Umuhimu wa kumsaidia Rais Samia katika kuirudisha Tanzania katika Misingi ya Haki

Umuhimu wa kumsaidia Rais Samia katika kuirudisha Tanzania katika Misingi ya Haki

MrMzalendo

Member
Joined
Apr 26, 2021
Posts
6
Reaction score
6
Ni ukweli ulio wazi ya kua Nchi yetu pendwa Tanzania ilikuwa inadidimia kwa kasi katika ktk suala la haki za raia wake. Mathalani ilikuwa imekua vigumu kwa watu kupaza sauti zao hata katika mambo yaliyo wazi kabisa kama wananchi kunyanyaswa, wafanya biashara kuonewa, wafanyanyakazi kutoongezewa mishahara na kupandishwa ngazi kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma.

Hii yote ilitokana na baadhi ya viongozi especially katika top level kutoheshimu sheria za nchi katika kutekeleza majukumu yao. Na hii ilisababisha kuongezeka kwa unafiki mwingi katika taifa ukiwemo watu fulani kuunga mkono juudi, kutesa watu ilimradi uonekane na walio juu nk.

Sasa Raisi SSH ameonesha kujali utawala wa Sheria, kuongea na kujadiliana inaanza ktk masuala mbalimbali kunaanza kurejea, walio kuwa hawagusiki wanaanza kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, furaha katika nyuso za watu zinaanza kurejea nk. Katika utekelezaji wake wa majukumu hajamuonea mtu, wala kumfokea mtu, wala kumtumbua mtu kwa sindano wala kumdhalilisha mtu bali ameacha tu sheria zitekelezwe na wala haja peleka bungeni sheriz kandamizi zitakazo mpa meno zaid.

Ni wazi watu wote wasomi na wasio wasomi ilmradi ni raia wa Tanzania, tunahitaji Raisi wa namna hii.Raisi ambae ukilala una uhakika wa kuamka salama. Raisi ambae atachagua kufuata sheria na katiba badala ya mapenzi yake binafsi, Raisi atakae chagua na kuteua viongozi waandamizi kwa misingi ya uweledi na wala sio kumtii na itikadi, Na Raisi ambae, watu wote watakuwa huru na salama na huyu ndo raisi tumtakae.

Kumekuwa na kundi dogo la watu linamkejeli. Linamdhihaki na kumtupia vijimaneno vya hovyo. Raisi wa namna hii tunahitaji kumtetea, kwa maana anatuunganisha tena. Nani asiyejua kuwa Taifa lilikuwa limegawanyika, limenuna, limevimba, watu hawapendani!!. Ni muda wa hao wanaojiita watunzaji wa legacy kujitafakari.

Mwisho nimsihi mama SSH, akumbuke kutuachia katiba mpya ambayo kila raisi ataifuata na kuitii. Hatukatai kuwa hatuna katiba la hasha! ila ni ukweli ulio wazi kuwa katba iliyopo, inatoa mwanya kwa kiongozi wa nchi kufanya akipendacho, anaweza kuwa dikteta na asitokee mtu wa kumkemea si kwa chama chake wala jeshi.

Tukitegemea busara zake kiongozi wa nchi haitadumu na lazima kila awamu adhaa ajitokeze mtu wa aina fulani ambaye ni lazima taifa liumie. Raisi, usichoke kulitafakali hili na usiwasikilize wale wa legacy ni wachache mnoo kuliko wanaopenda haki. Ujumbe kutoka kwa Mtanzania mpenda haki, amani na maendeleo.
 
Back
Top Bottom