Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

Labda uongezwe na muda wa kustaafu

Nenda English medium kuna watoto eleven years anamaliza la saba

We Chelewa na mwanao utamchelewesha kila kitu hata scholarship na ukijeba wake hapati
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mkuu umemliza la 7 na miaka 17........ila form one itakuwa hukupiga simu chooni maana hata form 2 wlikuwa wanakuamkia
Form 4 nimemaliza na 21, form 6 na 23-->24, versity na 28-->29.

Ila Mungu hamtupi mja wake, nimemaliza chuo tuu na kupata kazi sikukaa hata mwezi mtaani.

 
Naunga mkono hoja, elimu ya mtaani ina umuhimu mkubwa sana ukizingatia asilimia kubwa ya maisha yetu yatakuwa mtaani kuliko shuleni!.

Kimsingi watoto wakienda shule mapema tunawatengenezea mazingira ya kutegemea elimu ya darasani tu na kutegemea kuajiriwa tu. Fikiria mtoto wa siku hizi akimaliza form asipoendelea anaweza kujiajiri ...akili bado hata baadhi ya wanaomaliza vyuo siku hizi, yaani mtu ambaye unamuona kabisa bado anahitaji sana msaada wa wazazi.
 
Hakuna pointa ya maana hapoo yanii umcheleweshe mtoto kuanza shule ili amalize la saba akiwa mkubwa akusaidie kulima?????[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ishu ya unyanyasaji wa kijinsia hataa wanawake wa miaka 40 huwa wananyanyaswa vizuri tu...

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
aise pole
 
Akili hazichangiwi na umri pekee,
Akili zinachangiwa na aina ya malezi+mfumo wa elimu anayopewa katika umri husika
Bora ungesema tuchange mbinu za malezi ili mtoto ajitambue mapema pamoja na mfumo wa elimu uwe rahisi kwa mtoto badala ya kuwaza kwamba solution ni kumchelewesha shule
 
Pole mkuu
 
Hivi ukisema unamchelewesha shule anakuwa anawahi nini ikiwa ajira anaisoteamiqkq Minnesota, Bora akimaliza la Saba ashakuwa kijeba ambaye anaweza kuanza uzalishaji kuliko kumaliza shule mapema Alafu anaanza kutunzwa miaka mitatu. Bora serikali ipunguze madarasa lakini umri wa kuanza use miaka kumi
 
Toa takwimu.
 
Life span yenyewe miaka 40 halafuu aanze shule na miaka kumi?

Siungi mkono hoja at least ungesema MITANO TENA.
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Suala la umri wa mtoto kuanza shule akiwa na miaka mingi au michache kuna faida na changamoto pia.Kwa mfumo wetu wa elimu isiyomtambulisha mtoto juu maisha yake ya baadae imekua changamoto kubwa kwani kundi kubwa la watoto wanamaliza form four halafu haelewi cha kufanya anamsubiri mzazi amwulize kama kuna chuo,shule au course ya kuendelea,tofauti na zamani ambapo wengi walikuwa wanapambana kutafuta mzazi anahangika kumtafutia fedha.

Kwa kuwa elimu yetu haina specialization ndio maana kuna kundi kubwa la watoto wamemaliza form four,form six,chuo kikuu lakini hawaelewi mwelekeo wao na mstakabali wao na wengi utagundua kua hawajapevuka kiakili na bado wana akili ya utegemezi.

Hasara za kuanza shule kwa kuchelewa ni kua mtu anapoteza muda mwingi kusoma makaratasi kuliko uzalishaji hivyo taifa kupata wataalamu watakao hudumu kwa muda mfupi tofauti na zamani ambapo mtu alikua anafanya kazi then anaenda kuboost kimasomo.

Pili mtu anaanza kazi huku akiwa tayari anaandamwa na majukumu mengi ya kiutu uzima hivyo kuathiri muda ambao angeutumia katika uvumbuzi na ugunduzi mbalimbali kwa kushirikiana na wengine,kuzunguka sehemu mbalimbali za nchi na duniani.

Binafsi maoni yangu ni kua kama hatukubadili mfumo wa elimu basi mtoto asome elimu ya awali hadi miaka mitano na wa sita aanze la kwanza lakini mzazi naye apime vizuri kama mtoto wake yuko fiti kuanza darasa la kwanza kwa umri alionao.
Ni hayo tu.
 
Watu tunapeleka watoto wakiwa na miaka mitatu
We unazungumza ujima hapa
 
Wewe akili zako zipo reverse. Sasa hivi watoto wanakomaa ki akili mapema sana kulinganisha wale wa zaman. Mtoto wangu miaka 5 anaanza la kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…