Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

Inasemekana Dodoso (Questionnaire) lina maswali zaidi ya 100 ambayo hatuyajui yatahusu nini. Hivi kweli naweza kubuni vitu zaidi ya 100 watakavyouliza zaidi nikamfahamisha beki 3 na asisahau hata kimoja kweli??
... hivi kuna ugumu gani kuweka hilo dodoso public tukajiandaa na hayo maswali yao?

Sioni ni kwa namna gani nitamruhusu msichana wa kazi na wanangu wadogo wafungue geti eti karani wa sensa aingie in my absence; hicho kitu hakipo.

Kwa kitu muhimu kama sensa kinachotokea mara moja in 10 years kuna ugumu gani watu wakabaki majumbani ili zoezi lifanikiwe?

Ni ajabu sana CCM hawajafanya kitu kikaenda successfully bila dosari za kijinga. Kama issue ni watu kutakiwa kwenda kuchapa kazi, busara ilikuwa sensa ifanyike siku ya Nane Nane, 2022; au Nane Nane, 2022 iwe siku ya kazi kutoa nafasi kwa siku ya sensa watu kuwa majumbani kwao.

Alternatively, wangefanya Jumapili lingefanikiwa zaidi. Kwa akili zao hawakuona umuhimu huo - zoezi linaenda kufeli kwa kiwango kikubwa.
 
Inaonekana hata wenye zoezi yaani serikali haipo serious ama haiamini katika hiyo sensa ila inatimiza tu matakwa ya kisheria.

Anyway watu wameshajipigia hela wacha wakazitumbue sasa.
 
Moja ya swali ni kipato cha wastani cha kaya. Kwa hiyo umuachie housegirl au jirani hiyo taarifa kwamba bwana wastani wa kipato changu kwa mwezi ni laki 1.
... ha ha ha! Lingine ni kama kwenye kaya kuna mwenye maradhi ya kudumu; nalo umwachie jirani! By the way, huyo karani wa sensa atajua nimemwachia majibu jirani yupi kati ya wengi nilio nao?

Nilitegema hamasa ingetolewa kwa wananchi kubaki majumbani siku ya sensa kufanikisha zoezi kumbe kwa akili zao ni kinyume kabisa!

Matokeo ya kuachia wazee waliochoka mwili na akili vitu muhimu vya kitaifa kama sensa ndio hayo! Hawana uwezo kabisa wa kufikiria "in all dimensions".
 
Mambo haya ya kuhesabiana kila baada ya miaka 10, yameshapitwa na wakati
Dunia ya leo inasajili kila Mtoto anayezaliwa na kutiwa kwenye data base.
Kila mtu mzima anapewa Kitambulisho afikapo miaka 18.
Huwezi safiri au kusajili simu bila Kitambulisho.
Huwezi piga kira au kufungua Account ya bank bila kitambulisho.
Huwezi kufungua Biashara na kutafuta leseni bila Ktambulisho.
Sasa Taarifa zote hizi walizokusanya serikali wanazifanyia nini?
Hata kama umekufa ,huzikwi bila ya kupata hati ya mazishi toka kwa serikali ya Mtaa
Dunia inatuwacha mbali sana.
Tanzania inaajiri watu zaidi ya 1/2 milioni kuendesha zoezi la sensa , mamilioni ya fedha kuharibiwa kuwalipa na kununua vifaa zikiwemo computer, Ipad na stationaries. Magari ya kuwasafirisha nk.

Hasara ni kubwa mno.
Ingelifaa Kusajili Watu wote na kuboresha miundombinu ya kusajili watoto wanaozaliwa na watu wanaokufa ili kuweka takwimu za watu walio hai nchini up to date kila uchao badala ya kusubiri miaka 10 na kuharibu mabilioni ya Shiling za wanyonge.
 
Ndugu wana jamvi nmeona Serikali imetoa taarifa kuwa Ile siku inayotangazwa Sana ya Sensa kuwa sio siku ya mapumziko. Kiukweli niseme serikali inakosea Sana na haitapata taarifa sahihi kabisa.

Kuna Baadhi ya nyumba hakuna anaebaki Nyumbani hivyo hata wakienda kesho yake hawatakuta mtu maana wote wanaenda kazini.

Pia wanasema ukiondoka uache taarifa zako Kwa anaebaki. Hilo ni ngumu Kwa vile sio Kila niliepanga nae ninamuamini kiasi cha kueza kumuachia taarifa zangu zote binafsi.

Pia Kwa wale walio na wadada wa kazi haiwezekani kuanza kumuambia mdada wa kazi taarifa zangu na familia Kwa ujumla maana ni kama kuwa wazi sasa kitu ambacho sio wote tupo tayari.

Pia hawajasema ni taarifa zipi ambazo zinatakiwa kuachwa ili wakija waweze jibiwa maana tangazo linasema Tu taarifa ziachwe Nyumbani.

Naishauri serikali hiyo siku waifanye iwe ya mapumziko ili kuondoa hizi dosari lasivyo watapata taarifa potofu kuwa tumefika 67m kumbe tupo pungufu

View attachment 2326622

View attachment 2326626
Naunga mkono hoja zako. Siku zote za nyuma sensa ilikuwa ikifanyika Jumapili. Sasa wamebadilisha bila kusema kasoro waliyoiona na mtindo huo wa zamani. Siku ya mapumziko, watu wengi zaidi wanakuwepo nyumbani.

Mdadisi wa sensa anapata taarifa kutoka kwa mhojiwa ambaye ni mkuu wa kaya na bila shaka mkuu huyo atakuwa kazini siku ya kazi. Habari zingine mdadisi anazipata kwa 'body language' ya mtoa taarifa na kama hakuridhika na jibu lililotolewa atauliza maswali ya nyongeza ili apate ufafanuzi. Aidha, kila mwanamke wa miaka 15 na kuendelea huulizwa maswali yeye mwenyewe kuhusu uzazi. Hajibiwi na mkuu wa kaya kama ilivyo kwa maswali mengine yote.

Itoshe kusema kwamba serikali imepotoka kuitisha sensa siku isiyo ya mapumziko ambapo watu wengi zaidi wangekuwepo majumban kwao. Hivyo taarifa kamilifu zaidi zingepatikana.
 
Alipoteuliwa tu huyu bibi kuwa Kamishina wa Sensa nikajua tayari sensa imeharibika mapema
Labda tusimlaumu sana huyo mkuu wa Sensa kwa kuwa kazi yake ni kutekeleza tu hilo zoezi. Mtu wa kuamua lini zoezi lifanyike ni Serikali. Rais ndiye anayetangaza siku ya kufanya sensa kwa mujibu wa sheria inayopitishwa na Bunge. Sana sana mkuu wa Sensa tunaweza kumshutumu kwa kutoielimisha Serikali vilivyo kuhusu kasoro za kufanya zoezi hilo siu ya kazi.
 
Naunga mkono hoja zako. Siku zote za nyuma sensa ilikuwa ikifanyika Jumapili. Sasa wamebadilisha bila kusema kasoro waliyoiona na mtindo huo wa zamani. Siku ya mapumziko, watu wengi zaidi wanakuwepo nyumbani.

Mdadisi wa sensa anapata taarifa kutoka kwa mhojiwa ambaye ni mkuu wa kaya na bila shaka mkuu huyo atakuwa kazini siku ya kazi. Habari zingine mdadisi anazipata kwa 'body language' ya mtoa taarifa na kama hakuridhika na jibu lililotolewa atauliza maswali ya nyongeza ili apate ufafanuzi. Aidha, kila mwanamke wa miaka 15 na kuendelea huulizwa maswali yeye mwenyewe kuhusu uzazi. Hajibiwi na mkuu wa kaya kama ilivyo kwa maswali mengine yote.

Itoshe kusema kwamba serikali imepotoka kuitisha sensa siku isiyo ya mapumziko ambapo watu wengi zaidi wangekuwepo majumban kwao. Hivyo taarifa kamilifu zaidi zingepatikana.
Na pia ina maana siku hiyo ya sensa akipita mdau Tu kavaa kikoi cha njano akagonga mlango atafunguliwa. Naona kabisa watu wengi Sana wakiibiwa vitu vyao majumbani Kwa gia ya waandikisha Sensa. Hii serikali ivi ni Nani mshauri wake!!!
 
Muda bado upo kwa serikali kulitafakari hili suala kwani kufeli kujua idadi ya watu kwa usahihi basi ndio mwanzo wa kufeli kwa mipango mengine mingi ya maendeleo.
Naafiki kabisa maoni haya. Ni bora kukiri kukosea halafu mambo yakarekebishwa kuliko kuwa 'big headed' na kuendelea tu na uamuzi japo umejua kwamba uamuzi huo una kasoro.
 
Moja ya swali ni kipato cha wastani cha kaya. Kwa hiyo umuachie housegirl au jirani hiyo taarifa kwamba bwana wastani wa kipato changu kwa mwezi ni laki 1.
Ila siyo exactly amount, uzuri ni wastani haina nguvu sana.
 
Ila siyo exactly amount, uzuri ni wastani haina nguvu sana.
Na swali hilo halipo, nadhani jamaa amebuni tu. Au ndivyo alivyolielewa swali japo halikutaka hayo ayasemayo
 
Labda tusimlaumu sana huyo mkuu wa Sensa kwa kuwa kazi yake ni kutekeleza tu hilo zoezi. Mtu wa kuamua lini zoezi lifanyike ni Serikali. Rais ndiye anayetangaza siku ya kufanya sensa kwa mujibu wa sheria inayopitishwa na Bunge. Sana sana mkuu wa Sensa tunaweza kumshutumu kwa kutoielimisha Serikali vilivyo kuhusu kasoro za kufanya zoezi hilo siu ya kazi.
Huyu kazi yake ni posho tu kila siku 250,000 pamoja na kulipiwa kila kitu
 
Hivi unadhani swali la uchumi wenu unategemea kitu gani bila kuambiwa umuachie beki tatu majibu utajuaje hivi unafahamu kuwa kuna maswali kama 100 hivi kwenye Dodoso dogo
Lamda uwe umeamua tu kwa dhati hutaki kuwezesha zoezi la sensa kwenda salama. Lakini kama unania sensa iende salama hakuna kikwazo chochote unavyowazia wewe. Kuna baadhi ya details ni za muhimu kuacha kama vile 1. Kitambulisho cha NIDA au namba 2. Tar ya kuzaliwa ili kupata umri. 3. Shughuli za kiuchumi nk nk. Lakini inakubidi utambue kuwa kama kuna baadhi ya Mambo yatashindwa kujibiwa na muwakilishi wa kaya na ikabidi mkuu wa kaya awepo, karani itabidi aulizie muda ambao mkuu wa kaya atarudi nyumbani hata kama ni usiku na kurudi kuendelea na dodoso.
 
Gharama kubwa sana imetumika kwenye zoezi hili. Kww unyeti wake, naunga mkono hoja. Kuna watu wanakaa kwenye nyumba zakupanga, wakiondoka kwenda kazini hakuna wakumuacha nyumbani. Ni vzr siku hiyo ikapewa hadhi zaidi na kiwa siku maalum ya watu kubaki nyumbani na kutoa ushirikiano kwa hao maafisa. Labda serikali ingesema, utakuwa mapumziko ila baada ya kuhesabiwa utakuwa huru kuendelea na shughuli zako nyingine
 
Ndugu wana jamvi nmeona Serikali imetoa taarifa kuwa Ile siku inayotangazwa Sana ya Sensa kuwa sio siku ya mapumziko. Kiukweli niseme serikali inakosea Sana na haitapata taarifa sahihi kabisa.

Kuna Baadhi ya nyumba hakuna anaebaki Nyumbani hivyo hata wakienda kesho yake hawatakuta mtu maana wote wanaenda kazini.

Pia wanasema ukiondoka uache taarifa zako Kwa anaebaki. Hilo ni ngumu Kwa vile sio Kila niliepanga nae ninamuamini kiasi cha kueza kumuachia taarifa zangu zote binafsi.

Pia Kwa wale walio na wadada wa kazi haiwezekani kuanza kumuambia mdada wa kazi taarifa zangu na familia Kwa ujumla maana ni kama kuwa wazi sasa kitu ambacho sio wote tupo tayari.

Pia hawajasema ni taarifa zipi ambazo zinatakiwa kuachwa ili wakija waweze jibiwa maana tangazo linasema Tu taarifa ziachwe Nyumbani.

Naishauri serikali hiyo siku waifanye iwe ya mapumziko ili kuondoa hizi dosari lasivyo watapata taarifa potofu kuwa tumefika 67m kumbe tupo pungufu

View attachment 2326622

View attachment 2326626
Jf inatisha ! Ushauri wako umechukuliwa wote bila kubakisha chochote
 
Wewe serikali yako imeona ni sawa ,acha taifa likawajibike maana ukipiga hesabu siku ya sensa ni kuanzia tarehe 23 August mpaka 31 August sasa siku zote hizo watu wapumzike na taifa litajengwa na wakina nani
 
Taarifa za leo hii ni kwamba Diblo dibala aka Katelephone amesema kuwa mama yao kakubali kwamba siku hiyo iwe ya mapumziko, wanabishaga saaaana baadae wanakuja kukubali hasa kama hoja husika imetolewa na upinzani yaani watakomaa hata kama ndio ukweli halisi ili wasionekane hawajui, Shame mkahesabiwe ndugu zangu wanatozonia!
 
Back
Top Bottom