SoC02 Umuhimu wa kuwa na tafrija ya wanandoa wote wenye migogoro ili kutafuta ufumbuzi

SoC02 Umuhimu wa kuwa na tafrija ya wanandoa wote wenye migogoro ili kutafuta ufumbuzi

Stories of Change - 2022 Competition

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na migogoro mingi sana ya ndoa tofauti na ilivyokuwa zamani. Changamoto ni nyingi sana,labda sababu ya kipato, wengine ubize wa kazi, wengine mgongano wa mawazo na wengine labda matatizo ya kiafya na wengine ni kutokutilewa aut tu kwenda matembezi au sehemu mbalimbali.

Kulingana na kila mgogoro kuwa na changamoto yake huwenda kila mwandoa akashinda hii na kushindwa na nyingine. Mfano labda mimi ndoa yangu ilikuwa na mgogoro sababu ya ubize wa kazi lakini baada ya kugundua nikapambana kurekebisha ratiba yangu ili nisawazishe nigawe muda wa kazi na familia,nikafanikiwa ila bado kuna changamoto ndogo ndogo bado.

DHUMUNI LA TAFRIJA
Dhumuni la tafrija ni kubadilishana mawazo na kuweza kuulizana changamoto za ndoa kwa mwezio labda kama akifanikiwa kurekebisha alitumia mbinu gani ili na mimi nijifunze kupitia yeye. Kama kila mmoja atakuwa wazi huenda nikpata mbinu ambayo sikufahamu mwanzoni na mwingine akapata mbinu yangu iliyofaulu na sote kwa pamoja tukaweza kurekebisha changamoto hizo.

MUUNDO WA TAFRIJA
1.Wenzi wawili wa ndoa
2. Ukumbi mkubwa
3. Mziki laini wenye staha
4. MC mbobevu kwenye ndoa
5. Kuwe na vinywaji na vitafunwa mbalimbali
.


Kwenye kukaa baada ya kuingia basi wanaume watakaa upande wao na wanawake upande. Lengo ni nini? Kila mwanandoa awe huru kujifunza kupitia jinsia yake.

Tafrija zifanyike hata mara moja kwa mwaka na mikoa yote kulingana na mahitaji yao.

Utafiti mdogo niliofanya binafsi nimegundua changamoto zingine ndani ya ndoa zina tiba shida ni jinsi ya kuwafikia walengwa. Mwanamke anaweza kuwa na hasira sababu hujamtoa out muda mrefu au jirani au rafiki yake anatolewa mara kwa mara,sasa wivu au tamaa ya usaliti na kuhisi hapendwi kunaweza kuchangia migogoro pia.

Asanteni kama mmenielewa naombeni kura yenu. Niko tayari kujibu maswali mbalimbali hapa.
 
Upvote 5
Wengine watadundana huko huko ukumbini
😁😁😁Hapana, wanatakiwa kujua sehemu wanakoenda na dhumuni la tafrija hiyo,yani kama wanaenda kurefresh mind ili kupata mbinu mpya za kuishi pamoja.
 
Back
Top Bottom