SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

Stories of Change - 2023 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) Ni Idara ambayo inamajukumu ya kukusanya, kuchunguza na kuchambua Taarifa na shughuli zote zinazohusiana na Usalama wa Taifa. Ikiwa ni pamoja na kubaini matishio yote dhidi ya Tanzania lakini pia kushauri wizara zote juu maswala ya ulinzi na Usalama, Hivyo Tunaweza kusema idara hii ni idara ya muhimu na ya msingi katika uhai wa nchi yetu.

Katika kutekeleza majukumu yake idara inatumia mifumo na njia mbalimbali, Tufahamu yakuwa tupo katika dunia ya mabadiliko makubwa, Hivyo ni muhimu kwa idara yetu ya usalama wa taifa kuwa na mfumo wa kidigitali yaani tovuti ambayo raia wanaweza ingia na kuona taarifa mbalimbali lakini pia kuwezesha raia kutoa taarifa mbalimbali zitakazo saidia idara katika ufanyaji kazi.

Faida zitakazo tokana na uwepo wa tovuti hii sii tu wananchi kupata taarifa kutoka kwa idara bali pia idara kupokea taarifa kutoka kwa wananchi. Tukumbuke kuwa usalama wa Taifa unaanza na mwananchi, Hivyo ni muhimu kwa idara kuwa na mfumo utakao unganisha na kukuza mahusiano ya moja kwa moja na wananchi kwa kufanya hivi tutakuwa tumewavuta karibu wananchi na hivyo kuwa na mfumo shirikishi kati ya serikali na wananchi

MUUNDO WA TOVUTI

Napendekeza mfumo wa tovuti hii uwe na sehemu zifuatazo:-

SEHEMU YA HISTORIA YA IDARA

Katika sehemu hii idara iweke historia yake toka kuanzishwa kwake lakini pia viongozi waliowahi kuhudumu katika nafasi za ukurugenzi wa idara na historia zao, Lakini pia maono ya idara pamoja Na dira yake yaelezwe Kwa ufupi.

SEHEMU YA TAARIFA KUTOKA IDARA.

Sehemu hii iwe ni sehemu ambayo mwananchi akiingia ataona taarifa mbalimbali kama tahadhari za nchi zenye machafuko na nchi ambazo zina matishio ya ugaidi taarifa hizi idara itapokea kutoka kwa mabalozi wa Tanzania walio katika nchi mbalimbali na mara moja idara itaweka taarifa hizo katika tovuti yake hii itasaidia Wafanyabiashara, Watalii pamoja na Wanafunzi katika kupanga ratiba zao.

SEHEMU YA TAKWIMU.

Sehemu hii iwe na takwimu mbalimbali za Tanzania lakini pia takwimu za nchi nyingine za kijiografia, Kisiasa, Kiuchumi, biashara zinazofanywa na nchi nyingine. Mfano Mtanzania akitaka kujua ni maeneo gani katika nchi ya Rwanda biashara ya kuuza vitunguu ni kubwa moja kwa moja anaweza pata taarifa hizo kwenye tovuti ya usalama wa taifa taarifa za kweli na zenye uhakika.

SEHEMU YA NUKUU, VIPEPERUSHI NA MAKALA.

Hapa kuwekwe nukuu mbalimbali za viongozi wa nchi pamoja na nukuu za wakurugenzi wa idara ambazo zinahusiana na maswala ya ulinzi na usalama lakini pia vipeperushi na Makala ambazo zitakuwa zinaelezea umuhimu wa wananchi kushiriki na kutoa michango itayosaidia ukuaji mzuri wa nchi yetu, Makala za uelimishaji juu ya hatari za Rushwa, Ufisadi na ugaidi.

SEHEMU YA WANACHI KUTOA TAARIFA

Hii ni sehemu ya muhimu kwani hapa idara inaweza kukusanya taarifa mbalimbali za kiusalama kupitia wananchi sehemu itaruhusu wananchi kutoa taarifa ambapo mwanachi akiingia mfumo utamlinda na Hivyo kutoa taarifa zinazohusu ugaidi lakini pia kutoa taarifa juu ya viashiria vyovyote ambavyo ni hatari kwa taifa Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Kidini.

Tukumbuke kuwa idara ina jukumu nzito la kuilinda Tanzania dhidi ya matishio ya aina yeyeto Hivyo basi suala la kuwahusisha wananchi juu ya ulinzi na usalama kwa nchi yao si suala la kupuuzwa.

FAIDA ZA MFUMO KWA UJUMLA

  • Kutoa nafasi ya wananchi kushiriki katika ulinzi na usalama wa nchi yao Hivyo kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi.
  • Wananchi kujua historia ya nchi yao lakini pia kupata nafasi ya kujifunza maswala mbalailmbali na kwa kufanya hivi idara itakuwa inakuza na kufundisha uzalendo kwa wananchi hali hii itasaidia kuondoa Ukabila, Udini na Ukanda kwani tutategema idara kupitia tovuti yake kuweza kukemea na kuelimisha jamii. Hii itasaidia sio tu mahusiano ya wananchi na serikali lakini pia itaudumisha uhusiano huo.
  • Idara kuwa na wingi wa taarifa kutoka kila kona ya Tanzania na Hivyo kuifanya idara kuwa na utajiri wa taarifa ambazo idara itazitumia katika kutekeleza majukumu yake.


CHANGAMOTO ZA MFUMO

  • Ufikshwaji wa Taarifa za uongo, Watu wenye nia ovu wanaweza tumia tovuti kufikisha taarifa za uongo kwa idara jambo ambalo litaleta usumbufu kwa idara.
  • Kudukuliwa kwa mfumo, Hii ni dunia ya utandawazi watu wenye nia ovu wanaweza dukua mfumo na kupata taarifa ambazo wananchi wamezitoa kwa idara.
NJIA ZA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO HIZO

Njia nzuri ya kupambana na changamoto hizo kwanza ni kuundwa kwa tovuti yenye ulinzi na usalama wa hali ya juu ambao utakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kuzuia shambulio lolote la kujaribu kudukua mfumo lakini pia pale ambapo mwananchi anataka kutoa taarifa mfumo utamtaka ajaze taarifa zake binafsi na aruhusu mfumo kuweza kufikia taarifa zake za chombo anachotumia kuwasiliana na idara. Hii itasaidia wananchi kuogopa kutoa taarifa za uongo hivyo kuondoa usumbufu kwa idara,

Pia kuundwe kwa sheria ambayo endapo itabainika mwananchi ametoa taarifa za uongo kwa nia ovu ya kusumbua serikali hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

HITIMISHO

Tunatambua idara inafanya kazi zake kwa usiri mkubwa, Hivyo taarifa ambazo idara itakuwa inatoa ni taarifa ambazo hazina madhara dhidi ya usalama wa Tanzania. Pia nashauri idrara kupitia upya mifumo yao ya kuajiri na kuboresha idara ili iakisi dunia ya sasa.
 
Upvote 15
Mbona mm sioni hicho kialama
Kipo katikati ya mwisho wa uzi na comment ya kwanza kipo hivi ^ na pameandikwa 'vote' bonyeza hapo utakuwa umepiga kura
Asante.
 
Kwa Tanzania usalama wa Taifa wako maeneo mengi tu ikiwemo polisi

Tovuti ya polisi ina sehemu ya kuripoti

Wewe ripoti tu kama issue ya usalama wa taifa au ya JWTZ nk taarifa zitawafikia wahusika

Toa taarifa Tovuti ya polisi
 
Ni kweli kuwa usalama wa taifa wapo kila mahali lakini hilo halizuii wao kuwa na tovuti kumbuka tovuti haitakuwa kwa ajili ya kupokea taarifa tu bali pia kutoa taarifa kwa wananchi ambao ndio wenye nchi taarifa kama bajeti ya TISS, utaratibu wa kuajiri , dira na malengo yao ni muhimu kwa wananchi kujua hayo lakini pia tovuti inakuwa ni njia ya idara kutoa elimu kwa wananchi, kutoa machapisho na makala mbalimbali ambazo zitaongeza elimu kuhusu usalama wa taifa kwa raia.
Hivyo basi tovuti haiwi kwa lengo moja tu la kupokea taarifa.
Kusema kuwa wapo kila mahali sio kigezo cha wao kutokuwa na tovuti mbona JWTZ wapo ofisi za wilaya na mikoa , wapo kwenye wizara mbalimbali, wapo ikulu lakini bado wana tovuti?
 
Na walio mbali na huduma za police na wameona taarifa uoni wananyimwa haki.
Kwani email ya tiss ni ipi au ni Siri sana watu hawaruhusiwi kutuma taarifa za kiintelensia
 
Na walio mbali na huduma za police na wameona taarifa uoni wananyimwa haki.
Kwani email ya tiss ni ipi au ni Siri sana watu hawaruhusiwi kutuma taarifa za kiintelensia
Umesema kweli kabisa, Hapo ndio utaona umuhimu wa TISS kuwa na source yao ya taarifa ya kwao tofauti na polisi na taasisi nyingine.
Unaweza kuwa una taarifa muhimu lakini huna access ya kufikia polisi.
 
Ni kweli kuwa usalama wa taifa wapo kila mahali lakini hilo halizuii wao kuwa na tovuti kumbuka tovuti haitakuwa kwa ajili ya kupokea taarifa tu bali pia kutoa taarifa kwa wananchi ambao ndio wenye nchi taarifa kama bajeti ya TISS, utaratibu wa kuajiri , dira na malengo yao ni muhimu kwa wananchi kujua hayo lakini pia tovuti inakuwa ni njia ya idara kutoa elimu kwa wananchi, kutoa machapisho na makala mbalimbali ambazo zitaongeza elimu kuhusu usalama wa taifa kwa raia.
Hivyo basi tovuti haiwi kwa lengo moja tu la kupokea taarifa.
Kusema kuwa wapo kila mahali sio kigezo cha wao kutokuwa na tovuti mbona JWTZ wapo ofisi za wilaya na mikoa , wapo kwenye wizara mbalimbali, wapo ikulu lakini bado wana tovuti?
Kaka ,unabishana na mambumbumbu na kwa bahati iliyopo humu hatufahamiani ndio maana unakuta kajamaa ni kajinga fulani na hakajui lolote ila kwasababu hukaoni kanavyofanana ,kana uwezo gani juu ya kinachosisitizwa ndio maana vinatema pumba tu.Haiwezekani katika nchi zilizoendelea wao wawe na tovuti lakini sisi tusema eti ni Siri? Pumbavu ivi tovuti inazuia usiri gan? Au Wenda hawajui maana ya tovuti tuwasaidie .Inchi hii inawatu wa hovyo wanaoadmire vyombo vya ulinzi kipumbavu hatakama vinafanya uchafu .Pumbavu
 
Kaka ,unabishana na mambumbumbu na kwa bahati iliyopo humu hatufahamiani ndio maana unakuta kajamaa ni kajinga fulani na hakajui lolote ila kwasababu hukaoni kanavyofanana ,kana uwezo gani juu ya kinachosisitizwa ndio maana vinatema pumba tu.Haiwezekani katika nchi zilizoendelea wao wawe na tovuti lakini sisi tusema eti ni Siri? Pumbavu ivi tovuti inazuia usiri gan? Au Wenda hawajui maana ya tovuti tuwasaidie .Inchi hii inawatu wa hovyo wanaoadmire vyombo vya ulinzi kipumbavu hatakama vinafanya uchafu .Pumbavu
Wanashindwa kutofautisha kati ya mambo gani ni ya siri kiusalama na mambo gani sio siri.
 
Tiss inatakiwa wawe na lini Yao isiyotegemea taasisi zingine kupata information
 
Wewe nawe tunakuwa kama hatukuelewi kidogo,xx sijui kwamba na ww ni TISS ndio maana ukawa mkali ilivyotolewa kasoro ama vp.

Kimsingi Tiss ni taasisi za umma kama zilvyo taasisi nyengine ndani ya nchi na ndio maana imetungiwa hadi sheria na juzi tu ilikuwa inafanyiwa marekebisho.

Kwa iyo kama taasisi inatakiwa ijuulikane in formal address,kuanzia ofisi,uongozi,anuani, mawasilisno nk.wala kujulikana huku hakutafanya taarifa za tiss zivuje.

Kisingizio cha usalama wa udukuzi hakina ukweli wa aina yyt.Mbona mifumo mengine ipo wazi na haidukuliwi ikiwemo mawasiliano ya raisi ikulu ambayo ni nyeti kuliko hata iyo tiss.

Hawa jamaa hutumia kigezo cha usiri kuficha mambo yao yasijulikane kwa mengi ya hayo mambo ni maovu na yako kinyume na sheria,hiyo ndio sababu kubwa ya kujiwekea cover kubwa ya kujifanya wana siri katika mambo yao,ila hamna sababu nyengine yyt.
Basi fungua wewe tovuti, na hivyo vilivyofichwa vyote uviweke wazi. Sio lazima idara ndo ifanye. Fungua wewe!
 
Nani alikwambia haya mambo huwekwa waziwazi namna hiyo?! Kwani hakuna waliowahi kufikiria hivyo?! Mkiwa mna taarifa zenu pelekeni polisi... zitafika tu TISS, au huenda zimeshafika kabla nyie hamjajua.
TISS ya Tanzania? acha kuwapa credit ambazo hawana, ni wapuuzi tu hawana lolote, wajinga tu. Hawana maajabu. CIA, FBI, FSB n.k wana tovuti zipo wazi na wanatangaza ajira waziwazi, sio kila kitu eti ni siri , wanaficha upumbavu wao.
 
Huna unachojua wala hatufahamiani nyuma ya Keyboard... shortly! Hilo haliwezekani.

Njoo Makumbusho pale ulete huo mchango wako waziwazi kama unajiamini.
Mh!!!yaani kujua kuwa pale makumbusho pana ofisi ya TISS ndio unataka kutishia watu kweli,kwanza ww sio TISS ,maadili ya tiss hayaruhusu mtumishi wake kujitangaza kwa namna yyt kwa mtu kuwa yy ni usalama wa taifa.

Usitake tufahamiane kiundani hapa sio sehemu yake,kama una hoja za msingi toa,km huna hoja kaa pembeni watu wajadili.

Nakusisitiza wewe sio tiss,hata tiss wakiingia kwenye platform kama hizi huwa hawajitambulishi km unavotaka kutuonyesha wewe.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Usikute uko zako Kibondo unapalilia michikichi, ila mkwara kama vile uko Magogoni!
Tiss huwa hawana utaratibu wa kujitambulisha kwa aina hii,ni mwendawazimu mmoja ukute yuko malinyi anagina pomoni anaaza kutishatisha watu hapa.

Anafikiri himu kuna mtu wa kumtisha kwa style hiyo!!
 
Huenda ikawa wamejitanua kweli kama ulivyosema ila kujitanua kwao hakuzuii wao kuwa na tovuti
Nikuulize swali fikirishi tu kama unavyodai idara imejitanua kila sehemu tija yake ni nini? Mbona nchi inanuka Rushwa, ufisadi, wizi, utakatishaji fedha, uchochezi , n.k au hili nalo linahitaji mifano? Point yangu hapa ni hivi utaona pamoja na idara kujitanua bado inahitaji marekebisho makubwa na mimi kwa mtazamo wangu nimeona idara inabidi kuwa na tovuti yake ili kuchochea uwajibikaji kama nilivyoeleza, Kama na wewe una mchango ni jinsi gani idara ifanye kuchochea uwajibikaji uweke hapa lengo ni kujenga Tanzania imara.
Lakini kujificha kwenye kivuli cha idara ina watu kila mahali sijui idara hii ni ya siri na mambo mengine huku tuna ona hali ya maisha ya mtanzania moja mmoja ilivyo ngumu, Rushwa, udhalimu, n.k vinashamiri kila siku sio sawa kabisa. Idara ya usalama wa taifa ni kwa ajili ya taifa na taifa ni mimi na wewe na yule hivyo tuishauri idara kwa nia njema tu .
Idara haihusiki na mla rushwa wala mwizi wala fisadi,hivyo vyote vina wahusika wake
Idara ina kazi i yake maalum ambayo wakiona kitu hakiko sawa wao wanatoa taarifa kwa chombo husika kulingana na kitu chenyewe.
 
Idara haihusiki na mla rushwa wala mwizi wala fisadi,hivyo vyote vina wahusika wake
Idara ina kazi i yake maalum ambayo wakiona kitu hakiko sawa wao wanatoa taarifa kwa chombo husika kulingana na kitu chenyewe.
Sasa huo ufisadi na rushwa vipo xawa au??Naona u ataka kujichanganya kiufupi TISS wana mamlaka ya kufanya uchunguzi wa jambo lolote ovu ndani ya nchi hata uibe kuku basi wana haki ya kuchunguza tukio hilo na kuliwasilisha kwa chombo husika kuchukua hatua.
 
Idara haihusiki na mla rushwa wala mwizi wala fisadi,hivyo vyote vina wahusika wake
Idara ina kazi i yake maalum ambayo wakiona kitu hakiko sawa wao wanatoa taarifa kwa chombo husika kulingana na kitu chenyewe
Inaonekana una uelewa mdogo kuhusu usalama wa taifa
Ngoja nikupe elimu kidogo kwa taarifa yako TISS wapo kila taasisi ya serikali unayoijua wewe na huo mfumo wa kuweka mtu wa kitengo kwenye kila idara haujaanza leo kuna wakati watu wa usalama kutoka taasisi za serikali na binafsi pia walikuwa wanarudisha kufanya kazi kwenye ofisi zao rasmi yaani wanatoka site na huko site wanabaki informers tu. Idara ina mgawanyiko wa kazi kulingana na majukumu yake.
Hivyo basi hiyo PCCB inayohusika na Rushwa , Polisi wanaohusika na usalama wa raia na mali zao, BOT, TRA, Wizara zote namaanisha zote, jeshini kila jeshi unalolijua wewe hapa nchni, Vyuoni kote huko TISS wapo sasa wanafanya nini huko ikiwa hizo sio kazi zao.?
Kwa maarifa zaidi tafuta katiba ya TISS utajifunza mengi ningekuwekea hapa katiba yao ila naona haijakaa vizuri kuweka katiba yao hapa.
Lakini nikuulize swali unaelewa nini mtu anaposema usalama wa taifa??
 
Back
Top Bottom