Umri unaenda, nachanganyikiwa

Umri unaenda, nachanganyikiwa

USIOGOPE.
Neno "USIOGOPE" limetajwa mara 365 ndani ya Biblia. Mathalani katika nukuu kutoka waraka wa Tito 2:13 inaeleza Yesu Mungu Mkuu anakwambia usiogope, maana yupo pamoja nawe.

Mwaka mmoja una siku zipatazo 365 idadi sawa na ile ya neno hilo ndani ya maandiko haya matakatifu. Kwa hiyo kama ndivyo hivyo, basi siku zote JIPE MOYO kwani yote utayashinda. Kumbuka usijinenee neno lolote baya kwani Ibilisi atalichukua na kuli "brand" katika maisha yako, na wewe utakuwa hivyo.
Usiogope 👏
 
Mwezi ujao natimiza umri wa miaka 27

1 - Sina kazi

2 - Sina chochote ninachomiliki (kiwanja/nyumba n.K)

3 - Sina mahusiano ambayo yanaeleweka

4 - Sina mtoto (sitamani kuwa single mama)

Hii miaka 26 niliyoishi duniani namshukuru mungu kwasababu sikuile tulizaliwa wengi na leo hawapo.

Ninamshukuru mungu kwasababu nina afya njema kwasababu kuna ambao wapo hukooo wapigania uhai waooo hata waweze kuamka kitandani

Ahsante yesu kwa zawadi hii ya uhai hata nipo huku jf naandika hayaaaaa

Miaka yangu 27 inanitetemeshaaaaaa
Wee bado mteke sana, lkn bado unalo tumaini.
 
Niko hapa na 29yrs Sina mtoto, sina mume na siko kwenye committed relationship, Sina kipato Cha kueleweka ingawa nilikuwa nimeanza kusimama yakatokea yakutokea nipo naanza moja bado sitetemeki Ila tu napambana ili nipate kuinuka Tena, kikubwa usijikatie tamaa, jifunze kwa waliofanikiwa Ila kamwe usijilinganishe na wengine Cha muhimu wewe zishinde mechi zako
Njoo pm
 
Umejuaje kuwa huna chochote?...
Ni nini kinachokuambia kuwa hivyo unavyovitaja ni vyovyote?..
Mkuu jifunze kutokea ndani yako na siyo nje yako....hayo yote unayoyataja ni elimu uliyomezeshwa nje yako ila ndani yako kuna kila kitu.
................................................................................................................................................................
Nina uhakika wa zaidi ya asilimia 100% kuwa pamoja na hayoyote uliyoyataja kuna wakati unakisikia ndani yako vizuri na hapo ndipo ulipo " ni wewe" patumie vizuri.
 
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
 
Back
Top Bottom