Umri wako sio gereza, acha kujihukumu na ondoa hiyo fikra

Umri wako sio gereza, acha kujihukumu na ondoa hiyo fikra

True
Ni kweli umri una nafasi yake, lakini haujaumbwa kuwa mtego.
Kama kila kitu kingehesabiwa kwa kalenda ya binadamu,
Tungesema Abraham alichemka kumzaa Isaka akiwa mzee.
Lakini kumbe muda wa Mungu huwa hauna hofu ya "deadlines."

E
 
Asante ndio maana wanasiasa hukuta waapambana hata kama ana miaka 70 plus.

Unaweza kujiuliza huyu anapambana ili aende wapi wakati muda wa kuondoka duniani unakaribia?

Watu waliofanikiwa duniani hawana kizingiti cha umri kwenye harakati zao.
Rugemalila alikuwa bilionea, ungeweza kusema kwanini alikubali kufungwa wakati angetoa hongo akaondoka jela la mahabusu? Vijana wangesema bora uhonge utoke lakini kwa matajiri ni tofauti.
Kabisaa mkuu
 
Yaani bana hata sizingatii mi nawaza nipambane tuuu badae niwe na familia yangu huko kijijini maeneo ya pwani kama si mkuranga basi itakua chanika

Au kisarawe.. huko najenga naishi ntamalizia huko life langu na kama nitapangiwa dodoma kikazi basi takaa huko kule juu karibu na chuo
Naaam, naona kabisa mkuu hutaki makelel ya town🤣
 
Tulia ufike third floor ndo utaelewa kwanini watu huwa tunakataa umri wetu.....
Hapana siwezi kataa hata kidogo mimi...
Kingine maisha haya haya bana anything can happen mi selewi wala.nn huwenda hata nisifike huko third floor..

Sema uvivu wa kutembeza mboga mboga hutakiwi kua nao 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mchawi ni afya njema tu. Ukiwa na afya ya mwili na akili, hata uwe na miaka 90 bado unaweza kufanya utakacho na kuishi upendavyo.

Tatizo bana nchi zetu hizi ukishafikisha miaka 55+ unashangaa kila aina ya magonjwa yanaanza kukuandama na ni kama vile hua hamna solution. Ukifanikiwa kugonga 70 ni bahati😐

Wakati kuna nchi unakuta watu kugonga miaka 85 mpaka 100 ni kawaida kabisa.

Kiukweli mkuu, umesema ukweli mtupu, mchawi wa maisha mazuri ni afya bora ya mwili na akili.
Ukiwa na afya
Miaka 90 unaiangalia kama bonus tu ya michezo, siyo adhabu ya kungoja siku ya mwisho!

Ni kwamba kwenye nchi zetu hizi, ukifika miaka 55 tu – boom!
Pressure inakuja. Kisukari kinatuma salamu. Magoti yanaanza kushtaki.
Na ukisema uende hospitali, madaktari wanakutazama kama “zile siku zako” zimewadia.
Sio tiba—ni maandalizi ya kukubaliana na hatima.
🚫 Hili jambo si la asili.
🚫wala Sio la Mungu.
👉 Ni udhaifu wa mifumo yetu tu.

Kuna nchi watu wanakula vizuri, wanatembea kila siku, wanapewa matibabu bora,
Na zaidi ya yote – wanaishi maisha yenye amani ya moyo.
Si ajabu kwao mtu kuwa na miaka 85 hadi 100 na bado anahudhuria dansi za weekend.

Sasa sisi huku, tukifika miaka 60, mtu anatamani aombe dua ya kuondoka kwa heshima.
Kwa sababu amechoka sio kwa mwili tu – bali kwa kupuuzwa na mfumo, na maisha yasiyo na thamani tena
. Afya ni uhuru. Afya ni nafasi ya kuishi ndoto hata ukiwa na nywele nyeupe!
 
Aisee si kweli nyakati ni muhimu sana kuzitambua, siyo kwamba inakua mzigo hapana Ila umri inasaidia kupangilia vitu,
Huwezi kua na miaka 45 unafanya vitu ambavyo angefanya mtu mwenye miaka 25
 
Aisee si kweli nyakati ni muhimu sana kuzitambua, siyo kwamba inakua mzigo hapana Ila umri inasaidia kupangilia vitu,
Huwezi kua na miaka 45 unafanya vitu ambavyo angefanya mtu mwenye miaka 25
Wakati huo pia usishau kwamba mipango si matumizi!
Hakuna mtu hapendi asi achieve vile anavyovitamani kwa wakati! Wote tunapenda hivyo, ila muda usigeuke kifungo! Thts my point
 
Mungu akubariki sana mkuu kwa kukiandika hiki, maneno uliyoandika yanaweza kuwa tiba bora sana kwenye maisha ya wengi humu.

Wengi wanapitia/tunapitia sana nyakati zakuona muda umekutupa mkono na umeshapoteza ilihali kumbe unanafasi ya kujipanga na kusonga mbele.
 
Mungu akubariki sana mkuu kwa kukiandika hiki, maneno uliyoandika yanaweza kuwa tiba bora sana kwenye maisha ya wengi humu.

Wengi wanapitia/tunapitia sana nyakati zakuona muda umekutupa mkono na umeshapoteza ilihali kumbe unanafasi ya kujipanga na kusonga mbele.
🙏🙏 lets Hustle hard brother
 
Mchawi ni afya njema tu. Ukiwa na afya ya mwili na akili, hata uwe na miaka 90 bado unaweza kufanya utakacho na kuishi upendavyo.

Tatizo bana nchi zetu hizi ukishafikisha miaka 55+ unashangaa kila aina ya magonjwa yanaanza kukuandama na ni kama vile hua hamna solution. Ukifanikiwa kugonga 70 ni bahati😐

Wakati kuna nchi unakuta watu kugonga miaka 85 mpaka 100 ni kawaida kabisa.
Kuna bibi mmoja mjapani ana miaka 100 na bado anafanya kazi saloon huku bongo huo umri mtu anabebwa kupeleka nje kuanikwa na kurudishwa ndani sijui tunakwama wapi.
 
USIACHE UMRI UAMUE HATMA YAKO...

Unaweza kuanza kwa bidii, ukiwa na miaka 29 tu—
Ukajipanga, ukajiamini, ukajenga ndoto zako kimyakimya, baada ya kupoteza kwenye 18-25s

Miaka 31, ukaoa au kuolewa, maisha yakawa tulivu alafu poa tu yani.
Sio mchongo, bali upendo wa kweli, msingi wa kesho yako.

Ukafika 35, ghafla, ukapiga chini...
Kila kitu kikaenda mrama, tofauti na ulivyopanga,
Mungu ukaona amekaa kimya, hata mganga akawa hayupo kabisa.

Lakini miaka 38, ukajikongoja, ukanyanyuka polepole—
Kidogo kidogo, ukaanza kutabasamu tena,
Na amini, kusimama tena inawezekana!

Miaka 41 ikakukaribisha na dhoruba mpya,
Biashara ikayeyuka, marafiki wakawa hewa,
Hata tumaini likatoweka, ukatamani hata kifo kikutie nguvu
Lakini roho ikakuambia: "Don't fool yourself. Hujazaliwq kuwa Mac muga, Simama. Go for it again!"

Ukahangaika huku na kule...
Na hatimaye YOU MADE IT!

Miaka 43, ukaangalia nyuma ukasema:
"Kweli, pale nilipoanguka siyo mwisho wangu!"
Ukafanya RESET ya maisha—ukajenga upya kwa akili na neema.

Na ulipofika 45, maisha yakawa tulivu,
Kila kitu kikawa sawa, kama hakukuwa na mshindani,
Unajipigia zako bata kimya kimya! Yaan kama
Hakukuwa na historia mbaya—ni wewe tu na ushindi wako.

Kimya kimya, bila kelele, ukatoboa mzima mzima...

Sasa ni nani aliyesema umekwisha, ilhali bado unapumua?
Nani huyo anayeweza kuandika mwisho wa hadithi yako, wakati mwandishi bado ni wewe?


Maisha hayana ratiba moja kwa wote...
Kuchelewa si kushindwa, kuanguka si kufa...
Mradi unapumua—BADO UNA NAFASI YA KUSHINDA!
Mkuu umepitia hii experience au ni motivation speaker Tu?
 
Back
Top Bottom