Naona wakati umefika tuweke kigezo cha umri kwa watu wanaoteeuliwa kushika nafasi au madaraka makubwa serikalini na katika Utumishi wa umma.
Katika nchi yetu, uteuzi hufanywa zaidi na Raisi na wateule wa Raisi wote hupewa dhamana au madaraka makubwa na hivyo kuna uwezekano baadhi hupewa madaraka makubwa kuzidi umri wao( wanakuwa hawajakomaa).
Vijana wengi wa kitanzania chini ya miaka 35 wanakuwa bado wanasumbuliwa na ujana na hivyo inakuwa rahisi kulewa madraka na pia ni rahisi zaidi kwa watawala wabovu kuwatu vijana kwa mambo yaliyo kinyume na maadili yetu na hata utu wa mwanadamu.
Mbali na kusumbuliwa na ujana( kupsndisha mabega, n.k) ni wazi pia watawala huwachukulia vijana wanaowapa madaraka kama watoto wao wa kuwazaa hivyo inakuwa rahisi kuwatumia kwa mambo ya hovyo.
Ukiacha katika majeshi ambako amri ndio hutawala hivyo inakuwa rahisi hata kuwatumia watu wenye umri mkubwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na sheria za nchi na maadili ya kitabzania, nii vigumu kwa watawala kuwatumia wateule wenye umri sawa na wao kutenda mambo ya hovyo kama wanavyoweza kuwaagiza au kuwatumia vijana waliowapa madaraka.
Hivyo, japo si vijana wote wanakosa busara za uongozi na wanaoweza kutumika vibaya, napendekeza umri wa wateule wote wa Raisi nchi hii kuanzia walau miaka 35 na ikibidi zaidi ya hapo.
Najua wako vijana wanafanya vizuri tu katika uongozi, ila ni bora tuweke hiki kigezo ili kuondoa au kupunguza risk ya kuwa na vijana wanaotumika vibaya na watawala au kuwa na vijana ambao bado hawajakomaa kupewa madaraka makubwa ya kuteuliwa na Raisi au Mamlaka nyingine za uteuzi.
Vijana wengi wa kitanzania wa leo hii sio sawa na wale wa miaka ya nyuma walioweza kupewa madaraka makubwa na wasiwaangushe waliowapa madaraka.
Kuhusu viongozi wa kuchaguliwa, hiyo ni agenda nyingine ingawa bado agenda hiyo inaweza ku-fit hata katika hii mad na hivyo hapa sitaiongelea.
Nawasilisha.