PreGE2025 Umuhimu wa kila mtanzania kushiriki kupiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hao wananchi wana huo uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka? Tukijificha kwenye kivuli cha amani wakati hakuna haki tunakua wanafiki. Mfano Mzuri ni Mpina alichoongea na maelekezo aliyotoa Rais mbele ya hadhara. Je, Rais ndo anapaswa kuwachagulia wananchi mbunge au wananchi ndo wanatakiwa kumchagua mbunge wao. Uchaguzi wa Kenya wa 2022 Mstaafu Kikwete alikua ni mmoja kati ya waangalizi wa nje, alisifia transparence ya ule uchaguzi akisisitiza swala la mawakala kuruhusiwa kuingia na smartphones kwenye vyumba vya kuhesabia kura. Kwa nini hapa Tanzania wanakatazwa? Kwa nini wagombea wa Upinzani walienguliwa bila sababu za msingi? Mwenyekiti wa chama cha siasa anapokua na mamlaka ya kuteua wajumbe wa Tume ya uchaguzi akiwamo mwenyekiti mwenyewe wa Tume unategemea nini? Kanuni za maadili ya uchaguzi zina kila kiashiria cha kuiba kura, huo uchaguzi huru na haki mnaotaka kuwaaminisha watanzania ni upi?
 
Kupiga kura ni haki ya kikatiba inayomwezesha kila Mtanzania kushiriki katika maamuzi ya nchi kwa njia ya amani, kupitia kura wananchi huamua ni nani awaongoze katika nafasi za kisiasa kama Rais, Wabunge na Madiwani na hii ni njia halali ya kushiriki katika ujenzi wa taifa na kuhakikisha kuwa sauti ya wananchi inasikika.

Ni wajibu wa kiraia kwa kila mwenye sifa ya kupiga kura kuhakikisha anatumia haki hiyo, kutojitokeza kupiga kura ni kuruhusu watu wengine kufanya maamuzi kwa niaba yako, jambo linaloweza kusababisha kuchaguliwa kwa viongozi wasiowatumikia wananchi ipasavyo.

Wananchi wanapojitokeza kwa wingi kupiga kura, wana nafasi ya kuchagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuleta maendeleo, Kupitia kura matatizo ya huduma duni za jamii kama elimu, afya na maji yanaweza kushughulikiwa kwa kuchagua viongozi wanaojali maendeleo ya wananchi.

Aidha, kupiga kura huimarisha misingi ya demokrasia na utawala bora, inawafanya viongozi walioko madarakani kuwajibika kwa wananchi wakijua kuwa wanaweza kuondolewa kwa kura iwapo hawatatimiza ahadi zao.

Kila Mtanzania anapaswa kutambua kuwa kura yake ni sauti yake na anatakiwa kuwajibika ifikapo Oktoba Ili taifa lipige hatua, kila mwananchi mwenye sifa anapaswa kujitokeza kwa hiari na kwa wingi kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura kwa amani na utulivu.

#OktobaNawajibika
#OktobaTunatiki
#KuraYanguSautiYangu
#NoReformsNoElection
 
Kushiriki kupiga kukura ni muhimu sana ila kushiriki kupiga kura halafu wanawekwa watu ambao hawajachaguliwa ni kunyima haki ya kuchagua na kuchaguliwa

Kumbuka wakati wa uchaguzi kuna watu huwa wanaenda maporini rejea uthibitisho wa mkuu wa wilaya aliye tumbuliwa

Kama hakuna marekebisho ya mfumo wa kupiga kura, (uchaguzi), ni bora kubaki nyumbani mimi nitakuwa nakula keki yangu kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa 1 jioni

No electroral reforms 2025, no elections 2025

NER-2025, NE-2025
NERNE-2025
 
Kupiga kura ni haki ya kikatiba inayomwezesha kila Mtanzania kushiriki katika maamuzi ya nchi kwa njia ya amani, kupitia kura wananchi huamua ni nani awaongoze katika nafasi za kisiasa kama Rais, Wabunge na Madiwani na hii ni njia halali ya kushiriki katika ujenzi wa taifa na kuhakikisha kuwa sauti ya wananchi inasikika.

Ni wajibu wa kiraia kwa kila mwenye sifa ya kupiga kura kuhakikisha anatumia haki hiyo, kutojitokeza kupiga kura ni kuruhusu watu wengine kufanya maamuzi kwa niaba yako, jambo linaloweza kusababisha kuchaguliwa kwa viongozi wasiowatumikia wananchi ipasavyo.

Wananchi wanapojitokeza kwa wingi kupiga kura, wana nafasi ya kuchagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuleta maendeleo, Kupitia kura matatizo ya huduma duni za jamii kama elimu, afya na maji yanaweza kushughulikiwa kwa kuchagua viongozi wanaojali maendeleo ya wananchi.

Aidha, kupiga kura huimarisha misingi ya demokrasia na utawala bora, inawafanya viongozi walioko madarakani kuwajibika kwa wananchi wakijua kuwa wanaweza kuondolewa kwa kura iwapo hawatatimiza ahadi zao.

Kila Mtanzania anapaswa kutambua kuwa kura yake ni sauti yake na anatakiwa kuwajibika ifikapo Oktoba Ili taifa lipige hatua, kila mwananchi mwenye sifa anapaswa kujitokeza kwa hiari na kwa wingi kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura kwa amani na utulivu.

#OktobaNawajibika
#OktobaTunatiki
#KuraYanguSautiYangu
Kama kupiga kura ni haki ya kikatiba! Kwa nini mnafanya udanganyifu kwa kuiba hizo kura, na pia kuwatangaza wagombea wenu walioshindwa?

Kama kupiga kura kunaimarisha demokrasia! Kwa nini hamtaki mabadiliko ya msingi ya uwepo wa tume huru ya uchaguzi?

Kwa nini Rais, na ambaye ni mgombea na mwanachama wa chama tawala aruhusiwe kuteua wasimamizi na watangaza matokeo wa huo uchaguzi?
 
Mi kwa upande wangu naona shida sio kupiga kura shida ni heshima na dhamani ya kura yangu

Nakaa kwa zaidi ya miez3 nikifuatiria mchakato mzma wa kampeni zen sku ya mm kufanya maamuzi kura yangu inaibiwa, inaharibiwa na kibaya zaidi kura yangu inashindwa kufanya maamuzi sabu ya kiongozi mmoja kaamua ushindi wa lazima na katumia jeshi na polisi km kinga

Heshima ya kura ni kitu muhimu kwa upande wangu no reform no election haina maana cha maana kwangu ni heshima na dhamani ya kura yangu
 
Kama kupiga kura ni haki ya kikatiba! Kwa nini mnafanya udanganyifu kwa kuiba hizo kura, na pia kuwatangaza wagombea wenu walioshindwa?

Kama kupiga kura kunaimarisha demokrasia! Kwa nini hamtaki mabadiliko ya msingi ya uwepo wa tume huru ya uchaguzi?

Kwa nini Rais, na ambaye ni mgombea na mwanachama wa chama tawala aruhusiwe kuteua wasimamizi na watangaza matokeo wa huo uchaguzi?
Hawako Tayari kujibu maswali kama haya. Washawaona Watanzania ni mapoyoyo sana.
Kwanza Samia alishasema kua hata mkiwachagua wale wa upande mwingine, Serikali itaundwa na CCM. Wao kama wanataka kupiga kura wakapige, wasilazimishe watu. Watanzania wameelimika, wametambua kua kwa mazingira ya sasa kura zao hazina thamani yoyote, bora wakae nazo ndani.
 
Kupiga kura ni haki ya kikatiba inayomwezesha kila Mtanzania kushiriki katika maamuzi ya nchi kwa njia ya amani, kupitia kura wananchi huamua ni nani awaongoze katika nafasi za kisiasa kama Rais, Wabunge na Madiwani na hii ni njia halali ya kushiriki katika ujenzi wa taifa na kuhakikisha kuwa sauti ya wananchi inasikika.

Ni wajibu wa kiraia kwa kila mwenye sifa ya kupiga kura kuhakikisha anatumia haki hiyo, kutojitokeza kupiga kura ni kuruhusu watu wengine kufanya maamuzi kwa niaba yako, jambo linaloweza kusababisha kuchaguliwa kwa viongozi wasiowatumikia wananchi ipasavyo.

Wananchi wanapojitokeza kwa wingi kupiga kura, wana nafasi ya kuchagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuleta maendeleo, Kupitia kura matatizo ya huduma duni za jamii kama elimu, afya na maji yanaweza kushughulikiwa kwa kuchagua viongozi wanaojali maendeleo ya wananchi.

Aidha, kupiga kura huimarisha misingi ya demokrasia na utawala bora, inawafanya viongozi walioko madarakani kuwajibika kwa wananchi wakijua kuwa wanaweza kuondolewa kwa kura iwapo hawatatimiza ahadi zao.

Kila Mtanzania anapaswa kutambua kuwa kura yake ni sauti yake na anatakiwa kuwajibika ifikapo Oktoba Ili taifa lipige hatua, kila mwananchi mwenye sifa anapaswa kujitokeza kwa hiari na kwa wingi kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura kwa amani na utulivu.

#OktobaNawajibika
#OktobaTunatiki
#KuraYanguSautiYangu
NRNE....

KUPIGA KURA NI KUPOTEZA MUDA

ova
 
Back
Top Bottom