SoC04 Umuhimu wa elimu kuhusu magonjwa ya zinaa katika jamii

SoC04 Umuhimu wa elimu kuhusu magonjwa ya zinaa katika jamii

Tanzania Tuitakayo competition threads

Green_swaggz_tz

New Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Mdau wa SoCO4 mwenye namba ya simu 0765853732.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la waathirika wa magonjwa mbalimbali ya zinaa ikiwemo Virusi vya UKIMWI, Kisonono, kaswende, Chlamydia, na mengine.

Hii ni kutokana na kuongezeka kwa ngono zembe, maelezo mabovu ya watoto, ubakaji na ulawiti, pamoja na ongezeko la biashara ya ngono katika miji mbalimbali na vijana wenye umri wa miaka Kati ya miaka 14 mpaka 49 wakiwa katika hatari zaid ya kuathirika kwani ndiyo umri ambao hujihusisha Sana na masuala ya mapenzi ukilinganisha na umri mwingine.

Hii inaathiri nguvu kazi ya taifa la kesho kwa kiasi kikubwa, pia inasababisha serikali kutumia fedha nyingi sana katika kugharamia matibabu ya magonjwa haya mfano mzuri Virusi vya UKIMWI.

Nini kifanyike? Ili kukabiliana na changamoto hii;

✓Ni vema serikali ikaanzisha vipindi kwenye vyombo vya habari kuhusu magonjwa ya zinaa, hapo zamani kulikuwa na vipindi maalumu kuhusu UKIMWI kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii lakini miaka ya hivi karibuni vipindi hivyo vimepotea, ni vema serikali ikarudisha tena program hii kama ilivokuwa kwenye ugonjwa wa COVID-19 ili tuweze kunusuru kizazi kijacho.

✓Serikali iandae makongamano na semina; serikali kupitia wizara ya afya na idara zake ni vema ikaandaa makongamano kwenye vijiji na mitaa ili elimu iweze kuwafikia wananchi kwa urahisi na ufanisi zaidi.

✓Mikutano kwaajili ya kutoa elimu hii mhimu kwa jamii, serikali pamoja na vyama vya siasa ni vema vikatumia mikutano ya hadhara kutoa elimu hii mhimu kwa jamii kwani inakuwa rahis kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja.

✓Taasisi za dini na asasi nyingine za kiraia pia ni vema zikaandaa vipindi maalumu kwaajili ya kutoa elimu kwa waumini wao juu ya namna bora ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa haya hatari kwa ustawi wa taifa letu la Leo na kesho.

✓Serikali itoe vipeperushi kuhusu magonjwa yote ya zinaa; ni vema serikali kupitia wizara ya afya ikatoka vipeperushi ambavyo vitawafikia wananchi moja kwa moja ili waweze kujisomea na kupata elimu hii mhimu Kwao.

✓Serikali iandae utaratibu kupitia mitandao ya simu uwekwe utaratibu wa kutuma ujumbe mtuli yaani SMS kwenye line za siku juu ya taarifa mbalimbali kuhusu magonjwa ya zinaa, kwani ni sehemu sahihi Sana kuweza kuwafikia wananchi wengi kwa uharaka zaidi.

✓ Serikali itie mkazo kampeni ya kupima magonjwa ya zinaa, na ikiwezekana magonjwa yote ya zinaa yapimwe bure kwani magonjwa haya yanaenda kuathiri mifumo ya uzazi ambao ndo mstakabali wa taifa la kesho, ifanyike hivo kama ilivo kwenye ugonjwa wa Virusi vya UKIMWI.

✓Pia ni vema wazazi wakapewa elimu kuhusu kuongea na watoto wao pindi wanapofika umri wa kubalehe na kuvuna ungo wajue namna ya kukabiliana na janga hili kubwa ambalo limeikumbwa nchi yetu kwa Kasi kubwa; kwa asilimia kubwa watu wengi huharibikiwa katika umri wa balehe hivo ni vema wazazi wakapewa elimu juu ya umhimu wa kuongea na watoto wao kuhusu janga hili Kwani kumekuwa na dhana potofu baina ya wazazi kwamba ulimwambia mtoto wako kuhusu masuala ya mahusiano unamharibu au unamchochea kufanya ngono jambo ambalo so kweli na mwisho wa siku watoto wanaharibikiwa kwa kukosa elimu na uelewa kuhusu janga hili.

✓Wahudumu wa afya watoe elimu na ushauri sahihi kwa waathirika namna ya kujilinda na kuwalinda wengine; hivi karibuni ni kama elimu hii imelega kwani waathirika wengi wa magonjwa ya zinaa wamekuwa wakiambukiza kwa makusudi kwa watu wengine ili asiteseke peke yake jambo ambalo linaathiri sana jamii na taifa letu kwa ujumla, hivo ni vema waathirika wakapewa elimu sahihi kuhusu kuwalinda wengine dhidi ya magonjwa haya.

✓Ili kupambana kwa ufanisi zaidi pia ni vema serikali ikapambana kwa nguvu kubwa dhidi ya biashara ya ngono ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo chanzo cha magonjwa ya zinaa; biashara ya ngono imekuwa ni janga kubwa sana kwenye nchi yetu kwani karibia katika miji yote kuna madada poa na madanguro ambako wanawake wanajiuza na hapo ndipo watu wengi huambukizana magonjwa kwa kujua na kutokujua. Tumeona baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam serikali ikichukua hatua kali dhidi ya watu wanafanya biashara ya ngono hivo ni vema ikawa ni kampeni ya nchi nzima ili kukomesha biashara hii haramu ambayo ni kitovu kikubwa cha tatizo hili.

Hitimisho; Elimu, ujuzi, na maarifa ndo msingi wa kila kitu katika jamii. Jamii ya watanzania imekosa elimu sahihi ya chanzo na madhara ya magonjwa ya zinaa hivo endapo elimu itatolewa kwa usahihi ni wazi kwamba tutapunguza kwa kiasi kikubwa janga hili.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom