Umri unaenda, nachanganyikiwa

Umri unaenda, nachanganyikiwa

Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake: Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa; wakati wa kuua na wakati wa kuponya; wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga; wakati wa kulia na wakati wa kucheka; wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza; wakati wa kutupa mawe na wakati wa kuyakusanya mawe pamoja; wakati wa kukumbatia na wakati wa kuacha kukumbatia; wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza; wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa; wakati wa kurarua na wakati wa kushona; wakati wa kukaa kimya na wakati wa kuongea; wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia; wakati wa vita na wakati wa amani. Mfanyakazi hufaidi nini kutokana na juhudi zake hizo? Mimi nimeiona kazi ambayo binadamu amepewa na Mungu. Mungu amekifanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Amempa binadamu hamu ya kujua mambo ya baadaye, lakini hajamjalia fursa ya kuelewa matendo yake Mungu tangu mwanzo mpaka mwisho. Najua kwamba, kwa binadamu, liko jambo moja tu la kumfaa; kufurahi na kujifurahisha muda wote aishipo. Sote inatupasa kula na kunywa na kufurahia matunda ya kazi zetu.

Mhubiri 3:1-15
 
Sister kwenye maisha kuna kitu kinaitwa a point of no return na ndio hiyo uliyopo.

Haijalishi umefanya makosa yapi

Haijalishi hujapata au umekosa kipi kwenye maisha

Maana hata ukiyawaza hayatobadilika ila, ulichobakiza ni uhai na neema ya kuishi.
Jikubali na uikubali safari yako maana hakuna mtu wa kumkabidhi

Ni wewe tu ndio lazma uiishi. Najua ni ngumu ngumu ngumu sanaaa kuepuka kujilinganisha na wengine au la kuangalia ni vitu gani haukuvitimiza. Na mbaya zaidi watu wakikusema vibaya kama walivyoanza humu Ila kumbuka kujinenea mazuri

Kumbuka kujitakia mema, kumbuka kujipenda na kujithamini kwa sababu dhidi unavyoongeza umri ndivyo hizo kelele zitakapoongezeka.

Na usipokuwa makini, utajitumbukiza shimoni ili kufurahisha watu ilhali unajiteketeza zaidi haswa kwa kupata mahusiano na ridhki zisizo sahihi..

Kwa hiyo kuliepuka hili, jifunze kujipenda, kujithamini na kujifariji lakini pia mkumbuke Mungu wako. Funga, sali na utoe sadaka ikibidi, omba kwa kile kitu unachokitumainia..

Mungu atakusaidia. Stay strong
 
Hee! Mi dada ako nna 31
Sifa zangu ni - jobless - sijazaa -sijasoma - similiki mume - sina mchezo/kikoba/kiwanja/nyumba - sina mahusiano serious na sitegemei
Tena umri unavyozidi kwenda ndo nazidi kupandisha vigezo vingi vya mume nnaemtaka!
Ila siko desperate hata!!! Nahofia kufa sijalifanya kusudi la maisha yangu! Kama unavyojua kila mwanadamu ana kusudi lake duniani moja ama mengi ila mimi nikifa sijawa MSHAURI NASAHA/MZEE WA BARAZA ntajuta kuliko kuwa nayo yote hayo ya duniani
 
Zingatia hii hapa
1. Kila siku unayoiona unakuwa mchanga kwa umri wako uliobaki,
2. Utajiri haujalishi umeajiriwa au umejiajiri, inajalisha akili yako na ulivyojiposition
3. Acha kufanya jambo kwa comparison fanya jambo kwa deprivation , yaan naposema comparison Usifanye jambo au ukataka jambo kwa kujilinganisha na mtu au kuangalia umri wako, bali angalia Jana Hukuwa na nini na leo unacho nini hata kama hakijakamilika kiko katika hatua ipi, hata Kama ni kuomba kazi, idadi ya CV ulizosambaza Jana ziwe ndogo kulinganisha na ulizo sambaza leo

4. Usidharau fursa hata Kama ni ndogo, kuna watu wengi wanajitolea maofisin, mkikutana nao na matai mnawakadiria mshahara kwa shati walilovaa na kupigwa Pasi kumbe nao madhaifu yao hawayaweki wazi,

5. Usifuatilie mitandao sana ya instagram, maana utaishia kuona waliopiga picha na Mali za wengine ukadhan ni ZAO , Kumbuka hakuna anayeonesha madhaifu yake hadharani, BALI uonesha mazuri tu hata Kama ya kufeki,

6. Ukiishi kivyako BILA watu wasio wa Muhimu kujua shida zako au mishe zako utaenjoy sana hata kaka huna Mia

7. UMRI SI KIGEZO , MI NIMEAJIRIWA NIKIWA NA 25 Yrs Ila Pesa ya miaka 4 ya kwanza haikufanya la maana Ila nilipotimiza 30 na kuendelea ndo ikawa Kama nimeanza Kazi,

Ukipata muda pitia vitabu kuona matajiri wanavyosota na utajiri Wengine wameupata wakiwa 40+

Britanicca
 
Mwezi ujao natimiza umri wa miaka 27

1 - Sina kazi

2 - Sina chochote ninachomiliki (kiwanja/nyumba n.K)

3 - Sina mahusiano ambayo yanaeleweka

4 - Sina mtoto (sitamani kuwa single mama)

Hii miaka 26 niliyoishi duniani namshukuru mungu kwasababu sikuile tulizaliwa wengi na leo hawapo.

Ninamshukuru mungu kwasababu nina afya njema kwasababu kuna ambao wapo hukooo wapigania uhai waooo hata waweze kuamka kitandani

Ahsante yesu kwa zawadi hii ya uhai hata nipo huku jf naandika hayaaaaa

Miaka yangu 27 inanitetemeshaaaaaa
Nyinyi ndiyo wale wapumbavu mnao poteza muda mwingi kutajirisha wahuni makanisani wanao jihita mitume na manabii mnadhani Mungu wa hizo dini zenu ni mpuuzi alipo sema siku 6 fanya kazi ya 7 ndiyo ya bwana mungu
 
Zingatia hii hapa
1. Kila siku unayoiona unakuwa mchanga kwa umri wako uliobaki,
2. Utajiri haujalishi umeajiriwa au umejiajiri, inajalisha akili yako na ulivyojiposition
3. Acha kufanya jambo kwa comparison fanya jambo kwa deprivation , yaan naposema comparison Usifanye jambo au ukataka jambo kwa kujilinganisha na mtu au kuangalia umri wako, bali angalia Jana Hukuwa na nini na leo unacho nini hata kama hakijakamilika kiko katika hatua ipi, hata Kama ni kuomba kazi, idadi ya CV ulizosambaza Jana ziwe ndogo kulinganisha na ulizo sambaza leo

4. Usidharau fursa hata Kama ni ndogo, kuna watu wengi wanajitolea maofisin, mkikutana nao na matai mnawakadiria mshahara kwa shati walilovaa na kupigwa Pasi kumbe nao madhaifu yao hawayaweki wazi,

5. Usifuatilie mitandao sana ya instagram, maana utaishia kuona waliopiga picha na Mali za wengine ukadhan ni ZAO , Kumbuka hakuna anayeonesha madhaifu yake hadharani, BALI uonesha mazuri tu hata Kama ya kufeki,

6. Ukiishi kivyako BILA watu wasio wa Muhimu kujua shida zako au mishe zako utaenjoy sana hata kaka huna Mia

7. UMRI SI KIGEZO , MI NIMEAJIRIWA NIKIWA NA 25 Yrs Ila Pesa ya miaka 4 ya kwanza haikufanya la maana Ila nilipotimiza 30 na kuendelea ndo ikawa Kama nimeanza Kazi,

Ukipata muda pitia vitabu kuona matajiri wanavyosota na utajiri Wengine wameupata wakiwa 40+

Britanicca
Shukran
 
Hee! Mi dada ako nna 31
Sifa zangu ni - jobless - sijazaa -sijasoma - similiki mume - sina mchezo/kikoba/kiwanja/nyumba - sina mahusiano serious na sitegemei
Tena umri unavyozidi kwenda ndo nazidi kupandisha vigezo vingi vya mume nnaemtaka!
Ila siko desperate hata!!! Nahofia kufa sijalifanya kusudi la maisha yangu! Kama unavyojua kila mwanadamu ana kusudi lake duniani moja ama mengi ila mimi nikifa sijawa MSHAURI NASAHA/MZEE WA BARAZA ntajuta kuliko kuwa nayo yote hayo ya duniani
Et sina mchezo Wala kikoba 😄😄
 
Back
Top Bottom