Umuhimu wa kujifunza saikolojia

Umuhimu wa kujifunza saikolojia

Kabla hatujamaliza mwaka MziziMkavu karibu utupe somo maana Mashaxizo hukumjibu hapo juu!!!

Hebu Jaribu hii hapa chini:

Utajitambuje Kama Unaakili



KWAmujibu wa Mwanasaikolojia mwenzangu Howard Gardiner aliandika kuwa binadamu wanatofautiana kiakili kila binadamu anauwezo wake katika kufikiri.

Sasa ndugu mpenzi wa blogu hii, utajitambuaje kuwa wewe unaakili kiasi gani? Wewe na wenzako munatofautiaje katika kufikiri? Kulingana na akili uliyonayo unatakiwa uwe nani na uishije katika dunia hii?

Jibu la maswali hapo juu ni kwamba ili kujitambua akili yako unatakiwa kuwafanya mahesabu ya akili yako. Na kwa mujibu wa Gardiner unatakiwa kufuata fomula hii hapa chini:

Chukua Akili ya Umri wako gawanya kwa Mtiririko wa Umri wako na Zidisha kwa Miamoja = Akili yako.

Akili= Mental Age (MA) x 100
Chronological Age (CA)

Kama mental age ni kubwa kuliko chronogical age jua kuwa akili yako iko juu zaidi ya kawaida, kama mental age iko sawa na chronological age jua kuwa akili yako ipo katika hali ya kawada na kama mental age iko chini ya chronological age jua kuwa akili yako iko chini ya kawaida.

Sasa jitambue wewe uko katika hali gani jifanyie uchunguzi ili kujitambua zaidi fanya mahesabu ya kujua akili yako ili uweze kujikonturo na maisha, jiwekee malengo kwa kufuatana na uwezo wako wa kufikiri. Ni hayo tu mpenzi

Tumia njia hii hapa chini kopi link au bonyeza
http://images.pearsonclinical.com/images/ageCalculator/ageCalculator.htm

Chronological Age Calculator
[TABLE="width: 283"]
[TR]
[TD]
Name:
Age:

[TD="colspan: 2"]
Birthday Date://
Test Date://
[/TD]

[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
How to Calculate Your Mental Age?



photos.demandstudios.com%2F227%2F239%2Ffotolia_1886639_XS.jpg


Student placement is often determined by standardized testing that calculates "mental age." Photo Credit student image by Vasiliy Koval from Fotolia.comYour chronological age, that is, the number of years since the day of your birth, does not always align with what psychologists

term your "mental age." Determining the difference between the two is useful in designing lesson plans for the especially intelligent and mentally disabled, though the methods by which

psychologists calculate mental age are limited. Standardized tests like the Stanford-Binet intelligence quotient have proven reliable, while doctor assessments in cases of severe

disability are little more than educated guesses. Still, doctor assessments demonstrated reliability equal to that of testing in a 1986 study published in the "Journal of Pediatric Psychology."


Step 1


Take an IQ test administered by a qualified, professional proctor. Online tests can be fun, but they lack expert analysis and come with warnings that they are for entertainment purposes only.
Step 2

Write down your score in the following formula: IQ=MA/CA * 100, where "MA" is your mental age and "CA" is your chronological age. For example, if your chronological age is 10 and your IQ score is 120, the formula would read, 120=x/10 * 100, where "x" is your mental age.


Step 3

Divide both sides of the equation by 100. This leaves you with 1.2=x/10 because dividing the right side of the equation cancels out the multiplier of 100, and dividing the left side of the equation, or 120/100, equals 1.2.

Step 4


Multiply both sides of the equation by 10 to solve for "x," or your mental age. Since "x" is currently the numerator in the fraction x/10, multiplying by 10, or 10/1 to be specific, yields 10x/10, or simply, "x." Multiplying the left side of the equation equals 12, or 1.2 * 10. Therefore, x=12. So in this example, your mental age is 12.

Warnings



  • Cognitive development slows at 16, then stops at 18, making the calculation of mental age irrelevant.
  • IQ tests for adults use a "standard deviation" formula measured against a mean score of 100. No mental age calculation is used in the IQ scores of adults.

Things You'll Need



  • IQ test
 
Umuhimu wa kujifunza saikolojia-2


WENGI kati ya watu wanaosumbuliwa na matatizo yanaoitwaya dunia ni wale wanaopambana na nguvu zao bila kujua. Kwa kutumia akili zao vibaya, hujitesa kwa kufikiri na kutafsiri vibaya matukio ya kila siku yanayotokea duniani.

Kama nilivyowahi kusema katika moja ya makala zangu nilizochapisha kwenye toleo la kitabu changu cha pili cha saikolojia ni kwamba hakuna kitu kibaya katika ulimwengu kwa asili, isipokuwa mawazo ya mtu mwenyewe.


Kwa mfano, tukizungumzia kufa ambapo watu wengi wanaamini kwamba ni jambo baya, kuna wengine wanaona ni zuri ndiyo maana wapo wanaojiua, na kama tukisema vita ni hatari, bado kuna watu wanafurahia vita kwa vile si wote wanaowahurumia wafao vitani hata kama wataona maiti zao barabarani kwa wingi.


Kama nilivyosema, duniani kuna nguvu mbili, ambazo ni za watu wenyewe na za ulimwengu, hii ina maana kuwa hata mawazo ya mwanadamu ni nguvu na mtu anaposumbukia kuwaza jambo fulani kwa undani kiasi cha kuumiza moyo wake anakuwa anashindana na nguvu zake mwenyewe.


Ifahamike kuwa kadiri mwanadamu anavyozidi kuongeza nguvu ya kufikiri, iwe kwa kukua kimwili, kusoma na kujifunza mambo mengi zaidi, kwa asili anakuwa anaongeza nguvu ambazo asipokuwa makini anaweza kufa akishindana nazo badala ya kuzitumia katika kumsaidia kimaisha.


Kwa mfano, watu kutoka kabila la Wabarabeigi wanaopatikana mkoani Manyara, nchini Tanzania wanaishi maisha ya kuwinda wanyama na kula mizizi ya porini, hawawezi kukaa wakifikiri jinsi ya kupata gari kwa kuwa kwao gari halina maana. Kwao maendeleo ni kuwinda na kuzaliana.


Kwa maana hiyo linapokuja suala la maisha magumu litatokana na ukame na wala si ukosefu wa mitaji au kazi. Hawa hawawazi magari kwa sababu hawajajifunza umuhimu wake, hawajui umuhimu wa kuwa na zahanati, hospitali na wala bei ya mafuta haiwasumbui. Lakini kwa Wachaga waliozoea umeme wakikosa huduma hiyo kwao hilo litakuwa ni tatizo kubwa litakalowakosesha usingizi.


Vivyo hivyo, kwa watu waliozoea kutibiwa kwa sindano na vidonge, wakikosa tiba hizo itakuwa rahisi kwao kufa, kwa sababu akili zao zinatafsiri ukosefu huo kama tatizo kubwa kwao, lakini haiwi hivyo kwa Wasukuma wanaoishi maporini kusikokuwa na hospitali za rufaa wala umeme.


Tafsiri ya hili ni nini? Ni fikra zitokanazo na kujua mambo na namna ya kuyawaza. Watu wengi siku hizi wanajua utajiri, wanafahamu nini maana ya afya, wanaelewa umuhimu wa maendeleo lakini siyo wote wenye uwezo wa kukutana na changamoto hizo na kupata matokeo sahihi ya kile wanachokifahamu.


Kwenda hospitali kupimwa na kuambiwa kuwa una Kansa, Ukimwi, Kisukari, Pumu, TB na magonjwa kama hayo, siyo jambo linalowasaidia wengi kwa vile hawajui hatua ya kuelekea kwenye ujuzi huo wa mambo. Hapa ndipo elimu ya saikolojia inapohitajika ili iweze kumsaidia

mtu anayejua mambo hayo namna ya kuyakabili, kuyaendeleza na kupata mafanikio.

Jambo la kusikitisha ni kwamba watu wengi wanaofahamu mambo hawafaidiki nayo na pale wanapojaribu kutumia ujuzi wao walioupata shuleni, wanajikuta wanaingia kwenye mapambano ya nguvu ya vile wanavyovifahamu.

Watu wengi leo hawalali usiku kucha wakipambana na yale waliyoyafahamu, utakuta mtu kakonda kwa sababu katambua mpenzi wake si mwaminifu, anakesha akilia bila kujua afanye nini kumaliza tatizo.

Mtu mwingine anakonda kwa sababu ni maskini, hana mtaji na ajabu nyingine kuna wanaosumbukia hata kasoro za maumbile yao ambazo wameumbwa nazo!
 
Kukabiliana na hali ya maumbile yako

inatakikana kwanza kujielewa wewe ni Binadamu umeumbwa na Mungu na Mungu hakufanya makosa katika vile

alivyokupa mwilini mwako. Ingawa Binadamu haridhiki na kile alichopewa na Muumba wake ndio utakuta mtu ana kipara

anatafuta dawa za kurudisha nywele.Utamkuta mwanamke anataka awe na kikalio kikubwa wengi wanataka wawe na

Maziwa makubwa, utamkuta mtu mwengine ana kibamia anataka awe na dushelele kubwa na kadhalika. Binadamu ni

kiumbe dhaifu sana ameumbwa na Mungu lakini anayo mapungufu yake binafsi kwa Mungu hakuna mapungufu wala

kasoro katika uumbaji wake kwa viumbe wake inatakikana utosheke na kile alicho kupa Muumba wako na Kuridhika ni

kitu muhimu kwa binadamu ninakuachia hapo kwaleo bibie Mashaxizo

Ningekua na tindi kali ungeioga MziziMkavu!!!!
 
Last edited by a moderator:
Aaaagh! humu jf mwishowe tutaanza kuwa machizi sasa na hizi psychologies, kila mtu na yake!
 
Mzizi mkavu, mimi binafsi napenda sana kujua saikolojia lakini bahati mbaya sana sijapata mtu wa kunipa mwanga juu ya somo hili nimejitahidi kutafuta kitabu kizuri na comprehensive juu ya somo hili sipati, hebu nisaidie ni kitabu gani kinaweza kunisaidia na upatikanaji wake kwa hapa Dar? natanguliza shukrani
 
kwani amefanya makusudi au hajui kwamba wewe sio bibie!?

Anafanya makusudi. just read between line kwa hayo tuloongea leo tu.

Kabla ya haya alishawahi kuniita bibie na nilimwambia mimi ni me.

Possible reason.

Kuna siku alitoa ushauri mbovu kule jf doctor, as a result kuna mmama alipoteza uja uzito wake. huyu mzee hakutaka kukubali kosa na alikua mkali kama mbogo. ikiwa hujawai ona pumba za huyu mzee itafute ile mada.

Mimi nilisoma madai nakueleza uhalisia kwamba yeye anahusika na huyo mwenzakeanahusika.

Baada hapo huyu mzee akaanza hako kamchezo.

Hapendi kuheshimiwa nami nakwenda nae vile anataka.
 
Anafanya makusudi. just read between line kwa hayo tuloongea leo tu.

Kabla ya haya alishawahi kuniita bibie na nilimwambia mimi ni me.

Possible reason.

Kuna siku alitoa ushauri mbovu kule jf doctor, as a result kuna mmama alipoteza uja uzito wake. huyu mzee hakutaka kukubali kosa na alikua mkali kama mbogo. ikiwa hujawai ona pumba za huyu mzee itafute ile mada.

Mimi nilisoma madai nakueleza uhalisia kwamba yeye anahusika na huyo mwenzakeanahusika.

Baada hapo huyu mzee akaanza hako kamchezo.

Hapendi kuheshimiwa nami nakwenda nae vile anataka.
Mkuu hiyo mada aliyotoa ushauri kule jf doctor unaweza ukaweka link, au title ya hiyo thread... kule jf complaints nimeona kuna mtu analalamika juu ya dawa alizouziwa...
 
Mkuu mzizi mkavu.darasa limeishia hapa?shusha nondo kaka!
 
tafuta kitabu cha psychology for teachers by prof mwamwenda.ni kitavu kizuri ila kwa dar unaweza pata maktaba za vyuo hasa udsm maeneo ya cafteria na pia kwa wauzaji vitabu pake ubungo wanaweza kukutaftia.pia unaweza ingia ebook then ukadownload vtabu vingi tu vya psy.
 
tafuta kitabu cha psychology for teachers by prof mwamwenda.ni kitabu kizuri ila kwa dar unaweza pata maktaba za vyuo hasa udsm maeneo karibu na cafteria na pia kwa wauzaji vitabu pake ubungo wanaweza kukutaftia.pia unaweza ingia ebook then ukadownload vtabu vingi tu vya psy.
 
Back
Top Bottom