Wenzetu wana msemo wanasema" age is just a number " Nashangaa kwa nini mtu ufe na kihoro unadanganya umri ? ni namba tu hiyo , Binafsi huwa nasikia raha sana pale ninapotaja umri wangu halafu mtu ananiambia unaonekana mdogo zaidi , Inamaana Najitunza , na hicho ndicho kitu muhimu , Heshimu Mwili wako Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe....sasa ukiwaangalia hawa Vijana Inawezekana wengine kweli ni wadogo ila wengi wao wanaonekana wakubwa kwa miaka kumi zaidi ...yaani wanafuja sana Miili yao na Ulevi, Ngono zembe , Mihadarati ...Jiheshimuni na Muheshimu Miili yenu Bandugu !