Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

Labda uongezwe na muda wa kustaafu

Nenda English medium kuna watoto eleven years anamaliza la saba

We Chelewa na mwanao utamchelewesha kila kitu hata scholarship na ukijeba wake hapati
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mkuu umemliza la 7 na miaka 17........ila form one itakuwa hukupiga simu chooni maana hata form 2 wlikuwa wanakuamkia
Form 4 nimemaliza na 21, form 6 na 23-->24, versity na 28-->29.

Ila Mungu hamtupi mja wake, nimemaliza chuo tuu na kupata kazi sikukaa hata mwezi mtaani.

FB_IMG_1614545061794.jpg
 
Naunga mkono hoja, elimu ya mtaani ina umuhimu mkubwa sana ukizingatia asilimia kubwa ya maisha yetu yatakuwa mtaani kuliko shuleni!.

Kimsingi watoto wakienda shule mapema tunawatengenezea mazingira ya kutegemea elimu ya darasani tu na kutegemea kuajiriwa tu. Fikiria mtoto wa siku hizi akimaliza form asipoendelea anaweza kujiajiri ...akili bado hata baadhi ya wanaomaliza vyuo siku hizi, yaani mtu ambaye unamuona kabisa bado anahitaji sana msaada wa wazazi.
 
Hakuna pointa ya maana hapoo yanii umcheleweshe mtoto kuanza shule ili amalize la saba akiwa mkubwa akusaidie kulima?????[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ishu ya unyanyasaji wa kijinsia hataa wanawake wa miaka 40 huwa wananyanyaswa vizuri tu...

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni mmojawapo wa walioanza la kwanza na miaka 10.

Sio kwamba sikuwa na akili, bali tatizo ni ufupi na mkono ulikuwa mfupi nikiambiwa shika sikio la upande wa pili siwezi.

Toka nina miaka 7 naenda kuanza la kwanza lakini narudishwa.

Wote walionifanyia unyama huu nimewasamehe, nyambafu zenu.

Unforgetable
aise pole
 
Nisome upya madame, nimesema 18yrs kwa watanzania kusema wamekomaa ni uongo mtupu kwanza hata kujielewa 99% hawajielewi hata kujieleza hawajui yaani awe kasoma ama hapana

Kwa ulaya ni tofauti kule kweli 18yrs anajielewa nawe ndio umenambia hiyo kesi 16yrs huko Ulaya sawa niko bongo hapa

Bongo akili zinaanzaga kuja ana 30yrs ndio ana akili za 18yrs wa Ulaya na sehemu nyingine.
Akili hazichangiwi na umri pekee,
Akili zinachangiwa na aina ya malezi+mfumo wa elimu anayopewa katika umri husika
Bora ungesema tuchange mbinu za malezi ili mtoto ajitambue mapema pamoja na mfumo wa elimu uwe rahisi kwa mtoto badala ya kuwaza kwamba solution ni kumchelewesha shule
 
Mimi nilikosa schoolarship ya kwenda kusoma Austria sababu ya umri wangu kuwa mkbwa

Wao walikuwa wanahitaji undergraduate awe na 25 yrs below mimi nlikuwa na 27 na ndio nimemaliza form six

Ni vichwa vya watoto wetu ndio vigumu kutokana na misosi na african genetics thats all
Pole mkuu
 
Akili hazichangiwi na umri pekee,
Akili zinachangiwa na aina ya malezi+mfumo wa elimu anayopewa katika umri husika
Bora ungesema tuchange mbinu za malezi ili mtoto ajitambue mapema pamoja na mfumo wa elimu uwe rahisi kwa mtoto badala ya kuwaza kwamba solution ni kumchelewesha shule
Hivi ukisema unamchelewesha shule anakuwa anawahi nini ikiwa ajira anaisoteamiqkq Minnesota, Bora akimaliza la Saba ashakuwa kijeba ambaye anaweza kuanza uzalishaji kuliko kumaliza shule mapema Alafu anaanza kutunzwa miaka mitatu. Bora serikali ipunguze madarasa lakini umri wa kuanza use miaka kumi
 
Wana JF

Makuzi ya binadamu wa mtanzania yanapitia magumu mengi, hivyo pia akili huchelewa kukomaa kupata uelewa wa kujifunza kitu Kwa umakini. Natoa sababu Kwa nini umri miaka 10 ndio unafaa mtoto kuanza la kwanza.

1. Umri ukiwa miaka kumi mtoto anakuwa amekomaa, huondoa woga na anaweza kuhoji kama kitu sio sahihi.
2. Waliokosa lishe bora huwa ndio wakati ambao makuzi ya akili yanakuwa sawa.
3. Mtoto hadanganyiki kirahisi na akifanyiwa vitu vya unyanyasaji wa kijinsia ana uweza wa kumweleza mama yake au baba yake.
4. Ni umri ambao vipaji huchipuka mtoto kujua anapenda nini Na ana kipaji gani.
5. Kutokukubali kuonewa na mtu yeyote Kwa kuwa sio muoga.
6. Urahisi wa kuweza masomo walimu hawapati shida.
7. Kama shule ipo mbali huyu ndiye mwenye uwezo wa kutembea umbali mrefu.
8. Akimaliza darasa la saba anaweza kusaidia shughuli za kilimo au kuanza kujitegemea
9. Hauhitaji kumlea kama mtoto ikiwa hakufaulu kuendelea na masomo.
10. Kutokana na umri anakuwa amepunguza michezo mingi hatarishi kwa kuwa tayari ana uelewa

Kumbukumbu zinaonyesha wengi waliofanikiwa wengi walianza shule wakiwa na miaka 12.
Toa takwimu.
 
Life span yenyewe miaka 40 halafuu aanze shule na miaka kumi?

Siungi mkono hoja at least ungesema MITANO TENA.
 
ila tuwe wakweli mie wanaposema eti miaka 18 ni mtu mzima kwa watanzania nakataa, kuna watu miaka hiyo hawajielewi (wengi wa watanzania) hata kuhoji kitu hawezi yaani anapelekwa kama ndezi tu.

Mimi napendekeza shule tuanze na miaka 16 maana watanzania akili zetu ni ndogo sana wakati mwingine nahisigi hatuna akili kabisa (tunadaiwa akili)

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wana JF

Makuzi ya binadamu wa mtanzania yanapitia magumu mengi, hivyo pia akili huchelewa kukomaa kupata uelewa wa kujifunza kitu Kwa umakini. Natoa sababu Kwa nini umri miaka 10 ndio unafaa mtoto kuanza la kwanza.

1. Umri ukiwa miaka kumi mtoto anakuwa amekomaa, huondoa woga na anaweza kuhoji kama kitu sio sahihi.
2. Waliokosa lishe bora huwa ndio wakati ambao makuzi ya akili yanakuwa sawa.
3. Mtoto hadanganyiki kirahisi na akifanyiwa vitu vya unyanyasaji wa kijinsia ana uweza wa kumweleza mama yake au baba yake.
4. Ni umri ambao vipaji huchipuka mtoto kujua anapenda nini Na ana kipaji gani.
5. Kutokukubali kuonewa na mtu yeyote Kwa kuwa sio muoga.
6. Urahisi wa kuweza masomo walimu hawapati shida.
7. Kama shule ipo mbali huyu ndiye mwenye uwezo wa kutembea umbali mrefu.
8. Akimaliza darasa la saba anaweza kusaidia shughuli za kilimo au kuanza kujitegemea
9. Hauhitaji kumlea kama mtoto ikiwa hakufaulu kuendelea na masomo.
10. Kutokana na umri anakuwa amepunguza michezo mingi hatarishi kwa kuwa tayari ana uelewa

Kumbukumbu zinaonyesha wengi waliofanikiwa wengi walianza shule wakiwa na miaka 12.
Suala la umri wa mtoto kuanza shule akiwa na miaka mingi au michache kuna faida na changamoto pia.Kwa mfumo wetu wa elimu isiyomtambulisha mtoto juu maisha yake ya baadae imekua changamoto kubwa kwani kundi kubwa la watoto wanamaliza form four halafu haelewi cha kufanya anamsubiri mzazi amwulize kama kuna chuo,shule au course ya kuendelea,tofauti na zamani ambapo wengi walikuwa wanapambana kutafuta mzazi anahangika kumtafutia fedha.

Kwa kuwa elimu yetu haina specialization ndio maana kuna kundi kubwa la watoto wamemaliza form four,form six,chuo kikuu lakini hawaelewi mwelekeo wao na mstakabali wao na wengi utagundua kua hawajapevuka kiakili na bado wana akili ya utegemezi.

Hasara za kuanza shule kwa kuchelewa ni kua mtu anapoteza muda mwingi kusoma makaratasi kuliko uzalishaji hivyo taifa kupata wataalamu watakao hudumu kwa muda mfupi tofauti na zamani ambapo mtu alikua anafanya kazi then anaenda kuboost kimasomo.

Pili mtu anaanza kazi huku akiwa tayari anaandamwa na majukumu mengi ya kiutu uzima hivyo kuathiri muda ambao angeutumia katika uvumbuzi na ugunduzi mbalimbali kwa kushirikiana na wengine,kuzunguka sehemu mbalimbali za nchi na duniani.

Binafsi maoni yangu ni kua kama hatukubadili mfumo wa elimu basi mtoto asome elimu ya awali hadi miaka mitano na wa sita aanze la kwanza lakini mzazi naye apime vizuri kama mtoto wake yuko fiti kuanza darasa la kwanza kwa umri alionao.
Ni hayo tu.
 
Watu tunapeleka watoto wakiwa na miaka mitatu
We unazungumza ujima hapa
 
Wewe akili zako zipo reverse. Sasa hivi watoto wanakomaa ki akili mapema sana kulinganisha wale wa zaman. Mtoto wangu miaka 5 anaanza la kwanza
 
Back
Top Bottom