Umri gani ni sahihi kumtahiri mtoto wa kiume?

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,407
Reaction score
3,260

Jamani wadau nisaidieni mwenye kujua haya mambo, ni umri upi unaoshauriwa kitaalamu kumtahiri mtoto wa kiume, na je kuna njia ngapi za kufanya hiyo kitu.

Maana kuna maneno yanasema eti ukimfanyia akiwa bado mdogo kuanzia miaka 0 hadi mmoja eti atakuja kuwa dhaifu katika ile shughuli ya kikubwa, wengine wanasema ukimfanyia kakua ndio hiyo kitu itamtokea akiwa mkubwa

Pia njia ipi ni salama zaidi mimi najua ya kukata na kushonwa naambiwa ipo nyingine yakufunga na plastiki, je ipi ni nzuri?

Nategaemea msaada wenu waungwana, maana kunasehemu nilisoma eti matatizo mengi ya wanaume kushindwa kuwatimizia wepenzi wao tohara isiyo sahihi ni moja ya sababu
 
Sidhani kama kuna umri sahihi wa kutahiri, nadhani inategemea na wewe mwenyewe, kwangu mie nilitahiri akiwa na mwaka 1, na alishonwa, rafiki yangu alimtahiri mtoto akiwa na miezi 3, mwingine 7...cdhani kama kuna umri sahihi...na hizo nyingine nadhani ni imani tu.
 
Kuwahi kutahiri na hizo imani ni vitu wiwili tofauti...

Biblia inasema mtoto atahiriwe ndani ya siku 14... lakini ni vizuri akitahiriwa at least akiwa na miezi mitatu.... Hii itasaidia sana kwa sababu watoto wa kiume mara nyingi huugua sana UTI especially akianza kutambaa, na pia kwa umri huo anapona haraka sana, 7 days anakuwa amepona.
 
Lakini bado hamjajibu swali la akikuwa ataweza shughuli za kikubwa?
 
Inategemea hata miaka miwili,
Njia ya kushona ni nzuri zaidi
 
Niliwahi kuongea na Dr mmoja juu ya issue hii, actually nilikwenda kumuomba ushauri kabla ya kumfanyia mwanangu tohara, na jibu lake lilikuwa hakuna specific number of days!

Lakini kwa ushauri tu akaniambia ni vizuri zaidi kumtahiri mtoto akiwa tayari angalau ametimiza siku 7 au 8! Lakini kuwahi kabla ya hapo hakuna madhara, ila nadhani kuchelewa zaidi ndio kuna madhara hasa possibility ya maambukizi ya magonjwa!

Kama nakumbuka vizuri manabii wengi walisisitiza mtoto kutahiriwa siku ya nane tangu azaliwe!
 
Mkuu hapo umenigusa sana, wangu mimi ana umri wa miezi 5 na anasumuliwa sana na UTI Na ndio maana wazo la kumtahiri likaja tatizo ikawa hizo myth za mtaani.

na vipi kuhusu njia ya kushona au plastiki?
 
Njia ya kushona ni njia ambayo imedumu kwa muda mrefu, hii ya plastic ni njia mpya ambayo imejaribu kumuepusha muhusika na maambukizi ya magonjwa yanayotokana na kushirikiana vyombo vya tohara.

Hivyo basi, nashauri utumie plastic kwani ni salama zaidi. Ila usafi ni wa kuzingatia ili kuepusha maambukizi.
 
ila nadhani kuchelewa zaidi ndio kuna madhara hasa possibility ya maambukizi ya magonjwa!
suala ni kuwa mwangalifu tu na usafi wa hali ya juu otherwise maambukizi yatakuwa palepale
 
Mkuu hapo umenigusa sana, wangu mimi ana umri wa miezi 5 na anasumuliwa sana na UTI Na ndio maana wazo la kumtahiri likaja tatizo ikawa hizo myth za mtaani.

na vipi kuhusu njia ya kushona au plastiki?

Doctors hawashauri sana njia ya plastic, ile wanatumia tu kwa sababu wanadhani ni less painful na huuguzi kidonda... lakini madhara yake ni kwamba wakikosea kufunga, kwa mfano wakifunga kwa nguvu sana, basi inatokea Gangrine (sehemu ya juu ya uume unakosa circulation ya damu), panageuka peusi/blue na akicheleweshwa madhara yake ni mabaya zaidi... ila akiwekewa mpira inatakiwa close observation.
 
umri mzuri zaidi ni pale anapokuwa bado mdogo, kwasababu akishakua mtu mzima huwa wanapata tabu sana kupona kidonda.

Angalau kabla hajafikisha miaka saba awe tayari kafanyiwa tohara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…