Umuhimu wa Kupaki gari lenye kutumia automatic transimission kwa usahihi

Umuhimu wa Kupaki gari lenye kutumia automatic transimission kwa usahihi

Ni mambo yasiyo na umhim. P inajitosheleza sana labda ksma umepaki sehem ya mtrremko ama mlima ndo ufuate ushauri wako vinginevyo mm nimezoea nakanyaga foot brake then naweka p nazima gari
 
Hii ni special kwa wasio kuwa na uelewa wa kupaki gari lenye automatic transmission kwa usahihi

Hatua ni Kama zifuatavyo:
1.kikawaida gari llikiwa kwenye drive
au reverse ukiwa unajiandaa kupaki
cha kwanza kabisa ni kukanyaga
breki ya mguu na kushift hadi
kwenye neutral
2.Kisha baada ya hapo utavuta breki
ya mkono na kuachia breki ya
mguu kwa sekunde kadhaa kwa ajili
ya kuruhusu uzito wa gari ushikiriwe
na breki ya mkono
3.Kisha utakanyaga tena breki ya
mguu na kushift hadi kwenye
parking
4.kisha kuzima gari

so umuhimu ni kwamba hizi hatua zinasaidia kulinda gearbox isiwe inabeba uzito wa gari kwa muda mrefu ukiwa umepaki, kwa hiyo uzito. Utakuwa unashikiliwa na breki ya mkono kwa hiyo gearbox itadumu kwa muda mrefu

Naongea hivi kwa sababu mimi nishawahi kupata matatizo yatokanayo na kutokufuata hatua za hapo juu mfano 1.gari lilikuwa ukichengi gear kutoka parking kwenda drive kuna sauti ya kitu kugonga ilikuwa inatoka lakini
atf ipo ya kutosha na safi vile vile na mounting ni nzima

2.Gari kuna mda linachelewa kuchenji gia ( delay shifting) lakini
atf ipo full tena ni safi na haina mile age kubwa

Angalizo:
Hizo hatua hapo juu haziwahusu wale wenye magari ambayo yana electronic parking brake, kwa sababu
mimi sina uzoefu na gari hizo

Hitimisho:
Uzi tayari karibuni kuchangia na najua wajuaji hawatakosekana
Gear box itabebaje uzito wa gari ikiwa at rest na wakati huohuo parking brakes zimeshika? Hata kama hukuchukua precaution ya kuzirelease gears bado uzito wa gari (hata ukipark uphill) utakuwa absorbed na parking brakes!
 
Mkifikia kujadili baiskeli na maguta mniambie!!
 
Ni mambo yasiyo na umhim. P inajitosheleza sana labda ksma umepaki sehem ya mtrremko ama mlima ndo ufuate ushauri wako vinginevyo mm nimezoea nakanyaga foot brake then naweka p nazima gari
Watu wana complicate maisha. Huo ndio utaratibu tunaotumia miaka na miaka na gearbox haijawahi zingua.
 
Ipo hivi kwanza inashauriwa break ya mkono (handbrake) utumie pale tu inapobidi hasa kwenye miinuko lakini tafouti na hivyo kama unapaki sehemu tambalale weka kwenye P tu inatosha kwani handbrake kidogo kina shida kwenye kukirekebisha kinapoleta itata hivyo kinastahili kulindwa pia
umekosea, japo kwenye tambarare P haichukui uzito wa gari kama kupaki kwenye slope
 
Sijawahi kuendesha automatic Lakini kwa uzoefu wangu kwenye foleni ni neutral halafu parking brake
 
Kinacho sababisha giabox kuharibika ninini? Je ikiwa inagonga inaweza kutengenezeka?
Gearbox ikiharibika kutengeneza ni ngumu ila kama ikiwa inashindwa kufanya kazi Kwa ufanisi hapo inaweza kurekebishwa ambapo wengi ndo huita kutengeneza,mfano gearbox aibadili gia au inachelewa kubadili gia au Ina slip ,au gearbox inashindwa kuruhusu gari kurudi nyuma hizo shida zote zinaweza kurekebishwa kabisa

Kikubwa kinachosababisha gearbox kuharibika ni 1.ukosefu wa kilainishi(ATF au CVT whatever) au kutumiwa Kwa gearbox ikiwa na kilainishi pungufu Kwa muda mrefu
2.kutumia Kilaishi kisicho sahihi yaani ambacho kilichokuwa akijashauriwa na mtengenezaji mfano gari inatakiwa kutumia ATF ambayo dextron IV wewe unaweka dextron II au gari inatakiwa kutumia CVT fluid wewe unaweka ATF
3.kutokufanya routine au preventive maintainance mfano gearbox inaweza kuwa na leakage kutokana na kupasuka Kwa sample lakini kukosekana Kwa ufatiliaji inaweza kupelekea gearbox kufa
4.nk

Umeuliza kama gearbox ikiwa inagonga je inaweza kutengenezeka: jibu ni ndio inawezekana kabisa na mara nyingi inaweza kuwa inagonga Kwa sababu ya shida ya mounting kuwa dhaifu au pengine diff muhimu ni kufatilia tu
 
1. Press break to stop
2. Shift gear lever to Neutral
3. Engage parking brake, also known as a handbrake or emergency brake
4. Shift/press gear lever to the parking gear or parking pawl hiyo ndio sahihi kama mtoa mada alivyotoa ushauri.
 
huwezi kujua umuhimu wake mpka itokee siku gari unayoendesha igongwe kwa nyuma
Nilidhani ni salama zaidi ikigongwa ikatembea kuliko ikigongwa ikasota naomba elimu juu ya umuhimu huo
 
Kaka najaribu kufanya hivi lakini inakuwa nguma hasa nkipaki sehemu zene mteremko au mlima,coz ukiweka neutral gari inaendelea kuserereka

Nkisema niweke handbrake pia haishiki

Nazani hii ina apply sehemu tambarare ambazo ukiweka neutral gari inaweza simama.
Huyu mleta uzi ana agenda ya siri, huenda ana garage
 
FB_IMG_16964210592711439.jpg
 
Back
Top Bottom