Umri wa kustaafu uwe miaka 45/Utumishi kikomo iwe miaka 15

Ninafikiri kwamba, Umri wa kustaafu utumishi wa umma ushuke na kuwa angalau miaka 45 hivi, ama tuweke ukomo wa utumishi wa umma uwe miaka 15 tu, ili mtu akistaafu apate fursa ya kuyaishi maisha mengine ya kujitafutia kipato nje ya utumishi akiwa na nguvu zake kamili, na kuruhusu kizazi kingine kushika nafasi yake.,

Utafiti wangu usiorasmi unaonyesha wastaafu wengi hawakai miaka 5 hadi 15 hivi baada ya kistaafu wanakumbwa na matatizo ya kiafya ikiwemo msongo wa mawazo na ugumu wa kupata kipato kipya.

Ajira zote ziwe na ukomo ili kutuhusu watu wengi nchi kutumikia serikali ya Tanzania, Wako watu katika utumishi wanavipawa vya biashara na fani nyingine nyingi za kujiajiri, lakini wanauwa talanta zao kwa kumezwa na utumishi hadi uzeeni. Watoke waje mtaani wafanye biashara waonje maisha ya umma wa kawaida.

Tutapunguza sana pengo la walalaheri na walala hoi, hata nidhamu ya utumishi dhidi ya umma itarejea.

Na Yericko Nyerere
Utumishi wa Tanzania ni kuwa
Kasuku
Robot na msukule
Kazi Gani mtu anafanya bila malengo Wala upimwaji wawazi?
 
Ninafikiri kwamba, Umri wa kustaafu utumishi wa umma ushuke na kuwa angalau miaka 45 hivi, ama tuweke ukomo wa utumishi wa umma uwe miaka 15 tu, ili mtu akistaafu apate fursa ya kuyaishi maisha mengine ya kujitafutia kipato nje ya utumishi akiwa na nguvu zake kamili, na kuruhusu kizazi kingine kushika nafasi yake.,

Utafiti wangu usiorasmi unaonyesha wastaafu wengi hawakai miaka 5 hadi 15 hivi baada ya kistaafu wanakumbwa na matatizo ya kiafya ikiwemo msongo wa mawazo na ugumu wa kupata kipato kipya.

Ajira zote ziwe na ukomo ili kutuhusu watu wengi nchi kutumikia serikali ya Tanzania, Wako watu katika utumishi wanavipawa vya biashara na fani nyingine nyingi za kujiajiri, lakini wanauwa talanta zao kwa kumezwa na utumishi hadi uzeeni. Watoke waje mtaani wafanye biashara waonje maisha ya umma wa kawaida.

Tutapunguza sana pengo la walalaheri na walala hoi, hata nidhamu ya utumishi dhidi ya umma itarejea.

Na Yericko Nyerere
Hii inatumika Nchi gani nyingine? Je sheria za Kimataifa za kazi chini ya ILO ndivyo inataka Kwa wanachama wake au ni maoni Yako binafsi?
 
Takwimu hazi support hilo jambo kuleta tija.

Watumishi wa Umma Tanzania ni kama 500,000 kwa nchi ya watu milioni 70. Kuna incentive gani kwa wao kustaafu mapema?

Ingekuwa mimk ndo mtunga sheria ningeondoa umri wa watu kustaafu. Bali ningeruhusu mtu afanye kazi mpaka atavyojiskia kuacha.

We hujiulizi ni kwanini mtu akisfaafu anakaa kidogo na kufariki?
Hoja ya msingi,kwamba watu Laki 5 ndio wanasabanisha wengine wakose Ajira? Typical nonsense

Mtu Kam huyo Yericko tofauti na uandishi wa mambo ya siasa huku kwingine ni mweupe kama tissue.

Unaacha kuangalia tatizo kuu linalosababisha kukosa aggregate demand Ili kusapoti mass employment ya labour na resources unaangaika na jambo ambalo haliwesi kutatua shida.
 
Mawazo ya kinyumenyume. Kumlipa pensheni toka miaka 45 hadi anakufa ni hasara. Pia mtu atajiendelezaje kuwa mbobezi na akifika tu 45 anastaafu?
Na inaonekana hafuatilii au hajui kinachoendelea Duniani.

Nchi nyingi Duniani zinaongeza miaka ya kustaafu Ili kupunguza mzigo wa kulipa wazee harafu eti yeye anasema ipunguze,utalipa watu wasiofanya kazi Hadi lini?
 
45 haitowezekana labda 55. Mtu astaafu kwa hiari yaie @ 50, astaafu kwa sheria @ 55. Sababu ni hizi hapa;

Mfumo wetu wa elimu unatuweka sana shuleni, mtu anamaliza degree miaka 25+. Wapunguze muda wa kukaa shule ndipo waje wapunguze muda wa kustaafu. Elimu yetu, miaka 7 shule ya msingi, miaka 4, sekondari, miaka 2 high school, miaka 3-4 chuo, hapo mtoto anaanza shule na miaka sita au saba. 😁

Mbili ni kwamba, mfumo wetu wa mafao ni "merit-based/time-based" yaani ukikaa kazini miaka mingi na mafao yako ndo yanaongezeka. Ulaya unaweza piga kazi 15 years bado mafao yakawa makubwa na mazuri.

Mtu anakaa shule anasoma mavitu ambayo hayaji kuyatumia kazini, kupoteza muda tuu. Huo muda angekuja kuutumia kuzalisha/ajira. Mtu apate degree miaka 18, aingie kazini, miaka 55 astaafu. Miaka 50 astaafu kwa hiari, achukue chake akafie mbele akiwa na nguvu.
Hili Naunga mkono hoja
 
Kwa uadilifu Gani walionao hao wazee?
Elewa hiyo statement ya mwanzo,wangekuwa sio waadilifu wasingekuwepo kazi, utumishi wa Umma sio msaada Kwa jobless ni inapatikana Kwa merit pale tuu Serikali inapohitaji.
 
Tatizo unasema umri wa watumishi uiishie huko ila viongozi wa nchi na dunia kwa ujumla ni wazee..Imagine wazee wa miaka 70 wanasababisha vita kubwa inayoathiri dunia .
 
Takwimu hazi support hilo jambo kuleta tija.

Watumishi wa Umma Tanzania ni kama 500,000 kwa nchi ya watu milioni 70. Kuna incentive gani kwa wao kustaafu mapema?

Ingekuwa mimk ndo mtunga sheria ningeondoa umri wa watu kustaafu. Bali ningeruhusu mtu afanye kazi mpaka atavyojiskia kuacha.

We hujiulizi ni kwanini mtu akisfaafu anakaa kidogo na kufariki?
haitapendeza hata kidog kumbuka kuna vijana wengi tu waliosoma na wanatafuta ajira alaf mtu ana miaka 75 akae ofisini ata haoni vizur, mleta uzi yupo sahh
 
Huu n upuuzi, kuna watu wanagonga hadi 35 bado wanapambana kupata ajira serikalini
 
haitapendeza hata kidog kumbuka kuna vijana wengi tu waliosoma na wanatafuta ajira alaf mtu ana miaka 75 akae ofisini ata haoni vizur, mleta uzi yupo sahh
Hamna mtu anakaa utumishini mpaka akiwa na miaka 75. Mwisho ni 60 mkuu
 
Ninafikiri kwamba, Umri wa kustaafu utumishi wa umma ushuke na kuwa angalau miaka 45 hivi, ama tuweke ukomo wa utumishi wa umma uwe miaka 15 tu, ili mtu akistaafu apate fursa ya kuyaishi maisha mengine ya kujitafutia kipato nje ya utumishi akiwa na nguvu zake kamili, na kuruhusu kizazi kingine kushika nafasi yake.,

Utafiti wangu usiorasmi unaonyesha wastaafu wengi hawakai miaka 5 hadi 15 hivi baada ya kistaafu wanakumbwa na matatizo ya kiafya ikiwemo msongo wa mawazo na ugumu wa kupata kipato kipya.

Ajira zote ziwe na ukomo ili kutuhusu watu wengi nchi kutumikia serikali ya Tanzania, Wako watu katika utumishi wanavipawa vya biashara na fani nyingine nyingi za kujiajiri, lakini wanauwa talanta zao kwa kumezwa na utumishi hadi uzeeni. Watoke waje mtaani wafanye biashara waonje maisha ya umma wa kawaida.

Tutapunguza sana pengo la walalaheri na walala hoi, hata nidhamu ya utumishi dhidi ya umma itarejea.

Na Yericko Nyerere
Au wewe utakua ni mfanyakazi mwenzangu nini? Mbona umeandika kitu nilicho zoea kukisema nikiwa na staff wenzangu ili kuondoa malalamiko ya vijana mitaani
 
Unatoa hoja bila kutazama mfumo wa elimu yetu unavyochukua muda mrefu kusoma hadi kuhitimu🐒
 
Back
Top Bottom