Umri wa mimba

Umri wa mimba

El uno

Member
Joined
Oct 9, 2018
Posts
93
Reaction score
109
Wakuu habarini,ningependa kupata ufafanuzi,mara ya mwisho mke wangu alipata hedhi 20/4/2023.Ilitakiwa apate hedhi tena 17/5/2023 hakupata .22/5/2023 tukapima kupitia UPT ikaonesha ujauzito .1/8/2023 tukaenda kwa ajili ya clinic kama hudhurio la kwanza.Majibu ya ultrasound yakaonyesha ujauzito una umri wa majuma 16.Ukihesabu kwa kurefer LMP ilitakiwa isome majuma 14 kwa hiyo 1/8/2023.Ninaomba ufafanuzi wa kujua hayo majuma 2 yameongezekaje,
NB: Tulikutana kimwili siku zote za hatari
 
umri wa ujauzito unahesabiwa kuanza siku alipopata hedhi yake ya mwisho. hivyo, kuwa na amani. hizo wiki 16 ni halali.
 
Wakuu habarini,ningependa kupata ufafanuzi,mara ya mwisho mke wangu alipata hedhi 20/4/2023.Ilitakiwa apate hedhi tena 17/5/2023 hakupata .22/5/2023 tukapima kupitia UPT ikaonesha ujauzito .1/8/2023 tukaenda kwa ajili ya clinic kama hudhurio la kwanza.Majibu ya ultrasound yakaonyesha ujauzito una umri wa majuma 16.Ukihesabu kwa kurefer LMP ilitakiwa isome majuma 14 kwa hiyo 1/8/2023.Ninaomba ufafanuzi wa kujua hayo majuma 2 yameongezekaje,
NB: Tulikutana kimwili siku zote za hatari
Mbona ni wiki 16 hesabu kuanzia wiki ya tarehe 20/4 hadi wiki ya tarehe 1/August zitakua wiki 16.
 
Ni week 16 mkuu,
Huo mzigo ni wako kabisaaaaa,
Andaa pampus tu
 
Wakuu habarini,ningependa kupata ufafanuzi,mara ya mwisho mke wangu alipata hedhi 20/4/2023.Ilitakiwa apate hedhi tena 17/5/2023 hakupata .22/5/2023 tukapima kupitia UPT ikaonesha ujauzito .1/8/2023 tukaenda kwa ajili ya clinic kama hudhurio la kwanza.Majibu ya ultrasound yakaonyesha ujauzito una umri wa majuma 16.Ukihesabu kwa kurefer LMP ilitakiwa isome majuma 14 kwa hiyo 1/8/2023.Ninaomba ufafanuzi wa kujua hayo majuma 2 yameongezekaje,
NB: Tulikutana kimwili siku zote za hatari
Kwa unataka kusemaje mkuu ? Humwamini shemeji au?
 
Hapo nimepigia kwa taree uliyo enda clinic mimba ina week 14 na siku5

Screenshot_2023-09-11-10-44-24-98.png
 
Mkuu kwenye mambo ya ultrasound ujauzito unaweza kuwa measured behind yaani siku chache zaidi ya ilivyotakiwa kuwa au siku nyingi zaidi ilivyopaswa kuwa.

Hii ni kwa sababu ya mtoto kuwa mdogo au mtoto kuwa mkubwa kuliko ambapo angepaswa kuwa kwa wakati huo.

Ultrasound unatoa umri wa mimba kwa kuangalia ukubwa wa kiumbe chenyewe.
 
Back
Top Bottom