Umuhimu wa kuombea uchaguzi wa 2025 katika Taifa letu: Somo toka Ukraine

Umuhimu wa kuombea uchaguzi wa 2025 katika Taifa letu: Somo toka Ukraine

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Gia aliyoingia nayo Zelensky kwenye kampeni ya uchaguzi huko Ukraine ni KUAHIDI KULETA AMANI kwenye majimbo mawili ya Donbass yaliyojitenga. Aliahidi kuwa atayaruhusu kuwa na uhuru wa ndani lakini yakiwa ndani ya nchi ya ukraine kama ilivyo Hongkong iliyo huru lakini chini ya himaya ya China. Hilo wananchi wengi wa Ukraine walilipenda sana hasa baada ya kushuhudia mauaji makubwa katika vita kati ya majimbo ya Donbass yaliyojitenga na Ukraine. Ukraine ilishindwa kuyarudisha kwa nguvu za kijeshi. Kikundi pekee ambacho hakikupenda kauli hiyo ya Zelensky ni wale wenye itikadi kale ya mwelekeo wa Kinazi almaarufu kama "NATIONALISTS"/wapigania uhuru ambao huwaona wenyeji wa Donbass walio warusi kama wavamizi tu na hawapaswi kujitawala.​

A gamble for Ukraine's president​

By Jonah Fisher, BBC Kiev correspondent

President Zelensky made bringing peace to eastern Ukraine his number one election promise.

Watu wengi baada ya kupendezwa na ahadi hiyo ya Zelensky, wakamchagua kuwa Rais wa Ukraine. Alipopata urais akawageuka wananchi wake kwa kushirikiana na Marekani. Badala ya kuleta amani akaamua kuyarudisha hayo majimbo yaliyojitenga kwa nguvu. Marekani wakamwambia watamsaidia kushinda upinzani na mauaji yakaendelea tena. Kuona hivyo Urusi ikaamua kuwakingia kifua warusi walio wengi huko Donbass na ikatangaza kuyatambua rasmi kisha kuingia kijeshi kuyatetea. Matokeo ni mauaji na uharibifu mkubwa bambao usingetokea kama Zelensky angetekeleza kama alivyoahidi.

Hoja yangu ni kwamba Mungu ndiye ajuaye mioyo ya watu. Mtu anaweza kuahidi vizuri akiwa na lengo la kupata ushindi tu lakini moyoni ana lake jambo kama ilivyokuwa kwa Zelensky. Kwa hiyo tunapoelekea uchaguzi mkuu wa 2025, watanzania tunapaswa kumwomba sana Mungu ili tupate viongozi watakaokuwa wakweli na wenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo, amani na mshikamano katika nchi yetu!! Mungu atuepushe na matapeli kama Zelensky wanaosema hiki lakini kufanya kingine kisicho na maslahi mapana kwa Taifa. Wa-ukraine sasa wanajuta yaliyowakuta!! Tukimwomba Mungu kama Taifa tutaepushwa na uharibifu mkubwa hasa unaotokana na ushawishi mchafu wa mataifa ya magharibi, ambayo hutumia rushwa kushawishi viongozi kufuata matakwa yao.​
 
Back
Top Bottom