Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

Inasemekana Dodoso (Questionnaire) lina maswali zaidi ya 100 ambayo hatuyajui yatahusu nini. Hivi kweli naweza kubuni vitu zaidi ya 100 watakavyouliza zaidi nikamfahamisha beki 3 na asisahau hata kimoja kweli??
Kwahiyo siku hizo tajwaza siku ya sensa tupumzike tu yani toka 23 to 31 of August ,na taifa litajengwa na nani
 
Na kuna hii nimeikuta mahali...

Ndugu zangu watendaji huko serikalini naombeni kuconfirm kama siku ya sensa ni siku ya kazi kama kawaida…. And if yes I am worried na quality ya data tutakazozipata …. Few thoughts/concerns

1. Ijumaa nilifanyia kazi nyumbani bahati nzuri kata ya kawe wakawa wanafanya pre-testing na ikaangukia nyumbami kwangu … sikuwa nimejiandaa lakini niliwapokea vizuri and it took two hours kumaliza

2. Kwa maswali yale ya pre- testing wakisema twenda makazini , I have a serious concern na data watakazocollect…. House helpers kamwe hawataweza jibu maswali yote yale …. They are many and detailed in actual fact hata mkuu wa kaya mwenye wakati mwingine atahangaika

3. Mama makinda hapo anasema tuache taarifa nyumbani …. Taarifa zipi na ni nani atajua taarifa gani za kuacha hakuna hata mwongozo… yale maswali yapo kwenye categories nyingi na ni mengi sasa mtu atajua ni taarifa gani za kuacha home? Mfano kama kaya yako inawakazi sita na wote wana NIDA utahitaji kutoa namba zao zote za nida as per the questionnaire, lakini pia kuna taarifa za elimu, vizazi na vifo katika kaya …. Ni house girl gani atakuwa na hizo data zote?

4. Uwezo wa wahojaji wenyewe siyo mkubwa ukilinganisha na maswali halafu ndo aje akutane na house helper …. Itakuwa garbage in garbage out huyu mtoto alokuja hapa kwangu for pre testing it was a disaster mpaka nikaihurumia nchi yangu…. Ilibidi mpaka nimwulize kiwango cha elimu akanambia anasoma VETA lakini ni kadogo na hana confidence kabisa ya kuuliza …. I had to help him maana natamani saana zoezi hili lifanikiwe….

I wish wa reconside hii decision kwakweli…. We need quality data for our next ten years plans.
Zoezi limenyimwa kwanza airtime ya kutosha,channels wanazotumia kutoa elimu sidhani kama zinaweza kumfikia mtu aliekua kijijini mambo yda kukurupuka ni ya hovyo ,ila hilo la kufanya siku ya sensa iwe yav mapumziko siliungi mkono maana siku ni nyingi siku ni 7 ni nyingi kwa taifa kupumzika tu,pia dodoso lina maswali mengine unnecessary wangebeba taarifa muhumi ingetosha
 
Moja ya swali ni kipato cha wastani cha kaya. Kwa hiyo umuachie housegirl au jirani hiyo taarifa kwamba bwana wastani wa kipato changu kwa mwezi ni laki 1.
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
 
Mi kwanza naishi kibachela hata ikiwa siku ya mapumziko nimeshaamua hawanipati sensa ni kichaka cha watu kupiga Kodi zetu tu maendeleo ya maisha ni juhud binafsi
 
IMG-20220818-WA0064.jpg
 
Nimefikiri mara mbilimbili kuhusu sensa ya watu na makazi. Nimegundua Ili kupata takwimu sahihi kabisa Kuna umuhimu wa kuruhusu siku hiyo iwe ya mapumziko.

Itasaidia kupata takwimu sahihi lakini pia wahusika wakubwa wa hizo familia watakiwepo nyumbani na hivyo kutoa taarifa sahihi.

Hayo ni maoni yangu.

Pia, soma: Serikali: 23 Agosti ni siku ya mapumziko
Ahsante Sana kwa Hoja Yako. Serikali imekusikia na tumeitendea haki Hoja hii. Tuendelee kuungana na Serikali yetu sikivu. Ahsante kwa Hoja
 
Back
Top Bottom