SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

Stories of Change - 2023 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) Ni Idara ambayo inamajukumu ya kukusanya, kuchunguza na kuchambua Taarifa na shughuli zote zinazohusiana na Usalama wa Taifa. Ikiwa ni pamoja na kubaini matishio yote dhidi ya Tanzania lakini pia kushauri wizara zote juu maswala ya ulinzi na Usalama, Hivyo Tunaweza kusema idara hii ni idara ya muhimu na ya msingi katika uhai wa nchi yetu.

Katika kutekeleza majukumu yake idara inatumia mifumo na njia mbalimbali, Tufahamu yakuwa tupo katika dunia ya mabadiliko makubwa, Hivyo ni muhimu kwa idara yetu ya usalama wa taifa kuwa na mfumo wa kidigitali yaani tovuti ambayo raia wanaweza ingia na kuona taarifa mbalimbali lakini pia kuwezesha raia kutoa taarifa mbalimbali zitakazo saidia idara katika ufanyaji kazi.

Faida zitakazo tokana na uwepo wa tovuti hii sii tu wananchi kupata taarifa kutoka kwa idara bali pia idara kupokea taarifa kutoka kwa wananchi. Tukumbuke kuwa usalama wa Taifa unaanza na mwananchi, Hivyo ni muhimu kwa idara kuwa na mfumo utakao unganisha na kukuza mahusiano ya moja kwa moja na wananchi kwa kufanya hivi tutakuwa tumewavuta karibu wananchi na hivyo kuwa na mfumo shirikishi kati ya serikali na wananchi

MUUNDO WA TOVUTI

Napendekeza mfumo wa tovuti hii uwe na sehemu zifuatazo:-

SEHEMU YA HISTORIA YA IDARA

Katika sehemu hii idara iweke historia yake toka kuanzishwa kwake lakini pia viongozi waliowahi kuhudumu katika nafasi za ukurugenzi wa idara na historia zao, Lakini pia maono ya idara pamoja Na dira yake yaelezwe Kwa ufupi.

SEHEMU YA TAARIFA KUTOKA IDARA.

Sehemu hii iwe ni sehemu ambayo mwananchi akiingia ataona taarifa mbalimbali kama tahadhari za nchi zenye machafuko na nchi ambazo zina matishio ya ugaidi taarifa hizi idara itapokea kutoka kwa mabalozi wa Tanzania walio katika nchi mbalimbali na mara moja idara itaweka taarifa hizo katika tovuti yake hii itasaidia Wafanyabiashara, Watalii pamoja na Wanafunzi katika kupanga ratiba zao.

SEHEMU YA TAKWIMU.

Sehemu hii iwe na takwimu mbalimbali za Tanzania lakini pia takwimu za nchi nyingine za kijiografia, Kisiasa, Kiuchumi, biashara zinazofanywa na nchi nyingine. Mfano Mtanzania akitaka kujua ni maeneo gani katika nchi ya Rwanda biashara ya kuuza vitunguu ni kubwa moja kwa moja anaweza pata taarifa hizo kwenye tovuti ya usalama wa taifa taarifa za kweli na zenye uhakika.

SEHEMU YA NUKUU, VIPEPERUSHI NA MAKALA.

Hapa kuwekwe nukuu mbalimbali za viongozi wa nchi pamoja na nukuu za wakurugenzi wa idara ambazo zinahusiana na maswala ya ulinzi na usalama lakini pia vipeperushi na Makala ambazo zitakuwa zinaelezea umuhimu wa wananchi kushiriki na kutoa michango itayosaidia ukuaji mzuri wa nchi yetu, Makala za uelimishaji juu ya hatari za Rushwa, Ufisadi na ugaidi.

SEHEMU YA WANACHI KUTOA TAARIFA

Hii ni sehemu ya muhimu kwani hapa idara inaweza kukusanya taarifa mbalimbali za kiusalama kupitia wananchi sehemu itaruhusu wananchi kutoa taarifa ambapo mwanachi akiingia mfumo utamlinda na Hivyo kutoa taarifa zinazohusu ugaidi lakini pia kutoa taarifa juu ya viashiria vyovyote ambavyo ni hatari kwa taifa Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Kidini.

Tukumbuke kuwa idara ina jukumu nzito la kuilinda Tanzania dhidi ya matishio ya aina yeyeto Hivyo basi suala la kuwahusisha wananchi juu ya ulinzi na usalama kwa nchi yao si suala la kupuuzwa.

FAIDA ZA MFUMO KWA UJUMLA

  • Kutoa nafasi ya wananchi kushiriki katika ulinzi na usalama wa nchi yao Hivyo kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi.
  • Wananchi kujua historia ya nchi yao lakini pia kupata nafasi ya kujifunza maswala mbalailmbali na kwa kufanya hivi idara itakuwa inakuza na kufundisha uzalendo kwa wananchi hali hii itasaidia kuondoa Ukabila, Udini na Ukanda kwani tutategema idara kupitia tovuti yake kuweza kukemea na kuelimisha jamii. Hii itasaidia sio tu mahusiano ya wananchi na serikali lakini pia itaudumisha uhusiano huo.
  • Idara kuwa na wingi wa taarifa kutoka kila kona ya Tanzania na Hivyo kuifanya idara kuwa na utajiri wa taarifa ambazo idara itazitumia katika kutekeleza majukumu yake.


CHANGAMOTO ZA MFUMO

  • Ufikshwaji wa Taarifa za uongo, Watu wenye nia ovu wanaweza tumia tovuti kufikisha taarifa za uongo kwa idara jambo ambalo litaleta usumbufu kwa idara.
  • Kudukuliwa kwa mfumo, Hii ni dunia ya utandawazi watu wenye nia ovu wanaweza dukua mfumo na kupata taarifa ambazo wananchi wamezitoa kwa idara.
NJIA ZA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO HIZO

Njia nzuri ya kupambana na changamoto hizo kwanza ni kuundwa kwa tovuti yenye ulinzi na usalama wa hali ya juu ambao utakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kuzuia shambulio lolote la kujaribu kudukua mfumo lakini pia pale ambapo mwananchi anataka kutoa taarifa mfumo utamtaka ajaze taarifa zake binafsi na aruhusu mfumo kuweza kufikia taarifa zake za chombo anachotumia kuwasiliana na idara. Hii itasaidia wananchi kuogopa kutoa taarifa za uongo hivyo kuondoa usumbufu kwa idara,

Pia kuundwe kwa sheria ambayo endapo itabainika mwananchi ametoa taarifa za uongo kwa nia ovu ya kusumbua serikali hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

HITIMISHO

Tunatambua idara inafanya kazi zake kwa usiri mkubwa, Hivyo taarifa ambazo idara itakuwa inatoa ni taarifa ambazo hazina madhara dhidi ya usalama wa Tanzania. Pia nashauri idrara kupitia upya mifumo yao ya kuajiri na kuboresha idara ili iakisi dunia ya sasa.
 
Upvote 15
Haina umuhimu wowote hiyo.

Labda hujasikia kuwa kuna idara mpya ya uchunguzi wa wazi inaundwa? FBI ya Tanzania?

Hivi mbona "general knowledge" ya Watamnzania wengi iko finyu sana?

Kweli, Reforms na Rebuilding zinahitajika hata sana.


Naamini mleta mada haelewi hata maana ya TISS ni nini na uwepo wake una faida gani kwa nchi.
Haelewi mleta mada au huelewi wewe????
 
aah aah sio wa TiSS wetu utoe taarifa ya kiongozi badala waifanyie kazi watakuja kukubananisha wakuulize we umetoa wapi taarifa mara unachafua viongozi watakupa kesi kibao mwisho wa siku utahitajika kuisaidia polisi ....

tupo local saana hii Nchi taaluma inaingiliwa na siasa , recruit ya usalama ni ya kindugu kulinda ndugu zao .. ujinga tu.


inatakiwa iwe na I'd fake kama jf then taarifa zozote wapokee za uongo na kweli... wakichunguza Kwa muda wao watajua hipi ya kuifanyia kazi ipo ya kizushi.
 
Ila tovuti itakuwa ipo kwa lengo la kukusanya zaidi taarifa, Mashirika ya upelelezi kama CIA na FBI n.k wanazo tovuti na wanatoa na kupokea taarifa tujifunze wao wanawezaje?
Asante.
Wale wanamiliki technolojia hii ya mtandao. Sisi hatumiliki ...kwa hiyo matumizi ya mtandao kufanya kazi zetu kama nchi kujilinda inatakiwa uchukuliwe kwa umakini mkubwa. Vinginevyo, tutaumbuka kama nchi au tukubali kuwa vikaragosi wa hao wanaomiliki teknolojia ya mitandao. By the Way, mitandao unayoshauri kutumia kwa idara hizi haitasaidia kuondoa "mules" wa mashirika ya nchi nyingine bali inaweza kuongeza na kurahisisha utumaji wa taarifa za hatari kwa nchi yetu kwa hao waliowatuma.

Kumbuka sipingi matumizi ya mitandao bali napinga matumizi ya mtandao kwa masuala nyeti kiholela!
 
Wale wanamiliki technolojia hii ya mtandao. Sisi hatumiliki ...kwa hiyo matumizi ya mtandao kufanya kazi zetu kama nchi kujilinda inatakiwa uchukuliwe kwa umakini mkubwa. Vinginevyo, tutaumbuka kama nchi au tukubali kuwa vikaragosi wa hao wanaomiliki teknolojia ya mitandao. By the Way, mitandao unayoshauri kutumia kwa idara hizi haitasaidia kuondoa "mules" wa mashirika ya nchi nyingine bali inaweza kuongeza na kurahisisha utumaji wa taarifa za hatari kwa nchi yetu kwa hao waliowatuma.

Kumbuka sipingi matumizi ya mitandao bali napinga matumizi ya mtandao kwa masuala nyeti kiholela!
Umesomeka vyema mkuu, Ila lengo kubwa la kuwa na tovuti ni iweze kutumika kama nyenzo ya kukusanya, kuchambua na kutoa taarifa na hili linawezekana kuna mdau alitoa mfano kuwa jeshi letu la ulinzi JWTZ lina tovuti lakini hakuna masuala nyeti yanayowekwa mule bali inatumika kueleza kazi za jeshi, kamandi zake na majukumu na historia pamoja na kutoa matangazo ya nafasi za kazi.
Sasa idara ya usalama inaweza pia kuwa na tovuti na kwa kuwa idara inahusika na kuchakata taarifa inaweza anza na kujipambanua kazi zake na majukumu yake na utoaji wa taarifa, Maswala nyeti yatabaki kuwa siri na kudhibitiwa.
Lakini pia kama suala ni changamoto za usalama wa taarifa linaweza kuwa encountered kwa kuimarisha usalama wa mtandaoni, kuweka sera na sheria imara pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa idara ya usalama.
Kuhusu'' moles'' sidhani kama moles wanaweza kuwa na athari ya moja kwa moja kwa sisi kuwa na tovuti.
 
Maswala nyeti yatabaki kuwa siri na kudhibitiwa.
Lakini pia kama suala ni changamoto za usalama wa taarifa linaweza kuwa encountered kwa kuimarisha usalama wa mtandaoni, kuweka sera na sheria imara pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa idara ya usalama.
Kuhusu'' moles'' sidhani kama moles wanaweza kuwa na athari ya moja kwa moja kwa sisi kuwa na tovuti.
Mkuu ili tuwe kwenye ukurasa mmoja, naomba kwa ufupi sana unifafanulie namna:
1. mtandao wa kuweka hizo taarifa ulivyotengenezwa, unavyochakata taarifa zinazowekwa, unavyotunza taarifa zilizochakatwa na ambazo hazijachakatwa.
2. aina za "moles", namna moles wanavyopatikana, wanavyofanya kazi, nakadhalika.

Natanguliza shukrani; Asante.
 
Mkuu ili tuwe kwenye ukurasa mmoja, naomba kwa ufupi sana unifafanulie namna:
1. mtandao wa kuweka hizo taarifa ulivyotengenezwa, unavyochakata taarifa zinazowekwa, unavyotunza taarifa zilizochakatwa na ambazo hazijachakatwa.
2. aina za "moles", namna moles wanavyopatikana, wanavyofanya kazi, nakadhalika.

Natanguliza shukrani; Asante.
Mkuu nadhani ushakutana na msemo unaosema '' Information is the oxygen of the modern age'' Lakini pia tunafahamu kwamba ''information is carried by people'' kwa muktadha huu ndio manaa mashirika ya kijasusi yana struggle kwa kila namna kupata information hapa ndio tunaona umuhimu wa informaton katika ujasusi.
Hivyo basi ni jukumu la idara kutunza na kudumisha vyanzo vya taarifa lakini pia kubuni vyanzo vipya vya upatikanaji wa taarifa.
Sasa nikija katika maswali yako kuhusu namna mtandao utavyotengenezwa hapa niseme mimi sina ujuzi na maswala ya utengenezaji ila niliweka hint katika post jinsi mtandao unavyotakiwa kuwa na jinsi utakavyofanya kazi.
Najua point yako katika hili swali ipo katika usalama wa taarifa ukizingatia bado tupo nyuma katika teknolojia lakini jambo hili nilishalitolea ufafanuzi kuwa ni muda sasa na sisi kuanza kuwekeza katika research based technology ili kuwa na msingi mzuri wa ku -encounter threat zozote za kimfumo.
Swala la pili ni kuhusu moles, Katika swala la moles na jinsi wanavyofanya kazi na wanayopatikana nitajaribu kulielezea hivi kwa kuanza na aina za moles;-
  1. Sleeper Mole: Huyu ni mole ambaye amejipenyeza ndani ya shirika au tasisi lakini anabaki bila kufanya kazi kwa muda mrefu hadi anapohitajika. Mfano ni kama vile mole ambaye anaweza kuwa ameajiriwa katika kampuni ya teknolojia lakini anasubiri maagizo kutoka kwa shirika lake la asili.
  2. Double Agent: Huyu ni mole ambaye anajifanya kufanya kazi kwa shirika moja wakati kwa kweli anafanya kazi kwa shirika jingine. Mfano ni kama vile mtu anayefanya kazi kwa serikali moja lakini anatoa taarifa kwa serikali nyingine.
  3. Walk-In: Huyu ni mtu ambaye kwa hiari yake mwenyewe anajitolea kuwa mole, mara nyingi akichochewa na itikadi, pesa, au shinikizo. Mfano ni kama mfanyakazi wa ubalozi anayejitolea kutoa siri za nchi yake kwa nchi nyingine kwa sababu ya imani zake za kisiasa.
  4. False Flag: Huyu ni mole ambaye ameajiriwa kwa udanganyifu, akiamini kwamba anafanya kazi kwa shirika moja wakati in fact anahudumia shirika jingine. Mfano ni kama vile mtu anayefanya kazi kwa shirika la kijasusi la nchi moja lakini in fact anatoa taarifa kwa shirika la kijasusi la nchi nyingine.
  5. Agent Provocateur: Huyu ni mole ambaye hujipenyeza ndani ya kundi ili kuchochea wanachama wake kufanya vitendo haramu, hivyo basi kudhalilisha kundi hilo au kufichua wanachama wake. Mfano ni kama vile mole anayejipenyeza ndani ya kundi la wanaharakati ili kuwachochea kufanya maandamano yasiyo halali.
Tuje jinsi mole wanavyopatikana
  1. Employment(Uajiri): Shirika la kijasusi linaweza kumlenga mtu mwenye nafasi muhimu ndani ya shirika lingine. Uajiri unaweza kufanywa kwa kutumia mbinu kama vile:
    • Kuvutia kwa fedha: Kutoa malipo ya kifedha kwa kubadilishana na taarifa.
    • Shinikizo: Kutumia vitisho au shinikizo la kisheria au la kibinafsi.
    • Itikadi: Kuwashawishi watu kwa kutumia itikadi za kisiasa au kijamii.
    • Udanganyifu: Kuwafanya watu waamini kuwa wanasaidia shirika lao kumbe wanatoa taarifa kwa adui.
  2. Kujitolea: Watu wengine wanaweza kujitolea wenyewe kuwa moles kwa sababu mbalimbali kama vile kutoridhika na kazi yao ya sasa, itikadi, au tamaa ya malipo.

Jinsi Moles Wanavyofanya Kazi​

  1. Kujipenyeza: Mara baada ya kuajiriwa, mole hujipenyeza ndani ya shirika lengwa. Hii inaweza kuchukua muda mrefu na inahitaji uvumilivu na tahadhari kubwa ili kuepuka kugundulika.
  2. Kukusanya Taarifa: Mole hukusanya taarifa muhimu kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile:
    • Kufikia nyaraka za siri: Kupata nyaraka muhimu na kuzitoa kwa shirika lake la asili.
    • Kufuatilia mazungumzo: Kusikiliza na kurekodi mazungumzo muhimu.
    • Kudukua mifumo ya kompyuta: Kupata taarifa kupitia mifumo ya kompyuta ya shirika lengwa.
  3. Kuripoti: Mole huripoti taarifa alizokusanya kwa shirika lake la asili kwa kutumia njia salama kama vile:
    • Mikutano ya siri: Kukutana na maafisa wa shirika lake la asili katika maeneo ya siri.
    • Mawasiliano ya siri: Kutumia njia za mawasiliano za siri kama vile ujumbe uliosimbwa au vifaa vya kielektroniki.
  4. Kuepuka Kugundulika: Mole lazima awe makini sana ili kuepuka kugundulika. Hii inajumuisha:
    • Kuficha nyendo zake: Kuepuka vitendo vinavyoweza kumfichua.
    • Kudanganya: Kutumia udanganyifu ili kuficha shughuli zake za kijasusi.
Mkuu nadhani imeeleweka japo ABC
 
Back
Top Bottom