Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

Nisome upya madame, nimesema 18yrs kwa watanzania kusema wamekomaa ni uongo mtupu kwanza hata kujielewa 99% hawajielewi hata kujieleza hawajui yaani awe kasoma ama hapana

kwa ulaya ni tofauti kule kweli 18yrs anajielewa nawe ndo umenambia iyo kesi 16yrs huko ulaya sawa niko bongo hapa

bongo akili zinaanzaga kuja ana 30yrs ndo ana akili za 18yrs wa ulaya na sehemu nyingine.
Hapo tatizo so umri ila ni malez + curriculum tutumiayo mkuu.
 
Wenzetu wahindi na. Asia wanaanza la kwanza na miaka 5 Sisi ndo tuanze na miaka 10?

Atafika chuo kikuu na miaka mingapi? 25?

Miaka 25 kuna baadhi ya kazi huwezi pewa ufanye unakuwa ushazeeka..
Itabidi kustaafu nako waongeze muda, kustaafu kwa hiari iwe miaka 58 na kwa lazima iwe miaka 63

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada chapombe aliandika akiwa kalewa
Na atakuwa hataki kupeleka watoto shule 😂 😂 , kashtuka anaambiwa mtoto aende la 1, kapigiwa na hesabu ya school bus. Aisee great thinker!

Everyday is Saturday................................😎
 
Africa haipo sababu ya mtu kufika chuo kikuu! Kuna namna tunayotakiwa kufikiri kwa upya na kuchukua hatu kulingana na bara letu ni namna gani ya kujikomboa kiuchumi

Hii kufikiri vya nje ndo vinatuponza na unamkuta mtu anakuja humu anaanza kufananisha elimu,mazingira ya ulaya na kwetu na unamuona mtu wa namna hiyo anaandika humu kiswaenglish unagundua tu kwamba hawa ndiyo wanao tuludisha nyuma kimaendeleo

Mtanzania unamkuta anafikiri kizungu zungu na kuongea kizungu na kufuata mifumo ya mafanikio kizungu ilihali alipozaliwa na anapoishi uchumi wake hautegemei msamiati wa teknolojia bali ni kilimo

Na tunacho walithisha watoto kwa mfumo wa elimu hizi za kulipia pesa nyingi tegemeeni vitukuu na nyanya zetu kuja kuishi maisha mabaya sana ya kuigiza na hawataweza chochote na mwisho wa siku watalazimisha mzungu aje kuwaongoza na hapo ndipo ukoloni utarudi Africa na mambo kua pale pale mabaya zaidi
Ni kweli ndugu.
Hapa ndo tunahitaji mawazo bora ili tuone tuelekee wapi?
 
Mimi ni mmojawapo wa walioanza la kwanza na miaka 10.

Sio kwamba sikuwa na akili, bali tatizo ni ufupi na mkono ulikuwa mfupi nikiambiwa shika sikio la upande wa pili siwezi.

Toka nina miaka 7 naenda kuanza la kwanza lakini narudishwa.

Wote walionifanyia unyama huu nimewasamehe,nyambafu zenu.

Unforgetable
Tumsamehe na mtoa mada
 
Nyerere alianza la kwanza akiwa na miaka 12 alimaliza la nne la mkoloni akiwa na 16
 
Mimi nilikosa schoolarship ya kwenda kusoma Austria sababu ya umri wangu kuwa mkbwa

Wao walikuwa wanahitaji undergraduate awe na 25 yrs below mimi nlikuwa na 27 na ndio nimemaliza form six

Ni vichwa vya watoto wetu ndio vigumu kutokana na misosi na african genetics thats all
 
Wana jf

Makuzi ya binadamu wa mtanzania yanapitia magumu mengi, hivyo pia akili uchelewa kukomaa kupota uelewa wa kujifunza kitu Kwa umakini. Natoa sababu Kwa nini umri miaka 10 ndio unafaa mtoto kuanza la Saba.
1. Umri ukiwa miaka Kumi mtoto anakuwa amekomaa uondoa uwoga Na anaweza kuhoji kama kitu sio sahihi.
2. Waliokosa lishe Bora huwa ndio wakati ambao makuzi ya akili yanakuwa Sawa.
3. Mtoto adanganyiki kirahisi Na akifanyiwa vitu vya unyanyasaji wa kijinsia ana uweza wa kumweleza mama yake au baba yake.
4. Ni umri ambao vipaji uchipuka mtoto kujua anapenda nini Na ana kipaji gani.
5. Kutokukubali kuonewa Na mtu yeyote Kwa kuwa sio mwoga.
6. Urahisi wa kuweza masomo walimu hawapati shida.
7 . Kama shule IPO mbali huyu ndiye mwenye uwezi wa kutembea umbali mrefu.
8. Akimaliza darasa la Saba anaweza kusaidia shughuli za kilimo au kuanza kujitegemea
9. Hauhitaji kumulea kama mtoto ikiwa hakufaulu kuendelea Na masomo.
10. Kutokana Na umri anakuwa amepunguza michezo mingi hatarishi Kwa kuwa tayari ana uelewa

Kumbukumbu zinaonyesha wengi waliofanikiwa wengi walianza shule wakiwa Na miaka 12.
Mkuu mbona upo mbali sana huo umri, ingetakiwa kabisa awe ndiyo anamaliza la saba hebu angalia Tanzania one form 4 mwaka jana ana umri wa miaka 15 hiyo ndiyo range sahihi.
 
Huna hoja wewe
Hii ndiyo kasoro ya baadhi ya wana-JF wanaojifanya wajuaji. Mtu kakariri hata utafiti uliofanyika ili kuipa uzito hoja yake na wewe unaishia kusema 'huna hoja'. Aliyotoa ni nini sasa kama si hoja? Sema hukubaliani na hoja yake na wewe toa hoja yako inayotofautiana na yake na sisi tuwe huru kuamua ipi ni sahihi.
 
Dah! Nadhani hujaiangalia Tanzania/Afrika kwa mapana yake.
Asilimia kubwa ya wananchi waishio vijijini bado wana dhana potofu ya kuwaozesha watoto wa kike wangali wadogo. Swala la kupeleka watoto shule limepunguza sana ndoa za mapema na kuwalinda mabinti kuozeshwa.

Hebu vuta picha binti wa kitanga au Manyoni kule Singida amemaliza standard 7 Akiwa na miaka 17 (hapo viungo vyote vya uzazi vimekamilika) unadhani ni wangapi watapata nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari?

Ila kupanga ni kuchagua.
Pia hakuna awali iliyo mbaya
 
Mimi ni mmojawapo wa walioanza la kwanza na miaka 10.

Sio kwamba sikuwa na akili, bali tatizo ni ufupi na mkono ulikuwa mfupi nikiambiwa shika sikio la upande wa pili siwezi.

Toka nina miaka 7 naenda kuanza la kwanza lakini narudishwa.

Wote walionifanyia unyama huu nimewasamehe, nyambafu zenu.

Unforgetable
C&P
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...

Kama nyumbani hapako sawa hata makuzi ya mtoto pia hayatakua sawa...
 
Dah! Nadhani hujaiangalia Tanzania/africa kwa mapana yake.
Asilimia kubwa ya wananchi waishio vijijini bado wanadhana potofu ya kuwaodhesha watoto wakike wangali wadogo. Swala la kupeleka watoto shule limepunguza sana ndoa za mapema na kuwalinda mabinti kuozeshwa.

Hebu vuta picha binti wa kitanga au manyoni kule singida amemaliza standard 7 Akiwa na miaka 17 (hapo viungo vyote vya uzazi vimekamilika) unadhani ni wangapi watapata nafasi ya kujiunda na elimu ya secondari?

Ila kupanga ni kuchagua.
Pia hakuna awali iliyo mbaya
Utafiti nimeufanya kupitia prof Muhongo Na dr Bashru
 
ila tuwe wakweli mie wanaposema eti miaka 18 ni mtu mzima kwa watanzania nakataa kuna watu miaka iyo hajielewi (wengi wa watanzania ) hata kuhoji kitu hawezi yaani anapelekwa kama ndezi tu.

mi napendekeza shule tuanze na miaka 16 maana watanzania akili zetu ni ndogo sana wakati mwingine nahisigi hatuna akili kabisa (tunadaiwa akili)
Mazingira au malezi yamebadilika, zamani mtoto akimaliza la 7 kama wa kiume anafukuzwa nyumbani aende kujitegemea na anayamudu maisha vizuri sana na wengine mwaka huo huo anaoa na kumtunza mke, watoto na kuwasaidia wazazi wake.
Haya matoto ya siku hizi form five anapelekwa shule na mzazi yaani mtoto wa form 6 siku hizi anaongea pumba tupu
 
Back
Top Bottom