Umri wa mtoto kuweza kujisadia sehemu husika

Umri wa mtoto kuweza kujisadia sehemu husika

Mfundishe taratibu ataelewa...hakikisha siku unazokuwa nyumbani unamfundisha na dada wa kazi akiwepo ili ajue kuwa hilo nalo ni jukumu lake.
 
kuendelea kumvalisha pampa pia mtu wa miaka 2 na nusu siyo sawa, mtafutieni vikaptula vingi, akijojoa mnambadilisha, hiyo pia imemlemaza!
 
Kuanzia miaka 2 ni umri sahihi kwa mtoto kujisaidia kwenye pot/choo.Inabidi umfanyie pot training!
  1. Akiamka asubuhi jambo la mwanzo muweke kwenye pot
  2. Usimvulishe pamper kwenye hili zoezi,na muwekee pot eneo la karibu mfano kama part ya michezo yake na umuambie kwamba akitaka kujisaidia ajisaidie kwenye pot.Ni muhimu sana mtoto aelewe matumizi ya hilo pot
  3. Hakika mwanzoni atamwaga mkojo sehemu tofauti na hata atajinyea lkn ukishaona anaanza process hio we mkalishe kwenye pot.Kwasababu mtoto ameshazoea kujisaidia kwa uhuru kuna uwezekano pia asiweze kujizuia akishikwa na haja yoyote mpaka afikie pot,EPUKA KUWA MKALI HALI HII IKITOKEA CHUKULIA NI AJALI TU!
  4. Ni vizuri ukimuwekea rutine vilevile mfano kila baada ya mlo unamkalisha kwenye pot au kabla ya kulala.
  5. Wakati wa kulala ni vyema akiendelea kutumia pampers mpaka utakapoona amelala usiku kucha mara kadhaa bila kujikojolea.

vizuri sana,mi wa kwangu kwa kweli huwa nawaanzishia wakiwa na miezi minne kuwaweka kwenye poti akifikisha mwaka na nusu hata kitandani hakojoi anakuwa amesha jicondition huwa naamka usiku kuwakojolesha.
 
Kuanzia miaka 2 ni umri sahihi kwa mtoto kujisaidia kwenye pot/choo.Inabidi umfanyie pot training!
  1. Akiamka asubuhi jambo la mwanzo muweke kwenye pot
  2. Usimvulishe pamper kwenye hili zoezi,na muwekee pot eneo la karibu mfano kama part ya michezo yake na umuambie kwamba akitaka kujisaidia ajisaidie kwenye pot.Ni muhimu sana mtoto aelewe matumizi ya hilo pot
  3. Hakika mwanzoni atamwaga mkojo sehemu tofauti na hata atajinyea lkn ukishaona anaanza process hio we mkalishe kwenye pot.Kwasababu mtoto ameshazoea kujisaidia kwa uhuru kuna uwezekano pia asiweze kujizuia akishikwa na haja yoyote mpaka afikie pot,EPUKA KUWA MKALI HALI HII IKITOKEA CHUKULIA NI AJALI TU!
  4. Ni vizuri ukimuwekea rutine vilevile mfano kila baada ya mlo unamkalisha kwenye pot au kabla ya kulala.
  5. Wakati wa kulala ni vyema akiendelea kutumia pampers mpaka utakapoona amelala usiku kucha mara kadhaa bila kujikojolea.

Aisee umenisaidia sana maana nimeumiza sana kichwa na mwanangu anafika miaka miwili mwezi wa tano lakini kamechangamka mapema
 
Kuna jamaa aliwahi niambia, "alimtrain" mwanawe kipindi kirefu kutumia "pot" bila mafanikio, siku moja akamweka mwanawe pembeni ashuhudie akakaa yeye kwenye "pot" akadondosha mambo! "Pot" lilivyosafishwa tu, halikupita saa moja mtoto nae akalikalia akapiga mambo...baada ya hapo usiulize, mtoto na "pot", "pot" na yeye...

Sometimes creativity matters alot...
 
Mfundishe taratibu ataelewa...hakikisha siku unazokuwa nyumbani unamfundisha na dada wa kazi akiwepo ili ajue kuwa hilo nalo ni jukumu lake.

Ushindwe kumlea mwanao afu unakuja kifua mbele Eti dada wa kazi ajue kua ni jikumu lake
Lolz............mama ndie mwenye jukumu lakujua mwanae anakula nn.....analala wapi.....choo chake kikoje anapata choo kizur?

Lakn cha ajabu wanawake wanakwepa majukum yao na kuwapatia wadada wakaz lol kwa sh ngap haswa mnayowalipa
 
Mfundishe tu ataelewa kidogo kidogo
Umleavyo.ndivyo akuavyo
 
ngafu . . . .
Pole mwaya, japo umechelewa kumuanzishia kidogo sio mbaya sana. Anza sasa hivi ili akifikisha miaka mitatu umuachishe kabisa hizo diapers(kwanza zinakula hela sana).

Watoto wanajifunza vitu kwa mazoea. Wangu wa miezi 14 last week nilikuwa nimemvua nguo ili akaoge bahati nzuri muda huo huo akaanza kufanya mambo yake. Nikavuta poti haraka nikamkalisha aendelee pale huku namuongelesha "bebé anapupu, tulia -----, unapupu? Sema pupu" na kenyewe kanaitikia tu alafu kakaanza kusema pupu. Leo asubuhi alikuwa na diaper, akanifuata ananiambia "pupu,pupu" huku kanaendelea kufanya mambo yake kwenye pampers. Kwahiyo kameshajua kupupu ni kufanya nini, na kwamba kuna sehemu ya kupupia.

Tenga muda umfundishe mwanao. Usimpigie kelele wakati wa hilo zoezi, mfundishe taratibu kwa upendo huku unamuongelesha kuhusiana na hilo swala.

Tatizo wamama/hata wa dada wa kazi wengi (wale wenye hela ya diapers) wanakwepa hili zoezi kwa uvivu/kinyaa cha kudeal na pupu ya mtoto. Mtu anaogopa mtoto atapupu kwenye poti, chini ama kwenye nguo apate kazi ya kusafisha kwahiyo bora diaper. Akifanya mambo yake anamtoa tu na kumfuta na wipe amemaliza. Hata kuwanawisha na maji wanakwepa. Wanasahau kwamba kuvaa hizo pampers kwa muda mrefu ni adhabu haswa kwenye mazingira ya joto bila, kisababishi cha UTI haswa kama mtoto hasafishwi vizuri kila wakati, bila kusahau gharama. Hizo 4000, 5000, 12000 na 30000 unazonunulia diapers kila wiki/mwezi mnunulie mtoto hata toys tu afurahie.

Tusiwe wa mjini sana kwenye malezi ya watoto wetu. Kinyaa weka pembeni, mpe mtoto raha na uhuru wa kupata upepo kila anapokuwa nyumbani.
 
Last edited by a moderator:
gorgeousmimi nashukuru sana,nilianza kumzoesha mwanangu kutumia poti badala ya pampers na sahivi ameshazoea kabisaa hata ikitokea nimemvalisha pampers hajisaidii mpaka nimtoe hiyo pampers.
Ubarikiwe sana sana
Cc: Lizzy
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom