SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

Stories of Change - 2023 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) Ni Idara ambayo inamajukumu ya kukusanya, kuchunguza na kuchambua Taarifa na shughuli zote zinazohusiana na Usalama wa Taifa. Ikiwa ni pamoja na kubaini matishio yote dhidi ya Tanzania lakini pia kushauri wizara zote juu maswala ya ulinzi na Usalama, Hivyo Tunaweza kusema idara hii ni idara ya muhimu na ya msingi katika uhai wa nchi yetu.

Katika kutekeleza majukumu yake idara inatumia mifumo na njia mbalimbali, Tufahamu yakuwa tupo katika dunia ya mabadiliko makubwa, Hivyo ni muhimu kwa idara yetu ya usalama wa taifa kuwa na mfumo wa kidigitali yaani tovuti ambayo raia wanaweza ingia na kuona taarifa mbalimbali lakini pia kuwezesha raia kutoa taarifa mbalimbali zitakazo saidia idara katika ufanyaji kazi.

Faida zitakazo tokana na uwepo wa tovuti hii sii tu wananchi kupata taarifa kutoka kwa idara bali pia idara kupokea taarifa kutoka kwa wananchi. Tukumbuke kuwa usalama wa Taifa unaanza na mwananchi, Hivyo ni muhimu kwa idara kuwa na mfumo utakao unganisha na kukuza mahusiano ya moja kwa moja na wananchi kwa kufanya hivi tutakuwa tumewavuta karibu wananchi na hivyo kuwa na mfumo shirikishi kati ya serikali na wananchi

MUUNDO WA TOVUTI

Napendekeza mfumo wa tovuti hii uwe na sehemu zifuatazo:-

SEHEMU YA HISTORIA YA IDARA

Katika sehemu hii idara iweke historia yake toka kuanzishwa kwake lakini pia viongozi waliowahi kuhudumu katika nafasi za ukurugenzi wa idara na historia zao, Lakini pia maono ya idara pamoja Na dira yake yaelezwe Kwa ufupi.

SEHEMU YA TAARIFA KUTOKA IDARA.

Sehemu hii iwe ni sehemu ambayo mwananchi akiingia ataona taarifa mbalimbali kama tahadhari za nchi zenye machafuko na nchi ambazo zina matishio ya ugaidi taarifa hizi idara itapokea kutoka kwa mabalozi wa Tanzania walio katika nchi mbalimbali na mara moja idara itaweka taarifa hizo katika tovuti yake hii itasaidia Wafanyabiashara, Watalii pamoja na Wanafunzi katika kupanga ratiba zao.

SEHEMU YA TAKWIMU.

Sehemu hii iwe na takwimu mbalimbali za Tanzania lakini pia takwimu za nchi nyingine za kijiografia, Kisiasa, Kiuchumi, biashara zinazofanywa na nchi nyingine. Mfano Mtanzania akitaka kujua ni maeneo gani katika nchi ya Rwanda biashara ya kuuza vitunguu ni kubwa moja kwa moja anaweza pata taarifa hizo kwenye tovuti ya usalama wa taifa taarifa za kweli na zenye uhakika.

SEHEMU YA NUKUU, VIPEPERUSHI NA MAKALA.

Hapa kuwekwe nukuu mbalimbali za viongozi wa nchi pamoja na nukuu za wakurugenzi wa idara ambazo zinahusiana na maswala ya ulinzi na usalama lakini pia vipeperushi na Makala ambazo zitakuwa zinaelezea umuhimu wa wananchi kushiriki na kutoa michango itayosaidia ukuaji mzuri wa nchi yetu, Makala za uelimishaji juu ya hatari za Rushwa, Ufisadi na ugaidi.

SEHEMU YA WANACHI KUTOA TAARIFA

Hii ni sehemu ya muhimu kwani hapa idara inaweza kukusanya taarifa mbalimbali za kiusalama kupitia wananchi sehemu itaruhusu wananchi kutoa taarifa ambapo mwanachi akiingia mfumo utamlinda na Hivyo kutoa taarifa zinazohusu ugaidi lakini pia kutoa taarifa juu ya viashiria vyovyote ambavyo ni hatari kwa taifa Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Kidini.

Tukumbuke kuwa idara ina jukumu nzito la kuilinda Tanzania dhidi ya matishio ya aina yeyeto Hivyo basi suala la kuwahusisha wananchi juu ya ulinzi na usalama kwa nchi yao si suala la kupuuzwa.

FAIDA ZA MFUMO KWA UJUMLA

  • Kutoa nafasi ya wananchi kushiriki katika ulinzi na usalama wa nchi yao Hivyo kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi.
  • Wananchi kujua historia ya nchi yao lakini pia kupata nafasi ya kujifunza maswala mbalailmbali na kwa kufanya hivi idara itakuwa inakuza na kufundisha uzalendo kwa wananchi hali hii itasaidia kuondoa Ukabila, Udini na Ukanda kwani tutategema idara kupitia tovuti yake kuweza kukemea na kuelimisha jamii. Hii itasaidia sio tu mahusiano ya wananchi na serikali lakini pia itaudumisha uhusiano huo.
  • Idara kuwa na wingi wa taarifa kutoka kila kona ya Tanzania na Hivyo kuifanya idara kuwa na utajiri wa taarifa ambazo idara itazitumia katika kutekeleza majukumu yake.


CHANGAMOTO ZA MFUMO

  • Ufikshwaji wa Taarifa za uongo, Watu wenye nia ovu wanaweza tumia tovuti kufikisha taarifa za uongo kwa idara jambo ambalo litaleta usumbufu kwa idara.
  • Kudukuliwa kwa mfumo, Hii ni dunia ya utandawazi watu wenye nia ovu wanaweza dukua mfumo na kupata taarifa ambazo wananchi wamezitoa kwa idara.
NJIA ZA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO HIZO

Njia nzuri ya kupambana na changamoto hizo kwanza ni kuundwa kwa tovuti yenye ulinzi na usalama wa hali ya juu ambao utakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kuzuia shambulio lolote la kujaribu kudukua mfumo lakini pia pale ambapo mwananchi anataka kutoa taarifa mfumo utamtaka ajaze taarifa zake binafsi na aruhusu mfumo kuweza kufikia taarifa zake za chombo anachotumia kuwasiliana na idara. Hii itasaidia wananchi kuogopa kutoa taarifa za uongo hivyo kuondoa usumbufu kwa idara,

Pia kuundwe kwa sheria ambayo endapo itabainika mwananchi ametoa taarifa za uongo kwa nia ovu ya kusumbua serikali hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

HITIMISHO

Tunatambua idara inafanya kazi zake kwa usiri mkubwa, Hivyo taarifa ambazo idara itakuwa inatoa ni taarifa ambazo hazina madhara dhidi ya usalama wa Tanzania. Pia nashauri idrara kupitia upya mifumo yao ya kuajiri na kuboresha idara ili iakisi dunia ya sasa.
 
Upvote 15
Sasa huo ufisadi na rushwa vipo xawa au??Naona u ataka kujichanganya kiufupi TISS wana mamlaka ya kufanya uchunguzi wa jambo lolote ovu ndani ya nchi hata uibe kuku basi wana haki ya kuchunguza tukio hilo na kuliwasilisha kwa chombo husika kuchukua hatua.
Sasa mbona umerudia nilichosema.
Kumbe ushanielewa ni ubishi tuu
 
Nani alikwambia haya mambo huwekwa waziwazi namna hiyo?! Kwani hakuna waliowahi kufikiria hivyo?! Mkiwa mna taarifa zenu pelekeni polisi... zitafika tu TISS, au huenda zimeshafika kabla nyie hamjajua.
Mkuu mleta mada kama nimemuelewa vizuri ni kwamba idara iwe na mfumo ambao hauhusiani na Siri yoyote ila ni taarifa tu za msingi mbona idara idara zingine za Siri ila zina tovuti za wazi kabisa kwa malengo aliyoyasema mleta mada
 
Haina umuhimu wowote hiyo.

Labda hujasikia kuwa kuna idara mpya ya uchunguzi wa wazi inaundwa? FBI ya Tanzania?

Hivi mbona "general knowledge" ya Watamnzania wengi iko finyu sana?

Kweli, Reforms na Rebuilding zinahitajika hata sana.


Naamini mleta mada haelewi hata maana ya TISS ni nini na uwepo wake una faida gani kwa nchi.
 
wale wanachojua ni kuchaguana wenye roho ngumu yaan ngumu namaanisha na vitabia vyao vya kucheka kinafki ila wana roho mbaya tena wengine ni toka utotoni sijuh wanajuanaje!
 
Bado Sana Kutumia Mifumo Ingawa Dunia Imebadilika Na Tunatakiwa Kuitumia Haraka Mifumo
 
Mkuu mleta mada kama nimemuelewa vizuri ni kwamba idara iwe na mfumo ambao hauhusiani na Siri yoyote ila ni taarifa tu za msingi mbona idara idara zingine za Siri ila zina tovuti za wazi kabisa kwa malengo aliyoyasema mleta mada
Asante mkuu, Umenielewa .
 
Haina umuhimu wowote hiyo.

Labda hujasikia kuwa kuna idara mpya ya uchunguzi wa wazi inaundwa? FBI ya Tanzania?

Hivi mbona "general knowledge" ya Watamnzania wengi iko finyu sana?

Kweli, Reforms na Rebuilding zinahitajika hata sana.


Naamini mleta mada haelewi hata maana ya TISS ni nini na uwepo wake una faida gani kwa nchi.
Haina umuhimu wowote hiyo.

Labda hujasikia kuwa kuna idara mpya ya uchunguzi wa wazi inaundwa? FBI ya Tanzania?

Hivi mbona "general knowledge" ya Watamnzania wengi iko finyu sana?

Kweli, Reforms na Rebuilding zinahitajika hata sana.


Naamini mleta mada haelewi hata maana ya TISS ni nini na uwepo wake una faida gani kwa nchi.
Kulingana na The Tanzania Intelligence and security Service act ya 1996 ambayo ilikuja kusainiwa na The late Benjamin Mkapa Tarehe 20 January 1997 inaeleza kuwa majukumu ya TISS ni pamoja na kukusanya, kuchunguza na kuchambua mienendo yote ya taarifa na matukio ambayo ni tishio kwa usalama wa Tanzania. Nadhani hii ndio core duty yao japo kuna mengine mengi tu.
Mashirika ya upelelezi yapo Kila nchi na utaona yanaendeshwa vizuri wana website mifumo ya ajira ni ya wazi n.k.
Ukija kwa upande wa Tanzania vitu ni tofauti sana na baadhi ya mambo yanayofanywa yanatia shaka juu ya uwazi na uwajibikaji wa TISS mimi huu ni ushauri wangu kwa TISS wakiona ni wa muhimu watafanyia kazi lakini lengo ni kuiweka Tanzania salama na imara na kujitahidi kuziba kila penye upungufu.
Mwisho niseme kuwa TISS wanafanya kazi kwa kodi za watanzania hivyo jamii kui question sio kosa.
Asante kwa mchango.
 
Ndio nasisi tuwekeze huko kwenye masuala ya ICT ili tuwe vizuri kwani wao wameweza je?
Lakini pia dunia ndio inapoenda hatuwezi kukwepa mabadiliko ya lazima kwa kujificha kwenye kichaka cha kuwa tuna uwezo mdogo. Ni muhimu kwa serikali kupitia upya mifumo yake na kuwekeza zaidi huko kwani kuna faida nyingi mbali na changamoto zake.
Nikupe mfano, Hivi Unajua kuwa kupitia tovuti ya CIA raia yeyeto wa Marekani aliye ndani au nje ya nchi anaweza kutoa taarifa kupitia tovuti na akapata msaada vipi kuhusu Tanzania? Watanzania wangapi wanakufa nchi za nje na hakuna anayejua, Watanzania wangapi wanapotelea nchi za watu bila misaada na serikali ipo kimya mambo kama haya ilikuwa ni kitendo cha mtanzania kuchukua simu yake na kutuma ujumbe kwa Tovuti ya TISS na mambo ya kawa sawa.
Kwa sababu kuna mazingira mtu anakutana nayo nchi za nje awezi kuwasiliana na balozi ya nchi yake inahitajika njia mbadala huo ni mfano tu wa faida za tovuti kama ni maswala ya usalama kuhusu udukuaji ni kulifanyia kazi na sio kuhitimisha hatuwezi, Tukisema sisi hatuwezi nani atakayeweza? Je hii nchi itakuwa haipigi hatua kwa kisingizio hatuwezi ??
Tupeane tovuti ya CIA
 
Back
Top Bottom