Toofast
JF-Expert Member
- Dec 23, 2015
- 522
- 942
Hii ni special kwa wasio kuwa na uelewa wa kupaki gari lenye automatic transmission kwa usahihi.
Hatua ni kama zifuatavyo:
1. Kikawaida gari likiwa kwenye drive au reverse ukiwa unajiandaa kupaki, cha kwanza kabisa ni kukanyaga breki ya mguu na kushift hadi kwenye neutral.
2. Kisha baada ya hapo utavuta breki ya mkono na kuachia breki ya mguu kwa sekunde kadhaa kwa ajili ya kuruhusu uzito wa gari ushikiriwe na breki ya mkono.
3. Kisha utakanyaga tena breki ya mguu na kushift hadi kwenye parking.
4. Kisha kuzima gari.
Umuhimu ni kwamba hizi hatua zinasaidia kulinda gearbox isiwe inabeba uzito wa gari kwa muda mrefu ukiwa umepaki. Kwa hiyo, uzito utakuwa unashikiliwa na breki ya mkono, na gearbox itadumu kwa muda mrefu.
Naongea hivi kwa sababu mimi nishawahi kupata matatizo yatokanayo na kutokufuata hatua za hapo juu. Mfano:
1. Gari lilikuwa likichengi gear kutoka parking kwenda drive na kuna sauti ya kitu kugonga ilikuwa inatoka. Lakini ATF ipo ya kutosha na safi, vile vile na mounting ni nzima.
2. Gari kuna wakati linachelewa kuchenji gia (delay shifting), lakini ATF ipo full tena ni safi na haina mileage kubwa.
Angalizo: Hizo hatua hapo juu haziwahusu wale wenye magari ambayo yana electronic parking brake, kwa sababu mimi sina uzoefu na gari hizo.
Hitimisho: Uzi tayari karibuni kuchangia, na najua wajuaji hawatakosekana.