Umri wa mtu kuteuliwa kushika nafasi yoyote Serikalini uwe ni walau kuanzia miaka 35

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Naona wakati umefika tuweke kigezo cha umri kwa watu wanaoteeuliwa kushika nafasi au madaraka makubwa serikalini na katika Utumishi wa umma.

Katika nchi yetu, uteuzi hufanywa zaidi na Raisi na wateule wa Raisi wote hupewa dhamana au madaraka makubwa na hivyo kuna uwezekano baadhi hupewa madaraka makubwa kuzidi umri wao( wanakuwa hawajakomaa).

Vijana wengi wa kitanzania chini ya miaka 35 wanakuwa bado wanasumbuliwa na ujana na hivyo inakuwa rahisi kulewa madraka na pia ni rahisi zaidi kwa watawala wabovu kuwatu vijana kwa mambo yaliyo kinyume na maadili yetu na hata utu wa mwanadamu.

Mbali na kusumbuliwa na ujana( kupsndisha mabega, n.k) ni wazi pia watawala huwachukulia vijana wanaowapa madaraka kama watoto wao wa kuwazaa hivyo inakuwa rahisi kuwatumia kwa mambo ya hovyo.

Ukiacha katika majeshi ambako amri ndio hutawala hivyo inakuwa rahisi hata kuwatumia watu wenye umri mkubwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na Sheria za nchi na maadili ya kitabzania, nii vigumu kwa watawala kuwatumia wateule wenye umri sawa na wao kutenda mambo ya hovyo kama wanavyoweza kuwaagiza au kuwatumia vijana waliowapa madaraka.

Hivyo, japo si vijana wote wanakosa busara za uongozi na wanaoweza kutumika vibaya, napendekeza umri wa wateule wote wa Raisi nchi hii kuanzia walau miaka 35 na ikibidi zaidi ya hapo.

Najua wako vijana wanafanya vizuri tu katika uongozi, ila ni bora tuweke hiki kigezo ili kuondoa au kupunguza risk ya kuwa na vijana wanaotumika vibaya na watawala au kuwa na vijana ambao bado hawajakomaa kupewa madaraka makubwa ya kuteuliwa na Raisi au Mamlaka nyingine za uteuzi.

Vijana wengi wa kitanzania wa leo hii sio sawa na wale wa miaka ya nyuma walioweza kupewa madaraka makubwa na wasiwaangushe waliowapa madaraka.

Kuhusu viongozi wa kuchaguliwa, hiyo ni agenda nyingine ingawa bado agenda hiyo inaweza ku-fit hata katika hii mad na hivyo hapa sitaiongelea.

Nawasilisha.
 
Akili ya mtu ni ya mtu tu na huwa inatofautiana kati ya mtu na mtu.

Miaka 35 wewe ni mzee maisha yanaenda kasi sana.

Watu wanaongoza kaya zao wana MIAKA 10 na kaya zimefika (Kaya zinazoongozwa na watoto).

Sasa kijeba huyu ana MIAKA zaidi ya 25 umepewa madaraka amembwelambwela tu.

Hiyo ni tabia ya ulevi wa kawaida kabisa wa madaraka ambao haujalishi umri, jinsi, kabila, chama wala mambo yanayofanana na hayo wa mtu husika
 
Ubaguzi wa Kiumri umekatazwa kwenye Katiba ya Jamhuri.
 
Akili ya mtu ni ya mtu tu na huwa inatofautiana kati ya mtu na mtu
Miaka 35 wewe ni mzee maisha yanaenda kasi sana...
Hao kina Baahite na Sabaya ni zao tu la kupewa madaraka yanayowazidi umri.
 
Ni kweli kabisa. Pia na kufanya conclusion kutokea specific to majority.
Ni kweli kabisa na ndio maana hata kwenye umri wa kugombea uraisi wakafanya hivyo na wakaaingiza mpaka kwenye katiba na mkapitisha.
 
Mbona kwenye uraisi katiba hiyo hiyo imeweka limit kwenye umri wa kugombea uraisi?

Katiba kama hiyo ingekuwapo wakati Tanganyika inapata uhuru, Nyerere asingekuwa kiongozi mkuu wa serikali.

Hivyo hicho kipengele cha umri kwenye katiba kinapaswa kuondolewa na chenyewe.
 
Ndio maana nikisema vijana wa siku hizi sio sawa na wale wa enzi hizo.

Vijana wa leo wengi busara zero na kunyanyua mabega.

Watu kama kina Happy,Muro, Kheri James na wengineo wanaotoka UVCCM ni ushahidi tu vijana wengi wa leo hawapaswi kupewa madataka makubwa.
 
Mimi kizingiti cha umri sikubaliani nacho kwa ngazi yoyote ya uongozi. Muhimu kuzingatia sifa zingine.
Haya ni maoni binafsi.
Hukubaliana nacho ila huo ndio ukweli

Vijana wengi ndio sasa wanatumika vibaya kiutwala na ndio wanaongooza kwa ulevi wa madaraka japo pia wako wazee wanaolewa madaraka mfano Jiwe.
 
Miaka 30 is fair enough kama kuna Institutions imara za kuwadhibiti viongozi pale wanapoanza kukengeuka. Ushenzi wa mtu kama Sabaya na Bashite ulikuwa wazi awali kabisa ila wakalindwa (or rather wahusika wakaogopa kudeal nao kwa kuwa mteuzi wao alikuwa Rais na mtetezi wao)

Mtu mshenzi ni mshenzi tu hata akiwa na miaka 70
 
Naona wakati umefika tuweke kigezo cha umri kwa watu wanaoteeuliwa kushika nafasi au madaraka makubwa serikalini na katika Utumishi wa umma...
Umezungumza jambo la msingi sana. Nafasi za kiutawala na uongozi wa juu unahitaji umri uliopevuka. Hivi ndivyo ilivyo, hata kwenye vitabu vitakatifu Mwenyezimungu aliwapa utume na unabii wale waliofikia miaka 40.

Hii inamaanisha *Age matters. Bila shaka kuna haja ya kuliangalia hili kwa jicho la ziada kwa wenye mamlaka ya uteuzi.
 
Hukubaliana nacho ila huo ndio ukweli

Vijana wengi ndio sasa wanatumika vibaya kiutwala na ndio wanaongooza kwa ulevi wa madaraka japo pia wako wazee wanaolewa madaraka mfano Jiwe.
Jiwe hakuwahi kuwa mlevi.
Ila tukitumia mantiki hiyo ndio unaona kwamba umri sio tatizo. Ni hulka ya mtu ndio hupelekea yeye kulewa au vinginevyo.
Huwa nasema maisha ni yale yale. Mfano kama ulikuwa malaya enzi zako probably hata ukizeeka unaendelea kuwa hivyo.
 
Tukiweka umri wa chini, shurti tuweke na umri wa juu. Hakuna mantiki ya kuweka kigezo cha umri.

Kadhalika kigezo cha elimu hakifai kuwamo. Kwa maoni yangu mtu yeyote aruhusiwe kugombea. Mzee sana. Mdogo sana. Msomi sana. asiyesoma kabisa.
 
Hahahhhaa... Hilo sasa litakua taifa la wendawazimu..!!
 
Naona wakati umefika tuweke kigezo cha umri kwa watu wanaoteeuliwa kushika nafasi au madaraka makubwa serikalini na katika Utumishi wa umma...
Siyo wazee au watu wazima wote wana busara au umakini katika uongozi. Hata vijana wapumbavu wanazeeka na upumbavu wao!

Kikubwa ukipewa madaraka ufuate sheria. Ukishindwa kufuata sheria..basi sheria ichukue mkondo wake ukiwa madarakani au umeondolewa madarakani.
 
Jiwe hakuwahi kuwa mlevi.
Ila tukitumia mantiki hiyo ndio unaona kwamba umri sio tatizo. Ni hulka ya mtu ndio hupelekea yeye kulewa au vinginevyo.
Huwa nasema maisha ni yale yale. Mfano kama ulikuwa malaya enzi zako probably hata ukizeeka unaendelea kuwa hivyo.
Jiwe alikuwa mlevi wa madaraka na hawa akina Saambaya ni zao lake
 
Ndio maana nikisema vijana wa siku hizi sio sawa na wale wa enzi hizo.

Vijana wa leo wengi busara zero na kunyanyua mabega.

Watu kama kina Happy,Muro, Kheri James na wengineo wanaotoka UVCCM ni ushahidi tu vijana wengi wa leo hawapaswi kupewa madataka makubwa.
Inabidi mtu atumikie kwanza nafasi nyingine then aje ateuliwe.Vyeo vya kuteuliwa isiwe kama ajira ya msingi
 
Naona wakati umefika tuweke kigezo cha umri kwa watu wanaoteeuliwa kushika nafasi au madaraka makubwa serikalini na katika Utumishi wa umma.

Katika nchi yetu, uteuzi hufanywa zaidi na Raisi na wateule wa Raisi wote hupewa dhamana au madaraka makubwa na hivyo kuna uwezekano baadhi hupewa madaraka makubwa kuzidi umri wao( wanakuwa hawajakomaa).

Vijana wengi wa kitanzania chini ya miaka 35 wanakuwa bado wanasumbuliwa na ujana na hivyo inakuwa rahisi kulewa madraka na pia ni rahisi zaidi kwa watawala wabovu kuwatu vijana kwa mambo yaliyo kinyume na maadili yetu na hata utu wa mwanadamu.

Mbali na kusumbuliwa na ujana( kupsndisha mabega, n.k) ni wazi pia watawala huwachukulia vijana wanaowapa madaraka kama watoto wao wa kuwazaa hivyo inakuwa rahisi kuwatumia kwa mambo ya hovyo.

Ukiacha katika majeshi ambako amri ndio hutawala hivyo inakuwa rahisi hata kuwatumia watu wenye umri mkubwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na sheria za nchi na maadili ya kitabzania, nii vigumu kwa watawala kuwatumia wateule wenye umri sawa na wao kutenda mambo ya hovyo kama wanavyoweza kuwaagiza au kuwatumia vijana waliowapa madaraka.

Hivyo, japo si vijana wote wanakosa busara za uongozi na wanaoweza kutumika vibaya, napendekeza umri wa wateule wote wa Raisi nchi hii kuanzia walau miaka 35 na ikibidi zaidi ya hapo.

Najua wako vijana wanafanya vizuri tu katika uongozi, ila ni bora tuweke hiki kigezo ili kuondoa au kupunguza risk ya kuwa na vijana wanaotumika vibaya na watawala au kuwa na vijana ambao bado hawajakomaa kupewa madaraka makubwa ya kuteuliwa na Raisi au Mamlaka nyingine za uteuzi.

Vijana wengi wa kitanzania wa leo hii sio sawa na wale wa miaka ya nyuma walioweza kupewa madaraka makubwa na wasiwaangushe waliowapa madaraka.

Kuhusu viongozi wa kuchaguliwa, hiyo ni agenda nyingine ingawa bado agenda hiyo inaweza ku-fit hata katika hii mad na hivyo hapa sitaiongelea.

Nawasilisha.
Ndugai anazaidi ya miaka 61 mbona mambo ni ya hovyo? ni akili ya mtu tu ndiyo inaweza kumtuma kufanya ujinga na siyo umri
 
Back
Top Bottom