UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,753
- 12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!
Kuna Vijana baadhi ambao wamekuwa wakinifata pm Kwa kuniomba angalau niwape kazi au Vibarua kama vinapatikana!
Ndugu zangu, kwanza nawashukuru Kwa kudhani huenda Mimi UMUGHAKA naweza kuwasaidia, yawezekana ni taswira yangu hapa JF Kwa Vijana wengi ndio inapalekea hadi kuamini na kukubalika miongoni mwa Vijana wengi, Niwaambie tu ndugu zangu, Mimi pia ni muhangaikaji mwenzenu nisiyekuwa na lolote la maana!
Mimi binafsi ni muendesha Bodaboda tu ambaye ni deiwaka tu hapa mjini, uzuri ni kwamba huwa sichagui labda kazi inikimbie! Hivyo ndugu zangu siko kama mnavyonidhania! Huenda baadhi yenu mnaniona kama UMUGHAKA ni mzugaji tu atakuwa na kazi nzuri serikalini au kwenye taasisi fulani,hapana wanangu Mimi pia ni Hustler mwenzenu huku kitaani!
Niwaombe tu ndugu zangu ambao mnayajua machimbo ya Kazi za kideiwaka iwe UFUNDI, SAIDIA FUNDI, VIWANDANI, MASHAMBANI N.K hebu wasaidieni Vijana wenzenu maana Kuna Vijana hapa JF wanapitia msoto heavy,usione watu wanajichatisha hapa JF kila siku lakini Hali zao ni mbaya mno!
JF imekuwa ni sehemu ya kuwapatia faraja angalau kila wanapopekua nyuzi kadhaa,lakini kiukweli watu au Vijana wengi humu ndani Wana Hali mbaya! Tafadhali kama unaouwezo wa kuisaidia saidia bila kuwachoka Vijana!
Kama Kuna sehemu unapiga kazi za nguvu na bado nafasi zipo,basi washirikishe Vijana wenzio hapa JF Ili nao wakapambane,Vijana wanataka kazi lakini Kuna muda wanatafuta bila mafanikio,hawapaswi kusimangwa!
Kama Kuna fursa huko washitue Wana waje muipige wote,TUACHE UBINAFSI NA UCHOYO!