Regani H masuki
New Member
- Sep 1, 2022
- 4
- 2
UMUHIMU WA KUWA NA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO NA KUZINGATIA UTAWALA BORA
Dira ya taifa ya maendeleo ni kielelezo ambacho jamii au taifa linaongozwa kufanikisha matakwa au matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi katika muda uliokusudiwa na matakwa hayo sharti yaeleweke na kukubaliwa na jamii au taifa linalohusika.
Moja ya mambo muhimu ili kuweza kuijenga Tanzania iliyo bora na iliyo imara ni lazima kama nchi kuwa na dira madhubuti (mpango mkakati) wa miaka 20-30 ili kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia na dira husika.
Umuhimu wa dira ya maendeleo katika nchi ni jambo la msingi na huiwezesha Serikali kufanya mambo kwa utaratibu maalumu bila kutegemea utashi wa mtu au kiongozi aliepo madarakani kwani dira hii huweka mipango yote na kila kiongozi ajae kwa kila kipindi ni lazima atekeleze majukumu yake kwa kuzingatia muongozo wa dira hii na sio vinginevyo.
Nchi yoyote isiyokuwa na dira yaani mpango mkakati unaoeleweka ni dhahiri ni ngumu kupiga hatua moja mbele kwani viongozi wa serikali hufanya mambo kwa utashi wao pekee jambo ambalo hufanya baadhi ya mambo kutokufikiwa malengo yaliyokusudiwa, mfano mzuri ni hivi, pale nchi inapokuwa na mpango mkakati kila kiongozi lazima afanye kazi kwa kufuata mpango huo,ikitokea kiongozi mmoja ameachia ngazi aidha kwa kuondoka ofisini au kujiudhulu kiongozi anaefuata au anaeingia ofisini lazima atalazimika kuendelea na kazi aliyoikuta ikiendelezwa na mtangulizi wake kwa kua dira itamtaka kufanya hivyo na kumwelekeza nini cha kufanya.
Tofauti na ilivyo kwa sasa katika nchi yetu nzuri ya Tanzania pamoja uongozi madhubuti uliopita na uliopo kwa sasa. Yapo mambo meengi mazuri yaliyo anzishwa na viongozi mbali mbali waliopita lakini baadhi ya mambo yameshindwa kutekelezwa au kukamilika kikamilifu sababu tu ya ukosefu wa dira maalumu ambayo ingewataka kila mmoja kutekeleza kile alichokikuta kikifanyika na mtangulizi wake na kukamilisha kisha kuendelea na mipango mingine kama ilivyoainishwa kwenye dira.
Jambo jingine la msingi ni kuwa na dira yenye matokeo chanya naya kujenga taifa ambazo zitakua na faida kwa jamii na taifa kwa ujumla, mfano wa mipango mkakati iliyo na faida kwa jamii na taifa ni kuwa na dira zinazoelekeza kujenga jamii iliyo na watu wenye ujuzi wa kisasa, sayansi na teknolijia sababu ulimwengu wa sasa niwa sayansi endelevu, pia kuwa na mipango ya kujenga miundombinu yenye ubora na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika kwani itasaidia kupunguza matatizo mengi na gharama kwa serikali. Kuwepo na usimamizi thabiti katika kila sekta ili kuwezesha utekelezaji ulio bora na wenye tija kwa taifa zima. Pia lazma kuwe na mpango mkakati wa kudumu wenye kupambana na rushwa kwani bila kua na mpango huu ni ngumu kutekeleza mambo mengi ndani ya taifa sababu rushwa ni chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo na kufanya mambo kuwa mabaya zaidi. Aidha, pamoja na kuwepo kwa dira ya taifa mambo haya huenda sambamba na uwepo wa serikali yenye utawala bora.
Utawala bora ni nini?
Huu ni utawala (serikali) ambayo huzingatia na kufuata utawala wa sheria kwa ujumla. Ni serikali ambayo huzingatia mambo mengi kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya nchi, mfano; haki na usawa,uwazi,uwajibikaji,matumizi bora ya madaraka na utawala unaozingatia demokrasia kwa ujumla.
Umuhimu wa kuwepo kwa utawala bora ndani ya nchi ni nini?.
Kwanza, utawala bora husaidia viongozi wa nchi kutekeleza na kutumia madaraka waliyonayo kwa kuzingatia matakwa ya sheria hivyo kupelekea kuwepo kwa haki na usawa kwa wananchi bila kujali umri, dini na jinsia.
Pili, utawala bora huzingatia uwepo wa uwazi na uwajibikaji hivyo kila jambo katika nchi hufanyika kwa uhuru na uwazi na haya yote huwezekana sababu ya kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla, pia mambo yote ndani ya serikali hufanyika kwa uwazi hivyo kila mtu kuwa na uelewa wa mambo yote ndani ya nchi, haya yote hufanyika sawasawa pale tu serikali inapowajibika kutekeleza mambo yake bila kuwepo kwa namna yeyote ya uzuiaji wa vyombo vya habari ama wananchi kwa ujumla kupata taarifa.
Tatu, utawala bora huzingatia uwepo wa demokrasia, uwepo wa demokrasia ndani ya nchi hufanya mambo kuwa sawa kila upande. Demokrasia ndani ya nchi huwezesha uwepo wa uhuru wa vyama vya siasa na uhuru wa wanachi kuchagua na kuchaguliwa kuhudumu katika nafasi mbali mbali ndani ya serikali ili kuwezesha kusonga mbele katika ujenzi wa taifa lililo bora na imara.
Nne, utawala bora huzingatia haki na usawa kwa jamii yote bila kujali rangi,umri,jinsia na hata dini. Katika nchi inayozingatia utawala bora maendeleo huja kwa haraka na kwa usawa kwani kila jambo huzingatia matakwa ya sheria za nchi na sio kwa kuzingatia utashi wa mtu au kiongozi husika. Utawala bora huzingatia haki na hivyo kufanya watu wote kuwa huru kufanya mambo yao bila kuogopa jambo lolote.
Hivyo kama nchi ili iweze kusonga mbele na kuweza kufikia malengo yaliyo endelevu ni lazima kuzingatia mambo makuu mawili ambayo ni uwepo wa dira ya taifa(mpango mkakati) na utawala bora. Kwa kuzingatia haya ni dhahiri taifa litakuwa katka hali nzuri na kufikia malengo yaliyo bora kwa mustakabali wa taifa zima.
Hata hivyo, dira hii ama mpango mkakati huu ni lazima utengenezwe au kutayarishwa kwa kuzingatia utaratibu maalumu ambao utaiwezesha serikali iweze kufanya yale mambo ambayo ni muhimu na yanayohitaji uharaka ili kuwawezesha wananchi kunufaika vilivyo na sio kuwa na dira au mpango mkakati ambao utakuwa hauna masilahi mapana kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Pia dira hii lazima ieleweke na kukubaliwa na jamii husika na pia ni lazma serikali kuhakikisha inaitekeleza vilivyo.

Attachments
Upvote
2