SoC01 Umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo

Stories of Change - 2021 Competition

Abrianna

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
4,696
Reaction score
15,390
Utangulizi
Dira kwa maana fupi ni muelekeo. Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision (TDV) 2025 ilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 1999 ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2000 lengo kuu likiwa kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. 'www.tanzania.go.tz' (tovuti kuu ya serikali)

Melengo makuu matano yalioainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025 ni pamoja na kuboresha hali ya maisha ya kila Mtanzania, kuwepo kwa mazingira ya amani usalama na umoja,kujenga utawala bora,kujenga jamii iliyoelimika na kujenga uchumi imara unaokabiliana na ushindani. (Nukuu kutoka Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025).

Katika andiko hili, nitaangazia malengo makuu matano kama yalivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025. Andiko langu litaangazia pia utekelezaji wa malengo haya na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Katika uhalisia, Maendeleo ya Nchi yetu kwa asilimia kubwa yamekua yakitegemea Ilani ya chama tawala pamoja vipaumbele vya Rais aliye madarakani. Mfano halisi ni ununuzi wa ndege na ujenzi wa madaraja ambao uliingiza nchi katika madeni makubwa na umaskini. Ni wazi kwamba Dira ya Maendeleo ni kijarida tu ambacho kimetengenezwa kutimiza wajibu lakini hakina nafasi kubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Serikali imeunda mipango mingi kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo kama vile mpango wa maendeleo wa miaka mitanpo (Five Year Development Plan), MKUKUTA, Mpango wa Big Results Now (Matokeo Makubwa Sasa), Mpango wa maboresho ya utumishi wa Umma,pamoja na Maleongo ya Maendeleo ya Millenia chini ya nchi za Umoja wa Mataifa.

Katika mipango tajwa, yote ina malengo yanayolandana kwa maana ya kutokomeza umaskini kwa kuboresha huduma za afya, elimu, nishati, kilimo, maji, biashara, mahusiano ya kimataifa, ajira, kuboresha utumishi wa umma, kuweka usawa wa kijinsia pamoja na mengine mengi.

Hebu tuangazie miaka kumi nyuma tulinganishe na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na hali halisi ya Watanzania mpaka leo hii.

Hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kuwa duni pamoja na kwamba nchi yetu ipo katika uchumi wa kati wa chini, Mtanzania wa kawaida anashindwa kumudu gharama ndogo za mlo wa siku ilhali tunatangaziwa uchumi wetu umekua kwa asilimia 7% ( NBS 2019/2020).

Katika kujenga utawala bora, hali imezidi kuwa tete, ni wazi kwamba utawala wa sheria umekua jambo gumu katika nchi yetu hali inayopelekea kutokuwajibika kwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma (Rejea ripoti ya CAG 2020).

Katika Dira ya Mendeleo 2025, serikali imeonyesha nia ya kujenga jamii iliyoelimika na inayojifunza kila siku kulingana na mazingira na nyakati tulizopo, tukirudi kwenye uhalisia, kiwango cha ubora wa elimu zetu hakikidhi viwango vitakavyowawezesha wasomi wetu kuingia katika ushindani ndani na nje ya Tanzania, shule zetu nyingi hazina waalimu wa kutosha wala vifaa vya kufundishia, matamko ya kisiasa kwa upande mwingine yamekua yakiathiri mifumo ya elimu.

Kwa mfano mnamo mwezi Desemba 2020, Rais JPM aliagiza somo la historia ya Tanzania lianze kufundishwa katika shue za msingi mpaka sekondari, Wizara ya elimu iliandaa machapisho kwa ajili ya somo husika lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani somo hilo lilisitishwa rasmi.

Kwa upande mwingine serikali ilichangia kupotosha jamii badala ya kuelimisha. Nitoe mfano mdogo wa janga la Covid 19. Serikali ilisimama kidete kuuaminisha umma kwamba janga hili ni vita ya mabeberu dhidi yetu badala ya kutumia wataalamu wa afya kutoa elimu kuhusu namna bora ya kujikinga ili kuepuka maambukizi. Serikali ilienda mbali zaidi na kuhamasisha tiba mbadala na njia za asili ambazo zilitumika katika vituo vya afya pia.

Kauli ya serikali pamoja na viongozi wakuu wa nchi imeleta mkanganyiko pamoja na hisia tofauti juu ya janga hili na kusababisha watu kuishi pasipo kuchukua tahadhari hata baada ya serikali kubadili msimamo na kuamua kufuata njia za kitaalamu. Ukijaribu kuongea na watanzania kumi, tisa kati yao wanaogopa chanjo na kuamini kwamba mabeberu wanataka kutumaliza.

(picha kutoka mtandaoni)

Katika uboreshaji wa utumishi wa umma, vilio vimekua vingi, utekelezaji wa dhima hii umesahaulika kwa miaka zaidi ya mitano iliyopita, vilio vingi vya wafanyakazi kuhusu nyongeza za mishahara pamoja na kupanda madaraja, makato makubwa, na mishahara duni ambayo haikidhi maisha ya kila siku.

Mambo ya muhimu yaliyotajwa katika utekelezaji wa malengo ya milenia ni pamoja na kukuza mahusiano ya kimataifa, kutokomeza umaskini wa kipato na njaa. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Tanzania imepuuza kwa kiasi kikubwa sana mahusiano ya kimataifa kutokana na misimamo ya kiongozi aliyekua madarakani. Vipato vya wananchi vimeshuka kutokana na tozo kubwa katika bidhaa na huduma, mfumuko wa bei umeathiri pembejeo za kilimo na bidhaa mbalimbali, uonevu kwa wafanyabiashara,ubambikaji wa kesi na kodi uliosababisha biashara nyingi kufungwa. Tunao mfano halisi wa sasa katika tozo ya miamala ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi masikini ambao hata kula yao ni ya tabu.

Mapendekezo
• Serikali ianzishe taasisi maalumu kwaajili ya kuandaa na kusimamia Dira ya Maendeleo ya Taifa. Chombo hicho kiwe na kazi ya kuandaa, kusimamia pamoja na kuishauri serikali iliyopo madarakani bila kujali chama.Taasisi hii ihakikishe sera sera na mipango ya taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wizara zina uelekeo mmoja na zinashirikiana ka ukaribu. Kwa mfano suala la kuzalisha wahitimu wenye weledi ni lazima liendane na uboreshaji mfumo wa elimu, kwa hiyo ni lazima wizara ya kazi na wizara ya elimu zishirikiane kubaini mapungufu yanayoonekana kwa wahitimu wanaoajiriwa ili waweze kubaini njia bora ya kuboresha.

Taasisi hii ipewe mamlaka ya kusimamia serikali kama ilivyo bunge na mahakama na kwamba ilani ya chama cha kiongozi aliyeko madarakani ilenge kutafuta au kuonyesha njia sahihi za kuipeleka nchi kule ambako dira inaonyesha, hii itasaidia kutekeleza miradi iliyoachwa au iliyoanzishwa na kiongozi aliemaliza muda wake, mfano wakati Rais JPM naingia madarakani alisitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa madai kwamba mikataba ilikua mibovu na iliyojaa unyonyaji, siku chache baada ya Rais Samia kuingia madarakani mapitio ya ujenzi wa bandari yameanza, hii ni kwa sababu hakuna mfumo wa kusimamia viapaumbele vya maendeleo ya Taifa badala yake kila kiongozi anajiamulia kile anachopenda.

• Ipatikane katiba imara ambayo itasaidia kudhibiti na kusimamia viongozi walioko madarakani na hata baada ya kustaafu kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Marekani na Afrika ya Kusini. Hii itahakikisha viongozi wote wanafanya kazi kwa kuheshimu haki za binadamu na sheria na taratibu zilizopo bila kuathiri malengo ya Taifa kwa ujumla. Katiba imara pia itasaidia kuweka uwajibikaji na usawa kati ya watumishi/viongozi, kuondoa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

• Serikali ijikite zaidi katika kuvumbua vyanzo vipya vya mapato badala ya kujikita katika kuongeza kodi katika huduma mbalimbali za kijamii ili kupunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa wananchi na badala yake wananchi wapate unafuu wa maisha. Mfano sekta ya utalii na madini zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama tukiweka usimamizi mzuri na mifumo ya kuaminika ili kuepusha mianya ya ubadhirifu. Pia serikali ijikite katika kuboresha mfumo wa elimu ili kuruhusu vijana wengi kujiajiri katika nyanja mbalimbali badala ya kutegemea ajira kutoka serikalini.

• Bajeti za maendeleo zilizoidhinishwa na bunge zisitumike kinyume na lengo ili tuweze kutekeleza mipango iliyopangwa katika mwaka wa fedha wa serikali. Huko nyuma tulishuhudia pesa zikipelekwa katika matumizi ambayo hayakuidhinishwa na bunge hali iliyochangia kukwamishwa kwa miradi mingi ya maendeleo iliyoidhinishwa na bunge. Bajeti inayoidhinishwa pia iende sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

• Serikali iunde mfumo shirikishi utakaosaidia wananchi kushiriki katika kuonyesha vipaumbele vya maendeleo pamoja na utekelezaji. Hii itasaidia wananchi kuwa wasimamizi wa moja kwa moja wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

• Serikali iwatumie wataalamu wa masuala ya uchumi walioko nchini badala ya kutumia wanasiasa pekee katika kuandaa bajeti na matumizi ya serikali, pia serikali ijenge utamaduni wa kuwatumia wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali nchini katika kuandaa na kusimamia sera mbali mbali kwaajili ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa pamoja na kuheshimu mawazo na maelekezo ya wataalamu katika sekta mbalimbali hata pale yanapotokea majanga yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu. Kwa kufanya hivi, tutapunguza au kudhibiti matamko ya kisiasa katika mambo nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu kama vile Afya, Elimu na Uchumi.

Hitimisho
Natoa wito kwa viongozi/wenye mamlaka, na watunga sera wa nchi, maamuzi yoyote wanayofanya yanaathiri au kufaidisha jamii nzima, wao ni sehemu ya jamii na hivyo wataathirika au kufaidika na maamuzi hayo kwa namna moja au nyingine. Ni vyema kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kufanya maamuzi ili kuepuka athari zozote zitakazoisababishwa na maamuzi yao ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Asanteni Sana​
 
Upvote 1.3K
Sawa kabisa, bila katiba haya yote hayawezekani, tunahitaji sana katiba imara
 
Shukrani sana SHIMBA YA BUYENZE cha muhimu ni ujumbe uwafikie walengwa, upande wa kura kuna changamoto sana kwa wanaotumia app unless mtu aingie kupitia chrome au opera ndio ataweza kupiga kura, au hata kwenye PC.
 
Muheshimiwa-hongera sana kwa kupitia kwenye jukwaa la story of change ,nikajua upo tu kwenye jukwaaa pendwa la jf photos 😀
 
lets go Abrianna, ur too close to win .
Mkuu unaonaje kama serikali ingeipa mikoa au wilaya mamlaka ya kujitawala yenyewe,yani kwa maana kwamba wawe na viongozi ambao wanachaguliwa na wanachi let's say mkuu wa mkoa anachaguliwa na wanachi,then anaunda balaza lake ambalo linafanana na baraza la mawazi kutokana na wabunge na madiwani,mapato yawe yanatumika katika mikoa husika baada ya bajeti husika kupitishwa na hilo baraza,je unadhani hii ingesaidia kuongeza kasi ya maendeleo katika sehemu nyingi nchini?
 
kwa upande wa macho mawili ingefaa sana kuwa hivyo kila mkoa kujiendeleza na fursa,rasilimali zilizopo na zinazoweza
kukidhi mahitaji ya wananchi na mkoa husika,pengine wananchi wangekuwa wanatumia nguvu kidogo katika kuongea na
viongozi wao kuliko sasa rais anakuwa na majukumu mengi katika kutembelea kila mkoa,

kingine changamoto za ajira zitapungua kwa kasi kwasababu ya mkoa husika kuongeza mahitaji ya fursa kwa wanachi husika
ndani ya mkoa,pia kutakuwa na urahisi wa uangalizi wa ukusanyaji wa mapato kuoneka kwa urahisi.
 
Mfumo wa majimbo kama uliokuwa unapendekezwa na Lissu kama angeshinda urais? Pengine Case Study nzuri ni Nigeria ambako wana huo mfumo. Umewasaidia kupiga hatua?

Faida yake mojawapo kubwa ni kusogeza huduma kwa wananchi kwa ukaribu zaidi hasa ukizingatia kuwa kuanzia gavana na watumishi karibu wote ni wa mkoa huo huo hivyo kidogo ni rahisi kuchochea moyo wa kizalendo. Na kwa vile gavana anachaguliwa na wananchi kidogo inaleta unafuu katika utendaji wake. Mfumo huu ndio pia unatumika Marekani. Kila jimbo hupambana kivyake kuongeza ufanisi wa elimu, ajira na huduma zingine za kijamii na nadhani huwa inawasaidia japo kuna fyoko fyoko za majimbo yenye utajiri mkubwa kama Texas kutaka kujitenga na kuwa nchi kamili.

Shida mojawapo kubwa ya mfumo huu ni mgawanyo wa raslimali kwa sababu majimbo mengine yana utajiri mkubwa wa raslimali na mengine hayana. Kama serikali haitakaa macho, ni rahisi kwa majimbo mengine kubakia masikini na mengine yakisonga mbele kwa kasi ya 5G. Kusini huko wakae na gesi yao. Usukumani huko wabaki na ziwa lao, dhahabu, almasi na mengineyo. Kaskazini huko wafaidike na Tanzanite yao na utalii wa Mlima Kilimanjaro na Serengeti. Wengine wasio na raslimali za kutosha watafanyeje hasa ukizingatia ufisadi wa kutisha ulio katika mifumo hii dhaifu?
 
sawa kabisa,baadhi ya mikoa itakuwa ipo juu kuliko mingine kimaendeleo,ila bado njia zipo za kuikuza mikoa ambayo
haina rasilimali za kutosha,kwa mfano wa nchi kama japan hawategemei sana kilimo bali wapo juu sana kwenye technologia zaidi
hii ni kutokana na geografia ya nchi husika hai sapoti kilimo bali wameona ni bora kujikita na technologia na mambo mengine hii ingefanyika
pia hapa Tanzania.
 

Mkuu wazo sio baya sana. Lakini naamini kabisa tukiweka ubinafsi pembeni na tukawa na katiba inayojali wananchi ikisindikizwa na dira ya mpango wa maendeleo ya taifa inayotekelezeka, wote tutafurahi.

Hatutaridhika wote lakini maendeleo yatagusa wengi. Hapo kwenye majimbo/ wilaya/ mikoa kuwe na aina ya mapato inayobaki kwao ili wafaidike na rasirimali zilizopo kwenye eneo lao huku sehem nyingine ikienda kugusa miradi ya kitaifa.

Ukitizama kwa umakini tumerundika nafasi za kazi amvazo zingegawanywa vizuri kuna pesa ingeokolewa nyingi tu.
Tuna wabunge, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala, unakuta kuna vyeo vipo kwa sababu ndio mfumo tulioukuta lakini kimsingi hakuna tija yeyote.

Hua nawaza, bunge letu ingekua ni biashara, kwa pesa tunayoiteketeza pale, na faida tunayoipata, vinawiana kweli? Nafikiri ni biashara inayotuingizia hasara.

Sio lazima tufanane na nchi nyingine, tunaweza kuwa na mfumo wetu wa kipekee ilimradi unatunufaisha kama taifa.

Watu hao hao wanapitisha sheria mapendekezo ya kipumbavu, siku mbili wanarejea tena na mapendekezo ya kutengua walichokipitisha kabla ya siku chache kupita, unajiuliza hawa jamaa kichwani wapo sawa kweli?

Unagundua suala la maslahi ya taifa sio kipaumbele chao, wanajaribu kuangalia upepo unaendaje na wakuu wanataka nini ili waende sambamba watetee vibarua vyao.

Tungekua na wataalam wachache tu wanaojadili maboresho ya sheria, wanapelekewa mapendekezo, iwe ni sheria mpya au kubadili iliyopo, wanaangalia faida na hasara kwa mapana kisha wanakuja na pendekezo la kitaalam. Tuache wataalam wafanye kazi zao.

Niishie hapa nisiharibu Jumapili yangu, kuna vitu vinatia hasira sana. Mtu anasema ni kweli nna nyumba ya kuishi lakini kwa sababu ni takwa la kikatiba, inabidi nijengewe, na anafurahia kabisa.

Haiwezi kutokea watu wanaonufaika na katiba mbovu iliyopo wakatuvusha kupata katiba mpya iliyobora, haitatokea. Hii ni vita.
 
Nadhani ingeongeza perfomance maana hakuna kiongozi ambae angekubali kuona mkoa wake nakua nyuma, na pia wangeweka jitihada ili kujijenga kwa wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…