Umri wako sio gereza, acha kujihukumu na ondoa hiyo fikra

True
Ni kweli umri una nafasi yake, lakini haujaumbwa kuwa mtego.
Kama kila kitu kingehesabiwa kwa kalenda ya binadamu,
Tungesema Abraham alichemka kumzaa Isaka akiwa mzee.
Lakini kumbe muda wa Mungu huwa hauna hofu ya "deadlines."

E
 
Kabisaa mkuu
 
Naaam, naona kabisa mkuu hutaki makelel ya town🤣
 
Tulia ufike third floor ndo utaelewa kwanini watu huwa tunakataa umri wetu.....
Hapana siwezi kataa hata kidogo mimi...
Kingine maisha haya haya bana anything can happen mi selewi wala.nn huwenda hata nisifike huko third floor..

Sema uvivu wa kutembeza mboga mboga hutakiwi kua nao 🤣🤣🤣🤣🤣
 

Kiukweli mkuu, umesema ukweli mtupu, mchawi wa maisha mazuri ni afya bora ya mwili na akili.
Ukiwa na afya
Miaka 90 unaiangalia kama bonus tu ya michezo, siyo adhabu ya kungoja siku ya mwisho!

Ni kwamba kwenye nchi zetu hizi, ukifika miaka 55 tu – boom!
Pressure inakuja. Kisukari kinatuma salamu. Magoti yanaanza kushtaki.
Na ukisema uende hospitali, madaktari wanakutazama kama “zile siku zako” zimewadia.
Sio tiba—ni maandalizi ya kukubaliana na hatima.
🚫 Hili jambo si la asili.
🚫wala Sio la Mungu.
👉 Ni udhaifu wa mifumo yetu tu.

Kuna nchi watu wanakula vizuri, wanatembea kila siku, wanapewa matibabu bora,
Na zaidi ya yote – wanaishi maisha yenye amani ya moyo.
Si ajabu kwao mtu kuwa na miaka 85 hadi 100 na bado anahudhuria dansi za weekend.

Sasa sisi huku, tukifika miaka 60, mtu anatamani aombe dua ya kuondoka kwa heshima.
Kwa sababu amechoka sio kwa mwili tu – bali kwa kupuuzwa na mfumo, na maisha yasiyo na thamani tena
. Afya ni uhuru. Afya ni nafasi ya kuishi ndoto hata ukiwa na nywele nyeupe!
 
Aisee si kweli nyakati ni muhimu sana kuzitambua, siyo kwamba inakua mzigo hapana Ila umri inasaidia kupangilia vitu,
Huwezi kua na miaka 45 unafanya vitu ambavyo angefanya mtu mwenye miaka 25
 
Aisee si kweli nyakati ni muhimu sana kuzitambua, siyo kwamba inakua mzigo hapana Ila umri inasaidia kupangilia vitu,
Huwezi kua na miaka 45 unafanya vitu ambavyo angefanya mtu mwenye miaka 25
Wakati huo pia usishau kwamba mipango si matumizi!
Hakuna mtu hapendi asi achieve vile anavyovitamani kwa wakati! Wote tunapenda hivyo, ila muda usigeuke kifungo! Thts my point
 
Mungu akubariki sana mkuu kwa kukiandika hiki, maneno uliyoandika yanaweza kuwa tiba bora sana kwenye maisha ya wengi humu.

Wengi wanapitia/tunapitia sana nyakati zakuona muda umekutupa mkono na umeshapoteza ilihali kumbe unanafasi ya kujipanga na kusonga mbele.
 
🙏🙏 lets Hustle hard brother
 
Kuna bibi mmoja mjapani ana miaka 100 na bado anafanya kazi saloon huku bongo huo umri mtu anabebwa kupeleka nje kuanikwa na kurudishwa ndani sijui tunakwama wapi.
 
Mkuu umepitia hii experience au ni motivation speaker Tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…