45 haitowezekana labda 55. Mtu astaafu kwa hiari yaie @ 50, astaafu kwa sheria @ 55. Sababu ni hizi hapa;
Mfumo wetu wa elimu unatuweka sana shuleni, mtu anamaliza degree miaka 25+. Wapunguze muda wa kukaa shule ndipo waje wapunguze muda wa kustaafu. Elimu yetu, miaka 7 shule ya msingi, miaka 4, sekondari, miaka 2 high school, miaka 3-4 chuo, hapo mtoto anaanza shule na miaka sita au saba. π
Mbili ni kwamba, mfumo wetu wa mafao ni "merit-based/time-based" yaani ukikaa kazini miaka mingi na mafao yako ndo yanaongezeka. Ulaya unaweza piga kazi 15 years bado mafao yakawa makubwa na mazuri.
Mtu anakaa shule anasoma mavitu ambayo hayaji kuyatumia kazini, kupoteza muda tuu. Huo muda angekuja kuutumia kuzalisha/ajira. Mtu apate degree miaka 18, aingie kazini, miaka 55 astaafu. Miaka 50 astaafu kwa hiari, achukue chake akafie mbele akiwa na nguvu.