dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 23,782
- 54,213
... hivi kuna ugumu gani kuweka hilo dodoso public tukajiandaa na hayo maswali yao?Inasemekana Dodoso (Questionnaire) lina maswali zaidi ya 100 ambayo hatuyajui yatahusu nini. Hivi kweli naweza kubuni vitu zaidi ya 100 watakavyouliza zaidi nikamfahamisha beki 3 na asisahau hata kimoja kweli??
Sioni ni kwa namna gani nitamruhusu msichana wa kazi na wanangu wadogo wafungue geti eti karani wa sensa aingie in my absence; hicho kitu hakipo.
Kwa kitu muhimu kama sensa kinachotokea mara moja in 10 years kuna ugumu gani watu wakabaki majumbani ili zoezi lifanikiwe?
Ni ajabu sana CCM hawajafanya kitu kikaenda successfully bila dosari za kijinga. Kama issue ni watu kutakiwa kwenda kuchapa kazi, busara ilikuwa sensa ifanyike siku ya Nane Nane, 2022; au Nane Nane, 2022 iwe siku ya kazi kutoa nafasi kwa siku ya sensa watu kuwa majumbani kwao.
Alternatively, wangefanya Jumapili lingefanikiwa zaidi. Kwa akili zao hawakuona umuhimu huo - zoezi linaenda kufeli kwa kiwango kikubwa.