ngafu . . . .
Pole mwaya, japo umechelewa kumuanzishia kidogo sio mbaya sana. Anza sasa hivi ili akifikisha miaka mitatu umuachishe kabisa hizo diapers(kwanza zinakula hela sana).
Watoto wanajifunza vitu kwa mazoea. Wangu wa miezi 14 last week nilikuwa nimemvua nguo ili akaoge bahati nzuri muda huo huo akaanza kufanya mambo yake. Nikavuta poti haraka nikamkalisha aendelee pale huku namuongelesha "bebé anapupu, tulia -----, unapupu? Sema pupu" na kenyewe kanaitikia tu alafu kakaanza kusema pupu. Leo asubuhi alikuwa na diaper, akanifuata ananiambia "pupu,pupu" huku kanaendelea kufanya mambo yake kwenye pampers. Kwahiyo kameshajua kupupu ni kufanya nini, na kwamba kuna sehemu ya kupupia.
Tenga muda umfundishe mwanao. Usimpigie kelele wakati wa hilo zoezi, mfundishe taratibu kwa upendo huku unamuongelesha kuhusiana na hilo swala.
Tatizo wamama/hata wa dada wa kazi wengi (wale wenye hela ya diapers) wanakwepa hili zoezi kwa uvivu/kinyaa cha kudeal na pupu ya mtoto. Mtu anaogopa mtoto atapupu kwenye poti, chini ama kwenye nguo apate kazi ya kusafisha kwahiyo bora diaper. Akifanya mambo yake anamtoa tu na kumfuta na wipe amemaliza. Hata kuwanawisha na maji wanakwepa. Wanasahau kwamba kuvaa hizo pampers kwa muda mrefu ni adhabu haswa kwenye mazingira ya joto bila, kisababishi cha UTI haswa kama mtoto hasafishwi vizuri kila wakati, bila kusahau gharama. Hizo 4000, 5000, 12000 na 30000 unazonunulia diapers kila wiki/mwezi mnunulie mtoto hata toys tu afurahie.
Tusiwe wa mjini sana kwenye malezi ya watoto wetu. Kinyaa weka pembeni, mpe mtoto raha na uhuru wa kupata upepo kila anapokuwa nyumbani.