mpesamoses
New Member
- Nov 21, 2019
- 2
- 3
Ukweli ni kwamba kwa umuhimu wa elimu hakuna shaka kusema ndio kiungo kikubwa kwenye maisha ya binadamu kwasababu hiyo ili jamii iwe ni jamii kamili na yenye usawa na lazima kuwaelimisha wanawake ambao wao ni kiunganishi kikubwa kwa zaidi ya asilimia sabini kwanini nasema hivyo
Kwa takwimu ya binadamu na makazi yani sensa inatupa majibu kwamba wanawake ni takriban robo tatu ya watu wote duniani sasa nikisema ni kiungo kikubwa namaanisha ,kwa hiyo kama watakuwa ni wengi na wenye uduni wa elimu hili ni wazi kwamba jamii zetu hazita ishiwa na ujinga na umasikini kwasababu wazalishaji wenye tija watabaki kuwa wachache na wakati huo walaji ni wengi na ikumbukwe kidogo hakiwezi kutosheleza kikubwa
Kwa hiyo vizuri wazalishaji wakawa wengi na wasomi pia wakawa si wengi tu bali ni wote kwasababu suala la kukosa elimu ni suala ambalo humpelekea mwanamke kunyanyasika na kubwa zaidi kudhurumiwa haki zake za msingi kwa mfano katika suala la kawaida kabisa la kufanya miamala ya kutoa fedha hasa kwa kutumia mitandao ya simu inashauriwa nywila ni siri ya mtu mmoja tu na hasa mmiliki wa kadi ya simu lakina kulingana na uduni wa elimu watu wengi wameendelea kutoa nywila zao na wameendelea kuibiwa sasa kama suala hili la fedha anashindwa kulilinda vipi kuhusiana na afya na mazingira ni tatizo tena tatizo kubwa sana
Basi kwanini tunasema wanawake na kukazia wapewe elimu hii ni kutokana na kwamba wanawake unapofikia umri wa kuendeleza elimu zao katika madaraja ya juu ndipo hapo changamoto zao zinakuwa nyingi kutokana na kitendo cha upevukaji wao na ubadilikaji wa maumbile ya miili yao kitendo ambacho huwaweka katika hali ya kusumbuliwa na vishawashi vingi sana mwisho wake hudondoka na kuishia kupata mimba za utotoni wakati kijana wa kiume yeye ataendelea na masomo yake na kuhitimu bila kusumbuliwa na jambo lolote.
Tukisema umuhimu wa kumpa elimu mwanamke sio tu kumpeleka shule ni pamoja na kumlinda kwa sheria kali na zinazosimamiwa ipasavyo kwa kuwaadhibu wote wanaopelekea kukwamisha juhudi za serikali katika utoaji wa elimu kwa mtoto wa kike.
Ukweli ni kwamba mwanamke ni jinsia na sio udhaifu wala ujinga ukweli ni kwamba mwanamke ukitoa utofauti wa jinsia anaweza kufikiri na kuamua kama mwanaume lakini pia ana uwezo wakufanya jambo lolote muhimu kama afanyavyo mwanaume.
Itambulike tu wazi kwamba zama za ukandamizaji zinatakiwa kukoma na kila jinsia ijadiliwe kwa-:heshima, kanuni na utu bila ya kuijadili jinsia ya kike kama dosari na chanzo cha matatizo na pia ikumbukwe chanzo kikubwa cha matatizo ya kila siku ya wanawake ni uhaba wa upewaji elimu kulingana na ukubwa wa mfumo dume ambao ulikalilishwa hata kwenye akili za wanawake na wao kuukubali.
Ukweli ni kwamba kumuelimisha na kumpa dondoo za kimsingi mwanamke bila kujali kiwango cha elimu na bila kuwatenga kwenye madaraja yanayoonesha hadhi zao kunaweza kusaidia mapinduzi makubwa sana wote tukashuhudia mabadiliko makubwa katika jamii zetu na taifa kiujumla. Kwanini nimelisema hili la kutokuwaweka kwenye madaraja kiasi kikubwa ni kwasababu wanawake wenyewe ni tofauti na wanaume katika suala la kuyachukulia mambo kwa wepesi Ukweli ni kwamba mwanamke asiyealikwa kwenye jambo kuhudhulia ni ngumu sana ukitofautisha na mwanaume kwa hiyo ili kuweza kutoa elimu na ifike bila kipingamizi inatakiwa elimu itolewe mubashara kwenye vituo vya runinga pamoja na matamasha ya nje kwa wingi na inabidi kuelezea mara zote kwamba mwanamke ni binadamu mwenye jinsia ya kike na kuachana na baadhi ya maneno kama kusema (mwanamke sio kiumbe kizuri)
Tukiondokana na dhana hizi na wote tukujiona kama ni binadamu ambao tunaweza kupata haki sawa ikiwemo -:mavazi,maradhi na chakula na mengine mengi lakini kubwa likiwa ni elimu ya nadharia pamoja na vitendo ambayo hiyo ndiyo msingi wakujitegamea na kuzidi kupambana na ukandamizwaji dhidi yao.
Lakini ukweli na uwazi ni kwamba ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii, taifa na ulimwengu kwa ujumla, kwani ikumbukwe ya kwamba kabla mtoto hajakabidhiwa kwa walimu wa ulimwengu mwalimu namba moja kabla ya wote ni mama.

Upvote
1