Umri upi ni sahihi kumuita mtu mzee?

Umri upi ni sahihi kumuita mtu mzee?

siyo 44 mzee akina mkuchika bado wako uvccm bado
Hapo sawa kabisa. kwa hiyo vijana wasiwe na hofu. Uzee ni kujitakia tu, ukiwa na hela ahata ukiwa na miaka 22 tayari wewe ni mzee kabisa. Kwa kule Moshi unasalimiwa kwa heshima kabisa ukishakuwa na hela na kikao cha wazee hakiwezi kuendelea usipotia timu kikaoni. Ila ukiwa huna hela hata uwe na miaka 60 wewe unaonekana chokoraa tu.
 
Ukiwa na miaka 60 huna hela tunakuita kijana. Ukiwa na miaka 25 una pesa tunakuita mzee
Pesa ndio huamua nani aitwe mzee
 
Nina miaka 2 sijajiangalia kwenye kioo,uzi wako ukanikumbusha hilo nikachukua kioo,nilivyojitazama tu kwanza nikastuka,sina nuru tena,usoni nina makunyanzi na nyweleni kuna kama madoa meupe niliposogeza kioo karibu zaidi nikabaini ni mvi nilipogusa kichwani sehemuya juu ya kichwa kuelekea kisogoni kuna sehemu nikaona kama hakuna nywele nikabaini ni kakipara.Nimehuzunika sana nilipoangalia picha zangu za utotoni na ujanani.Baada ya hapo nikajiandaa nitoke njiani kuna jamaa naye ameanza kuzeeka akaniambia shikamoo mzee ikanibidi nihairishe nilipokuwa nakwenda nikarudi home nikajifungia ndani nikalia sana mpaka jirani akasikia akaja kugonga na kuuliza mzee unalia nini nikaanza kumtukana mpaka watu wakajazana wakaanza kusema mzee msamehe nikaanza kulia upya nilijua wangesema uncle msamehe
 
Mtanzania kijana ni mwenye miaka 18-35, je ukiwa na miaka 36 kwenda juu unakuwa umepata hadhi na status za kuitwa mzee, na kama sio mzee je mwenye miaka 36 kwenda juu ni nani.

Nataka kukata safari za kwenda bar, nijikite nyumba za ibada, niondoke kati kati ya mji nikajichimbie nje kidogo ya mji, niendelee kujipanga na kikokotoo, niache kabisa kuvichakata vibinti vya chuo nijikite kwa single mother na wajane maana hapa umri utakuwa umenitupa mkono nk, miaka yangu ni 38.
Pale mvi unapokuparamia kila eneo lenye nywele. Mvi huo hausikii saluni Wala supablaki,hapo ujue rasmi umeutimba uzee.
 
Nina miaka 2 sijajiangalia kwenye kioo,uzi wako ukanikumbusha hilo nikachukua kioo,nilivyojitazama tu kwanza nikastuka,sina nuru tena,usoni nina makunyanzi na nyweleni kuna kama madoa meupe niliposogeza kioo karibu zaidi nikabaini ni mvi nilipogusa kichwani sehemuya juu ya kichwa kuelekea kisogoni kuna sehemu nikaona kama hakuna nywele nikabaini ni kakipara.Nimehuzunika sana nilipoangalia picha zangu za utotoni na ujanani.Baada ya hapo nikajiandaa nitoke njiani kuna jamaa naye ameanza kuzeeka akaniambia shikamoo mzee ikanibidi nihairishe nilipokuwa nakwenda nikarudi home nikajifungia ndani nikalia sana mpaka jirani akasikia akaja kugonga na kuuliza mzee unalia nini nikaanza kumtukana mpaka watu wakajazana wakaanza kusema mzee msamehe nikaanza kulia upya nilijua wangesema uncle msamehe
😂😂
 
Mtu kuitwa mzee ni miaka 70 chini ya hapo ni ubatili tu kumuita mtu mzee
 
Mtanzania kijana ni mwenye miaka 18-35, je ukiwa na miaka 36 kwenda juu unakuwa umepata hadhi na status za kuitwa mzee, na kama sio mzee je mwenye miaka 36 kwenda juu ni nani.

Nataka kukata safari za kwenda bar, nijikite nyumba za ibada, niondoke kati kati ya mji nikajichimbie nje kidogo ya mji, niendelee kujipanga na kikokotoo, niache kabisa kuvichakata vibinti vya chuo nijikite kwa single mother na wajane maana hapa umri utakuwa umenitupa mkono nk, miaka yangu ni 38.
Ukishafikisha miaka 30 wewe ni mzee wa makamo.
 
Inategemea na unavyojitunza...
Unaweza kuwa na 28 lakin umekomaa kama una 40..utaitwa mzee
Sasa ili uepuke hayo
-kula vizuri
-vaa vizuri
-fanya mazoez
-tumia lotion nzur
 
Mtu yeyote mwenye kadi ya CCM ni mzee hata kama ana miaka 4.
 
Kwa mwanamke uzee unaanzia miaka 40, hata nature inasema mwanamke mwisho mzuri wa kuzaa Ni miaka 35. kwa mwanamme inategemea una hela kiasi gani. Wengi wetu tukistaafu tunarudi ujana upya na tutaendelea kua vijana Hadi pesa ya mkupuo ya kikokotoo imalizike.
Rupert Murdoch ambaye age mate wake wote wako over 90 lkn yeye ndio kwanza kafunga ndoa ya sita. Anakadiriwa kua na miaka 50. Age mate wake ambao hawana pesa wako 94 huko.
 
Duh mapeema mno! Uzee nadhani ni miaka 60+. 55 ni mzee kijana, 18-54 ni kijana.
Inaonyesha hutunzi afya yako kupelekea unachoka mapema.
 
Back
Top Bottom