Umuhimu wa Kupaki gari lenye kutumia automatic transimission kwa usahihi

Umuhimu wa Kupaki gari lenye kutumia automatic transimission kwa usahihi

Point ya msingi kwenye foleni unatakiwa kuweka gear kwenye neutral...
 
Mie nikisema kwenye miinuko wewe ukasema kwa kunipinga kua hata kwenye miteremko bado sijaona tofauti maana palipo na miinuko automatically kuna miteremko sijaelewa point yako ilikuwa nini ila nimecheka zaidi eti Hadi kwenye foleni unavuta handbrake duh
Kwahiyo mkuu wewe kwenye foleni huwa ni mguu kati mpaka gari zitakapoanza kuondoka?
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Mzee wewe gari yako ilikuwa na tatizo la gearbox from the start. Hizo hatua kwanza hazina ukweli wowote. nina chombo tangu 2015 hadi leo sijawahipo kufanya hizo hatua ulizozitaja na sijawahi kupata tatizo lolote la gear box. Mambo mengine ni MYTHS tu
 
mzee nashukuru kwa mchango wako
ni kweli parking mechanism ni tough lkn unavopaki gari bila kufata hatua za hapo juu ,unakuwa unaiuwa gearbox taratibu hususani kama unapaki sehemu yenye kilima yaani ingekuwa ugonjwa ningeweza kusema hilo tatizo basi ni kansa,halitokei yaani ghafla Ila baada ya gari kuwa na mileage za kutosha ndo utaanza kuona effects zake
Naomba unichanganulie hapa,vipi wakati wa kutaka kuondoka napo inakuwaje,ina maana utapaswa ukanyage brake,then uweke gear kwenye neutral then uachie handbrake au utaondoka kama kawaida?-Hapa nazungumzia kwa gari iliopaki kwenye kilima pua inaangalia bondeni...
 
Kwanza kabisa general name ni parking brake. Maana siyo zote zinakuwa operated na mikono. Gari kama Spacio, Premio, n.k. parking brake zake zinakuwa operated na mguu.

Pili, I wish ungejua parking mechanism ya gearbox ilivyo. Aiseeee haiko kimayai mayai. Ni tough.

Tatu, Parking mechanism has nothing to with matatizo ya gearbox ambayo uliyapata. Sijui kuchelewa kubadili gear au mshtuko.

Ni hivyo tu.
Fundi wa kwanza duniani kwenda against hii general recommendation

Fundi wa kwanza duniani niliyemsikia anarecommend uzito wote wa gari ulalie kile ki parking pawl

Wewe huwa ni fundi wa umeme sio? Sio mechanical per se?
 
Hii ni special kwa wasio kuwa na uelewa wa kupaki gari lenye automatic transmission kwa usahihi

Hatua ni Kama zifuatavyo:
1.kikawaida gari llikiwa kwenye drive
au reverse ukiwa unajiandaa kupaki
cha kwanza kabisa ni kukanyaga
breki ya mguu na kushift hadi
kwenye neutral
2.Kisha baada ya hapo utavuta breki
ya mkono na kuachia breki ya
mguu kwa sekunde kadhaa kwa ajili
ya kuruhusu uzito wa gari ushikiriwe
na breki ya mkono
3.Kisha utakanyaga tena breki ya
mguu na kushift hadi kwenye
parking
4.kisha kuzima gari

so umuhimu ni kwamba hizi hatua zinasaidia kulinda gearbox isiwe inabeba uzito wa gari kwa muda mrefu ukiwa umepaki, kwa hiyo uzito. Utakuwa unashikiliwa na breki ya mkono kwa hiyo gearbox itadumu kwa muda mrefu

Naongea hivi kwa sababu mimi nishawahi kupata matatizo yatokanayo na kutokufuata hatua za hapo juu mfano 1.gari lilikuwa ukichengi gear kutoka parking kwenda drive kuna sauti ya kitu kugonga ilikuwa inatoka lakini
atf ipo ya kutosha na safi vile vile na mounting ni nzima

2.Gari kuna mda linachelewa kuchenji gia ( delay shifting) lakini
atf ipo full tena ni safi na haina mile age kubwa

Angalizo:
Hizo hatua hapo juu haziwahusu wale wenye magari ambayo yana electronic parking brake, kwa sababu
mimi sina uzoefu na gari hizo

Hitimisho:
Uzi tayari karibuni kuchangia na najua wajuaji hawatakosekana

Kaka najaribu kufanya hivi lakini inakuwa nguma hasa nkipaki sehemu zene mteremko au mlima,coz ukiweka neutral gari inaendelea kuserereka

Nkisema niweke handbrake pia haishiki

Nazani hii ina apply sehemu tambarare ambazo ukiweka neutral gari inaweza simama.
 
Kwanza kabisa general name ni parking brake. Maana siyo zote zinakuwa operated na mikono. Gari kama Spacio, Premio, n.k. parking brake zake zinakuwa operated na mguu.

Pili, I wish ungejua parking mechanism ya gearbox ilivyo. Aiseeee haiko kimayai mayai. Ni tough.

Tatu, Parking mechanism has nothing to with matatizo ya gearbox ambayo uliyapata. Sijui kuchelewa kubadili gear au mshtuko.

Ni hivyo tu.
Imeisha.
 
Fundi wa kwanza duniani kwenda against hii general recommendation

Fundi wa kwanza duniani niliyemsikia anarecommend uzito wote wa gari ulalie kile ki parking pawl

Wewe huwa ni fundi wa umeme sio? Sio mechanical per se?
Hapo nmeenda against na nini mkuu?

Umepaki gari tambalale unaengage parking brake? Hapo kuna uzito gani umelalia parking pawl?

Mimi ni fundi wa umeme yes ila lete gearbox yoyote nitakuonesha parking pawl ilipo ndani.
 
Naomba unichanganulie hapa,vipi wakati wa kutaka kuondoka napo inakuwaje,ina maana utapaswa ukanyage brake,then uweke gear kwenye neutral then uachie handbrake au utaondoka kama kawaida?-Hapa nazungumzia kwa gari iliopaki kwenye kilima pua inaangalia bondeni...
Unakanyaga brake then unashift kutoka park kwenda drive kama unataka kwenda mbele na reverse kama unataka kurudi nyuma then una release handbrake baada ya hapo mwendo
 
Kaka najaribu kufanya hivi lakini inakuwa nguma hasa nkipaki sehemu zene mteremko au mlima,coz ukiweka neutral gari inaendelea kuserereka

Nkisema niweke handbrake pia haishiki

Nazani hii ina apply sehemu tambarare ambazo ukiweka neutral gari inaweza simama.
Unachotakiwa kufanya baada ya kuweka neutral ,engage handbrake haraka iwezekanavyo ,usisikilizie hata kidogo ,ukisikilizia lazima gari litaserereka tu,pia unaweza ukawa umefanya kama nilivyokwambia lakini gari Bado gari likaserereka ukiona hivyo jua handbrake Ina shida either handrake ipo out of adjustment so inabidi ifanyiwe adjust au ibadilishwe linerbrake Kwa gari inayotumia linerbrake na diskbrake Kwa gari ,inayotumia disk brake.
 
Back
Top Bottom