MIAKA YANGU 27 INANITETEMESHAAAAAA
Kijijini kwenu wazazi hawana ardhi, mashamba, mifugo, mitumbwi, nyavu n.k
Jamii zingine kama za watanzania wenye asili ya Kiarabu, Kihindi, Kisomali vijana hutegemewa kuendeleza pale walipoishia wazazi.
Hili suala la kukimbilia mjini wakati wazazi hawana chochote walichowekeza mjini lakini kijijinj wana mali nilizotaja hapo paragraph ya pili ni kujiita masikini wakati siyo kweli baba wa babu alimrithisha babu, naye babu yako akamrithisha baba yako mali hizo kijijini.
Lakini wewe umezipuuza kukimbilia mjini kutaka kuigiza familia ambazo tayari walifika mjini kitambo unataka kujifananisha nazo, hilo ni kosa kubwa.
Rudi kijijini ukaendeleza pale wazazi walipoishia, ya mjini waachie ambao wazazi wao waliwekeza kitambo na usisononeke kuona wenzio wana majumba, ardhi, daldala, kampuni n.k mjini ukataka kushindana nao. Wa mjini wameachiwa na wazazi na kuendeleza.
Kifupi wewe siyo masikini, lakini hufahamu hilo. Rudi haraka kijijini.