PreGE2025 Umuhimu wa kila mtanzania kushiriki kupiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
No reform, No election
 
We maku nini?...Acha ungese
 
Ukipiga wewe inatosha no reforms no elections
 
Ni muhimu ndio lakini sio LAZIMA hasa ninapoona uwezekano wa kura yangu kuibiwa. Katiba hiyo unayoitaja ilitungwa na kikundi cha watu wachache wanaonufaika na mema yote ya nchi.
Ni wakati sasa wa kurejea upya utungaji wa Katiba Mpya itakayojumuisha maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Warioba na pengine iboreshwe zaidi ndipo tushiriki uchaguzi..... Vinginevyo #NoreformsNoelection iko hai kwenye mioyo ya watu.
 
Umezuka toka sayari gani ?
Hujui ccm hawajali kura zenu Bali huteu wanaowataka?
 
Kwa Tanzania upige kura usipige ni sawa tu ndugu
 
Nitafuatilia kwa ukaribu sana meamba
Ukiona mjumbe wa CCM anaandikisha idadi ya wapigakura mtaani, ujue ni maandalizi ya kura yako kuhesabika imemchagua mtu wanayemtaka ashinde. Kwa jinsi watanzania tusivyokuwa na tabia ya kufuatilia mambo, wanakupigisha kura hata kama haupo..... Hiyo ndio modus operandi ya CCM.
 
Mimi nimejiandikisha vizuri na kitambulisho changu cha kura kiko vizuri na umri wangu ni zaidi ya miaka 60,lakini sitopiga kura ng'o, ni kupotezeana muda, kura haina thamani. Wacha wajipitishe kwa kishindo tuone kama nchi itakalika!
 
Hakuna asiejuabumuhimu wa kupiga kura ila unapiga kura katika mazingira yapi, hayahaya, ccm wajiapishe hakuna namna
 
Paskali, mnatufanya Watanzania wote maxuxu. Kura isiyokuwa na thamani ni kupoteza nguvu na muda wa kuzalisha; ili kura ya Mtanzania iwe na thamani inamgharimu kutumia nguvu kubwa ya kupambana na Polisi na Wasimamizi wa Uchaguzi, yote hayo ya nini?
Yaani kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya Jimbo la mjini kama Dar inachukua siku mbili na zaidi! Hapo kuna uchaguzi kweli?

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…