Umuhimu wa Mfumo Dume (Ubaba)

Umuhimu wa Mfumo Dume (Ubaba)

kwa hiyo tuseme ili kukidhi haja ya mfumo dume lazima mwanume awe na kipato zaidi ya mke wake?
 
eti ndo wanasema hivyo.

Ila mie naona mwanamke anaweza akamzidi mwanamme kipato.
Ila kama mwanamme ana akili ya kiume bado huwa hapotezi sifa sifa yake ya ubaba.

Anaongoza familia kama kawaida na nafasi yake inakuwa pale pale.

Mwanamme ni kichwani zaidi, kama zimo za kiume hata umzidi pesa hivi haumpelekeshi.

kwa hiyo tuseme ili kukidhi haja ya mfumo dume lazima mwanume awe na kipato zaidi ya mke wake?
 
Baada ya makuzi mema yanayopingana na mfumo dume sasa ni wakati wa kuuangalia upande wa pili wa shilingi. Kwanza kabisa tafsiri ya neno patriarchy ambalo wanaharakati wa jinsia wanadai ni mfumo dume sio sahihi. Tafsiri yake halisi ni ubaba. Hii ni hali ya uongozi ama utawala uliojikita katika baba akisaidiwa ama kusaidiana na mama.

Wanaokubaliana na patriarchy inayotafsiriwa kama ubaba wanaamini kazi kubwa ya ubaba ni 'p' tatu yaani protecting (kulinda), providing (kutoa) na preside (kuongoza) japo wapo wanaodai p ya tatu ni profess (kuaminisha). Kama tulivyoona kwenye mjadala wa maamuzi, mapenzi hayawezi kwenda bila ubaba huu wa kuongoza, kulinda na kutoa.

Pamoja na kupinga ukatili wa mfumo dume ukweli ndio huo, ili mapenzi yafanikiwe lazima ubaba uongoze. Na tunapoongelea kutoa tunaongelea pesa - bila fedha penzi linakuwa mahututi na mwisho wake ni kufa tu. Pesa posa.

Uko sawa kabisa kaka, pesa ni kati ya misingi ya mapenzi tuachane na mambo ya fairy tales na tamthilia.
Hawa wanaodai hawaangalii pesa kuna siku humu wamesema hawapendi wanaume wanaobeep kwenye simu.
Kama huwezi provide, protect, bila shaka msichana atakuchoka hata kama mwanzo alikuwa anakupenda ila mwisho atakuona mzigo.
Kuna familia kibao unakuta mwanzo mwanaume alikuwa na kazi mambo yalikuwa safi na mke alikuwa anampenda, kazi kafukuzwa hawezi timiza yale ya mwanzo mwanake kamkimbia au hampi upendo na heshima ya kama mwanzo.
In reality ela ina nafasi yake katika mapenzi.
 
Uko sawa kabisa kaka, pesa ni kati ya misingi ya mapenzi tuachane na mambo ya fairy tales na tamthilia.

Wewe unasema pesa ni "kati" ya misingi ya mapenzi. Companero anasema pesa ndiyo "msingi mkuu" wa mapenzi. Unaona tofauti hapo?
 
kwa hiyo tuseme ili kukidhi haja ya mfumo dume lazima mwanume awe na kipato zaidi ya mke wake?

Mwanamme kuwa na kipato zaidi ya mwanamke ndo mpango mzima.....

Lazima dume achakarike kuhakikisha anampita mwanamke kipato
 
eti ndo wanasema hivyo.

Ila mie naona mwanamke anaweza akamzidi mwanamme kipato.
Ila kama mwanamme ana akili ya kiume bado huwa hapotezi sifa sifa yake ya ubaba.

Anaongoza familia kama kawaida na nafasi yake inakuwa pale pale.

Mwanamme ni kichwani zaidi, kama zimo za kiume hata umzidi pesa hivi haumpelekeshi.

Pesa inakuwa msingi tu kama uhusiano ni wa kinafiki/usanii. Kama mwanzo sikusukumwa na pesha kumpenda basi hico kilichonisukuma kitabaki kuwa msingi kwenye mapenzi yangu...

Bado sijashawishika kuhusu pesa kwa sababu its not the primary thing I look into a man...

Labda tuache tu iwe kila mmoja ana msingi ambao kwao mapenzi yake na mwenza wake yamejengeka.
 
Mwanamme kuwa na kipato zaidi ya mwanamke ndo mpango mzima.....

Lazima dume achakarike kuhakikisha anampita mwanamke kipato
Kuchakarika bana ndo mpango mzima kwa mwanamke na mwanamme...

Nani anataka mwenza mvivu asiyepigania maisha? Lakini hamjanishawishi kwa kusema pesa ndo msingi....yapo mengi ya msingi kwenye mahusiano.

Wewe upo tayari kuishi na mume milionea amabye hakuheshimu?
 
piga ua galagaza ..... Pesa ni muhimu...
Mwanamke anahitaji kuwa na uhakika wa kesho...kwamba atakula, watoto watasoma nk

huitaji kuwa tajiri..... Unahitaji kuwa na pesa ya kuyimiza mahitaji. Na hupendeza zaidi mwanaume akiwa na kipato kumzidi mwanamke........

Unafikiri bila pesa, njaa tumboni hapo hata mapenzi yananoga?
 
Pesa sio msingi lakini ni muhimu kwa kiasi chake

Wanaume wengi hawapendi kuona hawawezi ku-provide kwa wake zao.
 
Kwangu fedha siyo "msingi mkuu wa mapenzi". Labda kwako na kwa wengine, lakini kwa baadhi ya watu wa karibu niwajuao mimi wakiwemo babu na bibi zangu sikuwahi kusikia wala kuona katika matendo yao kuwa fedha ndiyo msingi wao mkuu wa mapenzi yao.
Enzi za babu zako ardhi,ng'ombe,mbuzi etc ndo vilikuwa msingi wa mapenzi for a simple reason kwamba in those yesteryears those items were the currency of the day.No money no love bana asikudanganye mtu,binadamu haishi kwa longolongo bana anaishi kwa mkate (and of course pia kwa a good action in the sack!).
 
Fine, but just speak for yourself coz not everybody puts money ahead of everything.
 
Back
Top Bottom