SoC01 Umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo

Stories of Change - 2021 Competition

Abrianna

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
4,696
Reaction score
15,390
Utangulizi
Dira kwa maana fupi ni muelekeo. Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision (TDV) 2025 ilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 1999 ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2000 lengo kuu likiwa kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. 'www.tanzania.go.tz' (tovuti kuu ya serikali)

Melengo makuu matano yalioainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025 ni pamoja na kuboresha hali ya maisha ya kila Mtanzania, kuwepo kwa mazingira ya amani usalama na umoja,kujenga utawala bora,kujenga jamii iliyoelimika na kujenga uchumi imara unaokabiliana na ushindani. (Nukuu kutoka Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025).

Katika andiko hili, nitaangazia malengo makuu matano kama yalivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025. Andiko langu litaangazia pia utekelezaji wa malengo haya na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Katika uhalisia, Maendeleo ya Nchi yetu kwa asilimia kubwa yamekua yakitegemea Ilani ya chama tawala pamoja vipaumbele vya Rais aliye madarakani. Mfano halisi ni ununuzi wa ndege na ujenzi wa madaraja ambao uliingiza nchi katika madeni makubwa na umaskini. Ni wazi kwamba Dira ya Maendeleo ni kijarida tu ambacho kimetengenezwa kutimiza wajibu lakini hakina nafasi kubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Serikali imeunda mipango mingi kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo kama vile mpango wa maendeleo wa miaka mitanpo (Five Year Development Plan), MKUKUTA, Mpango wa Big Results Now (Matokeo Makubwa Sasa), Mpango wa maboresho ya utumishi wa Umma,pamoja na Maleongo ya Maendeleo ya Millenia chini ya nchi za Umoja wa Mataifa.

Katika mipango tajwa, yote ina malengo yanayolandana kwa maana ya kutokomeza umaskini kwa kuboresha huduma za afya, elimu, nishati, kilimo, maji, biashara, mahusiano ya kimataifa, ajira, kuboresha utumishi wa umma, kuweka usawa wa kijinsia pamoja na mengine mengi.

Hebu tuangazie miaka kumi nyuma tulinganishe na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na hali halisi ya Watanzania mpaka leo hii.

Hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kuwa duni pamoja na kwamba nchi yetu ipo katika uchumi wa kati wa chini, Mtanzania wa kawaida anashindwa kumudu gharama ndogo za mlo wa siku ilhali tunatangaziwa uchumi wetu umekua kwa asilimia 7% ( NBS 2019/2020).

Katika kujenga utawala bora, hali imezidi kuwa tete, ni wazi kwamba utawala wa sheria umekua jambo gumu katika nchi yetu hali inayopelekea kutokuwajibika kwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma (Rejea ripoti ya CAG 2020).

Katika Dira ya Mendeleo 2025, serikali imeonyesha nia ya kujenga jamii iliyoelimika na inayojifunza kila siku kulingana na mazingira na nyakati tulizopo, tukirudi kwenye uhalisia, kiwango cha ubora wa elimu zetu hakikidhi viwango vitakavyowawezesha wasomi wetu kuingia katika ushindani ndani na nje ya Tanzania, shule zetu nyingi hazina waalimu wa kutosha wala vifaa vya kufundishia, matamko ya kisiasa kwa upande mwingine yamekua yakiathiri mifumo ya elimu.

Kwa mfano mnamo mwezi Desemba 2020, Rais JPM aliagiza somo la historia ya Tanzania lianze kufundishwa katika shue za msingi mpaka sekondari, Wizara ya elimu iliandaa machapisho kwa ajili ya somo husika lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani somo hilo lilisitishwa rasmi.

Kwa upande mwingine serikali ilichangia kupotosha jamii badala ya kuelimisha. Nitoe mfano mdogo wa janga la Covid 19. Serikali ilisimama kidete kuuaminisha umma kwamba janga hili ni vita ya mabeberu dhidi yetu badala ya kutumia wataalamu wa afya kutoa elimu kuhusu namna bora ya kujikinga ili kuepuka maambukizi. Serikali ilienda mbali zaidi na kuhamasisha tiba mbadala na njia za asili ambazo zilitumika katika vituo vya afya pia.

Kauli ya serikali pamoja na viongozi wakuu wa nchi imeleta mkanganyiko pamoja na hisia tofauti juu ya janga hili na kusababisha watu kuishi pasipo kuchukua tahadhari hata baada ya serikali kubadili msimamo na kuamua kufuata njia za kitaalamu. Ukijaribu kuongea na watanzania kumi, tisa kati yao wanaogopa chanjo na kuamini kwamba mabeberu wanataka kutumaliza.

(picha kutoka mtandaoni)

Katika uboreshaji wa utumishi wa umma, vilio vimekua vingi, utekelezaji wa dhima hii umesahaulika kwa miaka zaidi ya mitano iliyopita, vilio vingi vya wafanyakazi kuhusu nyongeza za mishahara pamoja na kupanda madaraja, makato makubwa, na mishahara duni ambayo haikidhi maisha ya kila siku.

Mambo ya muhimu yaliyotajwa katika utekelezaji wa malengo ya milenia ni pamoja na kukuza mahusiano ya kimataifa, kutokomeza umaskini wa kipato na njaa. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Tanzania imepuuza kwa kiasi kikubwa sana mahusiano ya kimataifa kutokana na misimamo ya kiongozi aliyekua madarakani. Vipato vya wananchi vimeshuka kutokana na tozo kubwa katika bidhaa na huduma, mfumuko wa bei umeathiri pembejeo za kilimo na bidhaa mbalimbali, uonevu kwa wafanyabiashara,ubambikaji wa kesi na kodi uliosababisha biashara nyingi kufungwa. Tunao mfano halisi wa sasa katika tozo ya miamala ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi masikini ambao hata kula yao ni ya tabu.

Mapendekezo
• Serikali ianzishe taasisi maalumu kwaajili ya kuandaa na kusimamia Dira ya Maendeleo ya Taifa. Chombo hicho kiwe na kazi ya kuandaa, kusimamia pamoja na kuishauri serikali iliyopo madarakani bila kujali chama.Taasisi hii ihakikishe sera sera na mipango ya taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wizara zina uelekeo mmoja na zinashirikiana ka ukaribu. Kwa mfano suala la kuzalisha wahitimu wenye weledi ni lazima liendane na uboreshaji mfumo wa elimu, kwa hiyo ni lazima wizara ya kazi na wizara ya elimu zishirikiane kubaini mapungufu yanayoonekana kwa wahitimu wanaoajiriwa ili waweze kubaini njia bora ya kuboresha.

Taasisi hii ipewe mamlaka ya kusimamia serikali kama ilivyo bunge na mahakama na kwamba ilani ya chama cha kiongozi aliyeko madarakani ilenge kutafuta au kuonyesha njia sahihi za kuipeleka nchi kule ambako dira inaonyesha, hii itasaidia kutekeleza miradi iliyoachwa au iliyoanzishwa na kiongozi aliemaliza muda wake, mfano wakati Rais JPM naingia madarakani alisitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa madai kwamba mikataba ilikua mibovu na iliyojaa unyonyaji, siku chache baada ya Rais Samia kuingia madarakani mapitio ya ujenzi wa bandari yameanza, hii ni kwa sababu hakuna mfumo wa kusimamia viapaumbele vya maendeleo ya Taifa badala yake kila kiongozi anajiamulia kile anachopenda.

• Ipatikane katiba imara ambayo itasaidia kudhibiti na kusimamia viongozi walioko madarakani na hata baada ya kustaafu kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Marekani na Afrika ya Kusini. Hii itahakikisha viongozi wote wanafanya kazi kwa kuheshimu haki za binadamu na sheria na taratibu zilizopo bila kuathiri malengo ya Taifa kwa ujumla. Katiba imara pia itasaidia kuweka uwajibikaji na usawa kati ya watumishi/viongozi, kuondoa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

• Serikali ijikite zaidi katika kuvumbua vyanzo vipya vya mapato badala ya kujikita katika kuongeza kodi katika huduma mbalimbali za kijamii ili kupunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa wananchi na badala yake wananchi wapate unafuu wa maisha. Mfano sekta ya utalii na madini zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama tukiweka usimamizi mzuri na mifumo ya kuaminika ili kuepusha mianya ya ubadhirifu. Pia serikali ijikite katika kuboresha mfumo wa elimu ili kuruhusu vijana wengi kujiajiri katika nyanja mbalimbali badala ya kutegemea ajira kutoka serikalini.

• Bajeti za maendeleo zilizoidhinishwa na bunge zisitumike kinyume na lengo ili tuweze kutekeleza mipango iliyopangwa katika mwaka wa fedha wa serikali. Huko nyuma tulishuhudia pesa zikipelekwa katika matumizi ambayo hayakuidhinishwa na bunge hali iliyochangia kukwamishwa kwa miradi mingi ya maendeleo iliyoidhinishwa na bunge. Bajeti inayoidhinishwa pia iende sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

• Serikali iunde mfumo shirikishi utakaosaidia wananchi kushiriki katika kuonyesha vipaumbele vya maendeleo pamoja na utekelezaji. Hii itasaidia wananchi kuwa wasimamizi wa moja kwa moja wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

• Serikali iwatumie wataalamu wa masuala ya uchumi walioko nchini badala ya kutumia wanasiasa pekee katika kuandaa bajeti na matumizi ya serikali, pia serikali ijenge utamaduni wa kuwatumia wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali nchini katika kuandaa na kusimamia sera mbali mbali kwaajili ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa pamoja na kuheshimu mawazo na maelekezo ya wataalamu katika sekta mbalimbali hata pale yanapotokea majanga yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu. Kwa kufanya hivi, tutapunguza au kudhibiti matamko ya kisiasa katika mambo nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu kama vile Afya, Elimu na Uchumi.

Hitimisho
Natoa wito kwa viongozi/wenye mamlaka, na watunga sera wa nchi, maamuzi yoyote wanayofanya yanaathiri au kufaidisha jamii nzima, wao ni sehemu ya jamii na hivyo wataathirika au kufaidika na maamuzi hayo kwa namna moja au nyingine. Ni vyema kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kufanya maamuzi ili kuepuka athari zozote zitakazoisababishwa na maamuzi yao ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Asanteni Sana​
 
Upvote 1.3K
Hiyo yote ni kwa sababu hatuna chama cha kisiasa cha upinzani madhubuti waliopo nao ni wale wale kama wa CCM maslahi yao binafsi wanayatanguliza mbele
Kuna shida sana, chadema ndio inajifia siku hizi bora hata zamani ilikua tishio, raia na sisi tumekaa tumetulia kama vile mambo ni shwari kabisa
 
Keep on dreaming. Chadema is here to stay for so many years.
Mkuu BAK nakusalimu mkubwa wa kazi, Chadema haina mwelekeo kwa sasa, hawana dira wanahitaji msaada
Mimi ni mwanachadema kindakindaki and I HATE CCM ila chama changu kinakatisha tamaa
 
Hakina mwelekeo kwa kesi za KUBAMBIKIWA? Acha hizoooo Maccm yalishajifia siku nyingi sasa yamebaki kubebwa na polisiccm na mahakamaccm. Tia hiyo kauli kichwani mwako.

Mkuu BAK nakusalimu mkubwa wa kazi, Chadema haina mwelekeo kwa sasa, hawana dira wanahitaji msaada
Mimi ni mwanachadema kindakindaki and I HATE CCM ila chama changu kinakatisha tamaa
 
Hakina mwelekeo kwa kesi za KUBAMBIKIWA? Acha hizoooo Maccm yalishajifia siku nyingi sasa yamebaki kubebwa na polisiccm na mahakamaccm. Tia hiyo kauli kichwani mwako.
Ndio maana nasema bila katiba mpya na kuitoa ccm madarakani hakuna kitu, hata chadema wanapata tabu kwa sababu raia wameridhika, hatuwaungi mkono vya kutosha, bila kutumia nguvu ya umma hakuna kitu chadema itafanya, umma wenyewe ni akina nani wana uthubutu wa kuchukua hatua. Chadema wanatangaza makongamano ya katiba au maandamano lakini hakuna anaejitokeza zaidi ya viongozi ambao mwisho wa siku wanakamatwa wote and we are here doing nothing about it zaidi ya kuandamana kwenye keyboarda na kuwachangia. Wakati mwingine its not even about money, its about our unity, tusimame nao hata bila pesa, lets go out there polisi wakitupiga na sisi tunapambana nao, hakuna dola imewahi shinda nguvu ya umma
 
Raia wameridhika wapi? Unaongea na watu kuhusu maisha ya hofu, kuhusu kupanda gharama za maisha, kuhusu kukosa nyongeza ya mishahara kwa miaka sita sasa, kuhusu kukosekana ajira, kuhusu kuanguka kwa uchumi, elimu, huduma muhimu n.k. Wafanyakazi, Wakulima na Wafanyabiashara wote wanalia, Unaishi wapi huko kwenye Watanzania walioridhika na mwelekeo wa maisha? 😳

 
Watu ambao hawajaridhika huwa wanachukua hatua, miaka sita hakuna aliechukua hatua unasema hawajaridhika? Na bado tumeongezewa tozo kama saba na ushee, kwani mkuu wewe upo dunia gani? Sisi tumekubaliana na matokeo ya uchaguzi hakuna hata aliejitokeza barabarani, tulitulia tuliii mohome kwetu, tozo ndio hizo, mwenyekiti anahenyeshwa tupo tunaimba wimbo wa uzalendo, ni lini tutaamka?
 
Ahsante kwa mada nzuri...
Lakini pia vyama vya Siasa vinabidi ndiyo vyewe wajibu wa kusimamia dira ya Taifa asa chama kinachokua madarakani. Tukipigie kura chama kitakachoweza kusimama na dira ya Taifa..
Mpaka sasa hakuna hicho chama mkuu, labda kitokee chama kingine
 
Unadhani kwanini Watanzania wengi walifurahia kifo cha yule dhalimu mwendazake? Watu walioridhika na maisha yao wanaweza kufurahia kifo cha the so called their leader? Raia kutoingia mtaani haina maana wameridhika na mwelekeo wa maisha yao.

 
Unadhani kwanini Watanzania wengi walifurahia kifo cha yule dhalimu mwendazake? Watu walioridhika na maisha yao wanaweza kufurahia kifo cha the the so called their leader? Raia kutoingia mtaani haona maana wameridhika na mwelekeo wa maisha yao.
Watu walifurahia lakini haitoshi, something has to be done
 
Nakubaliana nawe si unaona mambo ya Hamza, mtaani wengi wanamuona ni Shujaa. Si unamsikia Mutungi anaweweseka na mikutano ya IGP na vyama vya siasa sijui kwa kutumia vipengele vipi vya katiba ya nchi au sheria za nchi za IGP ZERO eti akutane na vyama vya siasa.

Watu walifurahia lakini haitoshi, something has to be done
 
Hii ni nzuri, mimi natamani waweke sheria kandamizi na waongeze tozo mpaka wananchi wapate akili, watatufilisha tunapotaka kufika bila shaka ni suala la muda tu pengine raia wataamka kutoka usingizini maana tozo zinawagusa maccm pia na familia zao
 
Asante sana Freddie Matuja kwa kushare hiyo clip

Ni kweli tunahitaji mabadiliko ya sera zetu ili ziendana nyakati tulizopo, sio sera tu bali hata sheria zetu pamoja na strategy tunazozitumia katika kupanga na kutekeleza mipango yetu ya maendeleo

Na ili haya yote yafanyike, tunahitaji inputs za wataalamu mbalimbali, kama ulivyosema kwamba tunahitaji watu wenye fikra tofauti za kimaendeleo pasipo kuingiza propaganda za kisiasa na pia tinahitaji kujifunza kutoka nchi za wenzetu ambao wametuzidi

Nimeshauri pia katika andiko langu kwamba mambo mengi ya kitaalamu yatatuliwe kitaalamu na sio kisiasa.

Nakubaliana na wewe pia kwamba uongozo madhubuti ndio nguzo imara lakini niongezee kwamba uongozi madhubuti lazima uendane na katiba imara, kwa namna hiyo hata dira ya maendeleo itasimamiwa ipasavyo na itatekelezwa kama ilivyopangwa pasipo kuathiriwa na siasa au matakwa binafsi ya kiongozi
 
Maafisa mipango wapo na Tume ya mipango ipo, ila hiyo dira wanayoiandaa na mipango wanayoipanga haina usimamizi, hata wao wenyewe hawawezi kuisimamia itekelezwe kwa wakati, unadhani nini kifanyike?
Suluhisho ni katiba mpya,na dira ambayo haitoandaliwa na maafisa mipango pekee,dira iandaliwe na jopo la wataalamu ambalo litahusisha watu wenye taaluma mbalimbali ili kuweza kupata mafanikio makubwa,pia serikali ifanye kazi kutokana na dira iliyopo na pale ikitokea ukiukwaji wowote basi viongozi waliopo madarakani wawajibishwe.
 
Hilo pia ni tatizo la nchi kuongozwa na fikra za mtu mmoja,(Mkuu wa Nchi), kama nchi ingekuwa na dira inayoeleweka na inayotekelezeka basi ni rahisi hata wataalamu kuishauri serikali kwakuwa watakuwa na reference sahahi kutoka kwenye dira,ila kwa hali ilivyo sasa ni ngumu Wataalamu kuishauri serikali kwakuwa hata muda mwingine hawajui mkuu wa nchi anataka kuipeleka nchi kwenye uelekeo upi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…