Mwajuma wewe mchakarikaji?
hapana. Wewe je?
Nachakarika kama sina akili nzuri ila staki unipige mzinga, sawa Mwajei?
jitahidi kusoma posti zote kwa tuo, ni ushauri tu
kwa hiyo tuseme ili kukidhi haja ya mfumo dume lazima mwanume awe na kipato zaidi ya mke wake?
Baada ya makuzi mema yanayopingana na mfumo dume sasa ni wakati wa kuuangalia upande wa pili wa shilingi. Kwanza kabisa tafsiri ya neno patriarchy ambalo wanaharakati wa jinsia wanadai ni mfumo dume sio sahihi. Tafsiri yake halisi ni ubaba. Hii ni hali ya uongozi ama utawala uliojikita katika baba akisaidiwa ama kusaidiana na mama.
Wanaokubaliana na patriarchy inayotafsiriwa kama ubaba wanaamini kazi kubwa ya ubaba ni 'p' tatu yaani protecting (kulinda), providing (kutoa) na preside (kuongoza) japo wapo wanaodai p ya tatu ni profess (kuaminisha). Kama tulivyoona kwenye mjadala wa maamuzi, mapenzi hayawezi kwenda bila ubaba huu wa kuongoza, kulinda na kutoa.
Pamoja na kupinga ukatili wa mfumo dume ukweli ndio huo, ili mapenzi yafanikiwe lazima ubaba uongoze. Na tunapoongelea kutoa tunaongelea pesa - bila fedha penzi linakuwa mahututi na mwisho wake ni kufa tu. Pesa posa.
Ila mie naona mwanamke anaweza akamzidi mwanamme kipato.
Uko sawa kabisa kaka, pesa ni kati ya misingi ya mapenzi tuachane na mambo ya fairy tales na tamthilia.
kwa hiyo tuseme ili kukidhi haja ya mfumo dume lazima mwanume awe na kipato zaidi ya mke wake?
eti ndo wanasema hivyo.
Ila mie naona mwanamke anaweza akamzidi mwanamme kipato.
Ila kama mwanamme ana akili ya kiume bado huwa hapotezi sifa sifa yake ya ubaba.
Anaongoza familia kama kawaida na nafasi yake inakuwa pale pale.
Mwanamme ni kichwani zaidi, kama zimo za kiume hata umzidi pesa hivi haumpelekeshi.
Kuchakarika bana ndo mpango mzima kwa mwanamke na mwanamme...Mwanamme kuwa na kipato zaidi ya mwanamke ndo mpango mzima.....
Lazima dume achakarike kuhakikisha anampita mwanamke kipato
Kwa nini?Hiyo hapana aisee. Mara nyingi hali ikiwa hivyo huo uhusiano utakuwa hati hati.
Mwanamke anahitaji kuwa na uhakika wa kesho...kwamba atakula, watoto watasoma nk
Kwa nini?
Pesa sio msingi lakini ni muhimu kwa kiasi chake
Wanaume wengi hawapendi kuona hawawezi ku-provide kwa wake zao.
Enzi za babu zako ardhi,ng'ombe,mbuzi etc ndo vilikuwa msingi wa mapenzi for a simple reason kwamba in those yesteryears those items were the currency of the day.No money no love bana asikudanganye mtu,binadamu haishi kwa longolongo bana anaishi kwa mkate (and of course pia kwa a good action in the sack!).Kwangu fedha siyo "msingi mkuu wa mapenzi". Labda kwako na kwa wengine, lakini kwa baadhi ya watu wa karibu niwajuao mimi wakiwemo babu na bibi zangu sikuwahi kusikia wala kuona katika matendo yao kuwa fedha ndiyo msingi wao mkuu wa mapenzi yao.
Enzi za babu zako ardhi,ng'ombe,mbuzi etc ndo vilikuwa msingi wa mapenzi for a simple reason kwamba in those yesteryears those items were the currency of the day.No money no love bana asikudanganye mtu,binadamu haishi kwa longolongo bana anaishi kwa mkate (and of course pia kwa a good action in the sack!).