Umri upi ni sahihi kumuita mtu mzee?

Umri upi ni sahihi kumuita mtu mzee?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Mtanzania kijana ni mwenye miaka 18-35, je ukiwa na miaka 36 kwenda juu unakuwa umepata hadhi na status za kuitwa mzee, na kama sio mzee je mwenye miaka 36 kwenda juu ni nani.

Nataka kukata safari za kwenda bar, nijikite nyumba za ibada, niondoke kati kati ya mji nikajichimbie nje kidogo ya mji, niendelee kujipanga na kikokotoo, niache kabisa kuvichakata vibinti vya chuo nijikite kwa single mother na wajane maana hapa umri utakuwa umenitupa mkono nk, miaka yangu ni 38.
 
Hizo mambo ni huwa zinakata automatically mkuu. Hakuna formula wala specific age. Kila mtu uzee inamuingia kwa wakati wake sio kwa miaka.

Vile wewe umeanza kufikiria kukata hayo mambo katika miaka 38 tu ni ishara tosha 'uzee' utakuingia mapema

Kuna vidingi hadi vina 68 bado vinang'ang'ana kwenye clubs na vinapambana kupata toto za chuo. Ni saikolojia ya mtu binafsi tu
 
Mtanzania kijana ni mwenye miaka 18-35,je ukiwa na miaka 36 kwenda juu unakuwa umepata hadhi na status za kuitwa mzee, na kama sio mzee je mwenye miaka 36 kwenda juu ni nani. Nataka kukata safari za kwenda bar, nijikite nyumba za ibada, niondoke kati kati ya mji nikajichimbie nje kidogo ya mji, niendelee kujipanga na kikokotoo , niache kabisa kuvichakata vibinti vya chuo nijikite kwa single mother na wajane maana hapa umri utakuwa umenitupa mkono nk miaka yangu ni 38
Wewe tayari ni babu. Unasubiri kufa tu. Zidisha sala na kwenda nyumba za ibada. Umesshapita umri wa kuwa mzee.
 
Inategemea unazungumza katika madhingira gani ,lakini wengi kibongobongo wanavyoita mtu Mzee wanamainisha( SIR) tukigeuza kwa lugha ya kimombo yaani sio kwamba ni Mzee ya umri bali sifa na heshima uliyo nayo katika jamii .
 
Mtanzania kijana ni mwenye miaka 18-35, je ukiwa na miaka 36 kwenda juu unakuwa umepata hadhi na status za kuitwa mzee, na kama sio mzee je mwenye miaka 36 kwenda juu ni nani.

Nataka kukata safari za kwenda bar, nijikite nyumba za ibada, niondoke kati kati ya mji nikajichimbie nje kidogo ya mji, niendelee kujipanga na kikokotoo, niache kabisa kuvichakata vibinti vya chuo nijikite kwa single mother na wajane maana hapa umri utakuwa umenitupa mkono nk, miaka yangu ni 38.
Kuanzia miaka 25 kuendelea ukishakuwa na hela basi wewe ni mzee tu
 
Back
Top Bottom