la Watu wamoja na Taifa lenye Lugha moja.
Tulipigana Vita ya Kagera VS Uganda na tukashinda kutokana na msisimko wa uzalendo ambao Waasisi wetu walipanda kwa Watanzania. Msisimuko ule wenye ari na nguvu ya kuliona Taifa halionewi,Kuliona Taifa linashinda na Kuliona Taifa linaogopwa na Waovu ,ulikuwa ndiyo msingi wa ushindi wetu kabla hata Jeshi halijaingia Vitani.
Kuwa na Taifa la aina hiyo,Taifa lenye kutamani kuwa juu,Taifa lenye Watu wenye upendo,Umoja na Mshikamano siyo Ushamba bali ni ufahali.
Kwa sasa Viko Viashiria vya kila aina vinavyoonesha kwamba sisi Watanzania siyo wamoja tena,Siyo Watu tunaoamini tena kwenye misingi ya Usawa wa binadamu,Siyo Watu tena wenye ari na nguvu ya kuuheshimu ukuu wa Taifa letu tena. Viashiria hivi vitupe maswali juu ya iwapo itatokea vita na Mataifa jirani tutashinda sote???Au tutaliona hilo kuwa ni jukumu la Viongozi wetu na Jeshi.
Nitoe Wito kwa viongozi wetu kutuongoza kwenye tafakuri ya kurejesha misingi iliyoasisi Taifa letu,Utaifa ni Ufahali wetu sote.

- Ahsante.