Umuhimu wa Kupaki gari lenye kutumia automatic transimission kwa usahihi

Point ya msingi kwenye foleni unatakiwa kuweka gear kwenye neutral...
 
Kwahiyo mkuu wewe kwenye foleni huwa ni mguu kati mpaka gari zitakapoanza kuondoka?
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Mzee wewe gari yako ilikuwa na tatizo la gearbox from the start. Hizo hatua kwanza hazina ukweli wowote. nina chombo tangu 2015 hadi leo sijawahipo kufanya hizo hatua ulizozitaja na sijawahi kupata tatizo lolote la gear box. Mambo mengine ni MYTHS tu
 
Naomba unichanganulie hapa,vipi wakati wa kutaka kuondoka napo inakuwaje,ina maana utapaswa ukanyage brake,then uweke gear kwenye neutral then uachie handbrake au utaondoka kama kawaida?-Hapa nazungumzia kwa gari iliopaki kwenye kilima pua inaangalia bondeni...
 
Fundi wa kwanza duniani kwenda against hii general recommendation

Fundi wa kwanza duniani niliyemsikia anarecommend uzito wote wa gari ulalie kile ki parking pawl

Wewe huwa ni fundi wa umeme sio? Sio mechanical per se?
 

Kaka najaribu kufanya hivi lakini inakuwa nguma hasa nkipaki sehemu zene mteremko au mlima,coz ukiweka neutral gari inaendelea kuserereka

Nkisema niweke handbrake pia haishiki

Nazani hii ina apply sehemu tambarare ambazo ukiweka neutral gari inaweza simama.
 
Imeisha.
 
Fundi wa kwanza duniani kwenda against hii general recommendation

Fundi wa kwanza duniani niliyemsikia anarecommend uzito wote wa gari ulalie kile ki parking pawl

Wewe huwa ni fundi wa umeme sio? Sio mechanical per se?
Hapo nmeenda against na nini mkuu?

Umepaki gari tambalale unaengage parking brake? Hapo kuna uzito gani umelalia parking pawl?

Mimi ni fundi wa umeme yes ila lete gearbox yoyote nitakuonesha parking pawl ilipo ndani.
 
Unakanyaga brake then unashift kutoka park kwenda drive kama unataka kwenda mbele na reverse kama unataka kurudi nyuma then una release handbrake baada ya hapo mwendo
 
Unachotakiwa kufanya baada ya kuweka neutral ,engage handbrake haraka iwezekanavyo ,usisikilizie hata kidogo ,ukisikilizia lazima gari litaserereka tu,pia unaweza ukawa umefanya kama nilivyokwambia lakini gari Bado gari likaserereka ukiona hivyo jua handbrake Ina shida either handrake ipo out of adjustment so inabidi ifanyiwe adjust au ibadilishwe linerbrake Kwa gari inayotumia linerbrake na diskbrake Kwa gari ,inayotumia disk brake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…