Umuhimu wa kusamehe

Umuhimu wa kusamehe

Lover boi

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
316
Reaction score
439
Nini maana halisi ya kusamehe?

Kusamehe ni kuamua kutomchukulia mtu hatua na kuondoa kinyongo moyoni mwako kutokana na jambo baya ulilofanyiwa na mtu huyo. Kusamehe kunasema hutakiwi kusikia neno “nisamehe” ndipo uendelee na maisha yako. Kusamehe kumewekwa na ni kwa manufaa zaidi kwa yule aliyekosewa.

Faida za kusamehe ni

1. Unakuwa huru katika harakati zako

2. Kuimarika kiafya mfano kuepuka kuwaza(msongo wa mawazo)

3. Kuondoa hasira na chuki

4. Kuondoa utawala wa mtu mwingine katika akili yako

5. Ni aina bora ya kisasi

6. Kiashiria cha ukomavu

7. Kuongeza utulivu wa akili

8. Kuinyesha upendo.

Asanteni.
 
Upo sahihi, watu wengi wamekuwa wakipata matatizo kwenye afya zao baada ya kushindwa kusamehe kwa muda mrefu.

Madhara yake yanajitokeza baada ya miaka mingi kupita.

Ukisamemehe sio tu kwa ajili ya aliekukosea bali hata kwa ajili yako mwenyewe.
 
Shukrani
 
Nini maana halisi ya kusamehe?

Kusamehe ni kuamua kutomchukulia mtu hatua na kuondoa kinyongo moyoni mwako kutokana na jambo baya ulilofanyiwa na mtu huyo. Kusamehe kunasema hutakiwi kusikia neno “nisamehe” ndipo uendelee na maisha yako. Kusamehe kumewekwa na ni kwa manufaa zaidi kwa yule aliyekosewa.

Faida za kusamehe ni

1. Unakuwa huru katika harakati zako

2. Kuimarika kiafya mfano kuepuka kuwaza(msongo wa mawazo)

3. Kuondoa hasira na chuki

4. Kuondoa utawala wa mtu mwingine katika akili yako

5. Ni aina bora ya kisasi

6. Kiashiria cha ukomavu

7. Kuongeza utulivu wa akili

8. Kuinyesha upendo.

Asanteni.
Maneno ya Mungu yanasema hivi... Usishindwe na ubaya bali ushinde ubaya kwa wema

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa, kuishi na makosa ya mtu rohoni mpaka yanakuniga eti tu hutaki kusamehe na kusahau ni sawa na kubeba gunia la mchanga mgongoni halafu uanze kuogelea baharini, matokeo yake hakuna asiyeyajua...
 
Jifunzen kudeal nawatu wabaya wenu Kichwa kwa kichwa

Hata Ng'ombe mkorofi dawa yake ni kumshika mapembe.

Mambo ya kusamehee yalishapita.

Akikutenda moja..tenda mawili.

Akikujibu shit, jibu shit mara mbili

Maisha ya kubembelezana yalishapitaaaa.

Mimi kuna watu wawili hivi karibun walitaka kuniharibia maisha ya ulaji...Mamaee sasa hivi navyoongea muda wowote wanatolewa Kazini . Wananipigia simu tu kunuomba msamaha et nikawaombee msamaha huko juu...walimwaga mboga, hawakujua Ugali wao jinsi unavyopikwa namm naujua, sasa nikaumwaga huo ugali .

Haya Maisha saizi ni Timing tu.

Wacha wakaonje joto la ubaya.
 
Sometimes wewe unaesema 'nimsamehe'
Kumbe wewe ndo mkosefu...

Watu wengi tunajipa Haji ya kuwahukumu wengine na kujipa nafasi ya kuwa hatuna makosa...
 
Back
Top Bottom